Ushauri: Kama unataka kulamba asali bila wasiwasi soma degree ya manunuzi

Ushauri: Kama unataka kulamba asali bila wasiwasi soma degree ya manunuzi

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!
Waswahili wanasema kama huwezi kuwapiga basi ungana nao ili nawe uanze kuwapiga maadui ambao awali mlikuwa marafiki.
Uza hata mashamba, achana na kufanya vitu visivyoleta tija.
Ukiingia serikalini umeula, yaani ni mwendo wa kula asali tu.
Box la peni serikalini linauzwa mpaka elfu 50, bunda la karatasi 60 mpaka laki.
Tofali ya kawaida tu inauzwa mpaka elfu 5.
Vijana uzeni mashamba yenu ya urithi someeni procurement.
Pambana upate ka degree inatosha unadubiri ajira, ikiwezekana kapange hata nyumba ya tope Dodoma ili uhudhurie usaili mara kwa mara , ndani ya miaka 2 lazima utapata kazi uanze kulamba asali
 
Thubutuuuuu manunuzi yapi hayo, labda upate kazi huku tozoniani vinginevyo kwa wahindi ama wachina utajuta kuzaliwa , yani akupe wewe vitu vyake ukanunue , wale kila kitu wananunua wenyewe na kibaya zaidi wananunua kwa wenzao tu we mwenzangu na mimi itakula kwako huli hata mia, tafuta cha kufanya hasa biashara mambo ya sijui kutafuta ajira katika taasisi gani za umma ni kujichosha tu kwanza nafasi hamna, pili lazima uwe na connection na kadi ya chama kileeee , jikite kwenye business tu ndio kilichobakia mtakuja kunishukuru sana baadaye.
 
Una weza kusoma hiyo kozi na ukaishia kufwafwanzika.

Anakujua nani huko tozoniani?
 
Ndugu yangu mmoja alidanganyika na degree ya manunuzi.... shughuli ilikuwa kupata hiyo kazi! Ajira hakuna na hata kujiajiri ni almost impossible.

Kabla ya kusoma kitu jiulize

1. Soko lake la ajira
2. Uwezekano wa kujiajiri mwenyewe.
 
Ilikuwa zamani sio Sasa hao wenye hio niko nao tunalima nao vitunguu huku
 
Ndugu yangu kasoma hiyo procurement and supply miaka 7 sasa hajapata ajira,ameamua kufanya kazi ndogondogo za kumuingizia kipato nje ya fani
 
Back
Top Bottom