Ushauri kati ya hizi gari wanajamvi

Ushauri kati ya hizi gari wanajamvi

Bandarini c-class ni 7-9mil ambayo inalingana kabisa na Crown. labda gharama za maintanance nazo nadhani sio za kutisha.
 
Mm nakushauri uchukue ya kwanza ambayo ni toyota Crown Athlete.

Kwa sababu hizi, nikirejea kwenye thread yko, unadai kwamba hiyo ndio gari yako ya kwanza ya luxury.

Siku zote ukitaka uvipende vitu vizuri basi sharti udumu navyo na pia visikuchoshe na wala ww mwenyewe usivichoshe.

Pili Toyota ni rafiki wa mazingira yetu ya kiafrica, nikiwa na Maana kwmb, kwa upande wa spare zake ni reliable, service yake unaweza kuifanya kwa urahisi na pia kwa muundo wa ndani wa athlete ni mzuri Mara mia ya Benz.

Shida ya benz ni kwmb vifaa vyke kwanza ni mama mkwe, Service yke sio lelemama, ukimpata fundi wa kiaina unaweza ukajikuta umeingia loss kubwa
Asante sana kaka, ushauri mzuri.
 
chukua crown though cjajua ya mwaka gani but kwa mazingira yetu ya tanzania utaweza kuimudu vizuri tu,ingawaje engine yake ni kubwa kidogo 2.5 V6 ila ulaji ni wa kawaida tu,crown ni luxurious ina power ya kutosha na spacious too..

kama ulivyosema hali ya sasa ngumu usichukue gari una ipark mahali roho inakuwa juu juu,coz spare part na maintanance ya benz iko juu.go for crown 212HP alternative yake ni mark x same engine ila body tofauti tu.
 
Tafuta BMW 7 series ya mwaka 2004 hebu, hao wote vikaragosi.
 
Back
Top Bottom