Ushauri: Kama una mke au binti nyumbani kwako mshauri aache tabia ya kuposti picha zake mtandaoni


Kweli kabisa Mwamuzi wa Tanzania . Kuna kisa kimoja kilitokea marekani. Kijana wa kiume wa miaka kati ya 17 & 19 alikuwa akichati na mtu mwingine feki (aliyejifanya mwanamke), ambaye baadaye ilikuja kujulikana alikuwa ni kijana wa miaka kati ya 19 & 21. Sasa wakawa wana wasiliana kwa jumbe za kawaida. Baadaye wakaanza kuwasiliana kwa jumbe za kimahaba. Baadaye yule binti feki akawa hata anamtumia picha za utupu. Hata video, sasa sijui ndiyo zile unazosema wanazichota mtandaoni!!? Baada ya muda, yule kijana ambaye siyo feki naye akaanza kutuma picha na video za utupu. Yule binti feki alivyojiridhisha kwamba sasa ana picha ambazo siyo feki na kijana ambaye siyo feki, akamtisha kwamba hizi picha zako za hovyo ulizonitumia zita go viral kama hutanilipa kiasi fulani cha dolari. Yule kijana alivyojua katapeliwa, ikabidi afanye maarifa ili amlipe yule mtu zile pesa. Haikuishia hapo, akawa mara kwa mara akimtaka alipe pesa vinginevyo anazipeperusha picha hizo hewani kama manyoya (na sijui kuna yeyote ambaye ataweza kuyakusanya tena hayo manyoa). Hiyo ikampelekea kijana huyo kuwa na sonona na stress nyingi. Mama yake (ambaye alikuwa singo maza kwa mtoto huyo pekee), anaeleza kwamba ghafla hali ya kijana wake ikabadilika, akawa ni kijana mkimwa, hachangamki, anapenda kujitenga muda mwingi. Akiulizwa nini kina msibu, hasemi. Kilichotokea baada ya muda mfupi, yule kijana akajiua. Walivyoanza kufuatilia ndiyo wakagundua haya niliyoyaeleza. Kwa kweli vijana wetu tunahitaji kuwaasa sana na mambo ya cyber (bullying). Siyo madogo au rahisi kama tunavyodhani
 
Kuna binti mmoja hua tunaheshimiana sana hapa mtaani, katika pitapita zangu mitandaoni nikabahatika kukutana na A/c kwenye mitandao ya jamii imejaa picha zake halafu imewekwa mpaka bei elekezi.
Kuanzia siku ile heshima kwa yule binti nimeishusha kwa asilimia kubwa sana.
Huenda kuna mtu unatumia picha zake pasi na yeye kujua au inawezekana ni yeye mwenyewe kaamua kufungua biashara mtandaoni, ila maisha halisi tunayoishi nae hapa mtaani hayaendani hata kidogo na kile nilichokiona mtandaoni.
 
Aisee hiki kisa sijawahi kukisikia ila ni kizito sana.
Dunia iko kasi
 
Yawezekana wagalatia wamepita naye while yeye hajui chochote
 
Ilo kupost ni lazima. Mwanamke akipendeze au akienda sehem nzuri wengi lazima aonyeshe na wengine mtandaoni. It's nature
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…