Ushauri: Kichanga wangu analia sana usiku

Ushauri: Kichanga wangu analia sana usiku

aliyetegwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
313
Reaction score
486
Mwanangu anaumri wa miezi miwili, kipindi cha nyuma mambo yalikua shwari hakua na tabia ya kulia usiku hivi karibuni tabia yake imebadilika na usiku wa kuamkia leo ndo imekua funga kazi, mtoto ameanza kulia gafla kilio kikali kilichojaa uchungu ndani yake kwa sauti ya juu sana.

Kitu kilichofanya mwili wake upoe na awe akitoka jasho kila sehemu ya mwili wake kama amemwagiwa maji, ilikua ni hali inayoongopesha sana maana tulibembeleza na kuembeleza baada ya mda mrefu alinyamaza kwa kupitiwa usingizi mwili wake ukiwa umechoka sana.

Hana ugojwa wala haumwi popote maana mda wa mchana anakua mchangamfu na mwenye afya tele ila usiku hulia kwa kiasi cha juu sana naombeni ushauri kwa yeyote aliyewahi kukutana na hali hii ama mwenye kujua nini kifanyike kukomesha hali hii.
Natanguliza shukurani.
 
Ndio njia pekee mtoto anaweza kuwasiliana na wanaomlea aweze kupata msaada ndivyo anavyowasilisha woga wake, maumivu yake ya tumbo ( Mara nyingi kutokana na kujaa gesi) , njaa , kulowana kwa mavazi yake n.k.

Mnyonyeshe vya kutosha ( ideally kila baada ya Massa 2), ukiwa na mtoto wa umri huo usilale gizani ili anaamka mwanga uwepo ( ingawa hawaoni uzuri mbali but mwanga ukiwapo woga hupungua),

Ukihisi ni maumivu ya tumbo kujaa gesi weka tumbo began au mchezeshe miguu juu chini na kumminya vidole vya miguu taratibu, pia waweza kutumia maji special yaka kupunguza gasi kulingana na Dr atakavyokushsuri na upatikanaji wake.

Kulia usiku kwa mtoto wa umri huu inafikirika kuwa ni survival mechanism anaifanya unconsciously but ni njia mojawapo ya kudelay kuzaliwa mtoto mwingine, ikumbukwe mtoto mwingine akizaliwa mapema care yake na lishe vinakuwa mashakani.

Kwa Julia na kumsumbua mama usiku , mama anakuwa stressed, ovulation very unlikely kutokea kwa hiyo mimba za haraka/ chapchap zinahairishwa. Hata mgegedo pia sio rahisi nyakati za stress.

Kwa msaada zaidi na uelewa mpana, Fanya matumizi sahihi ya smart phone yako - google " why news babies cry at night" , utapata maarifa ya kutosha ya kukusaidia wewe na wengine ili kuepukana na swaga za anaona vibwengo au anataka jina la babu.
Jpili njema.
 
A) Mtoto wangu wakiume alitusumbua sana usiku hatukuwa tunalala kwa kulia tulibadilishana, sasa amekuwa ya darasa la nne.

Siku moja kwa kuchoshwa nikampa maji ya yaliyopowa akiwa mchanga wa mwezi mmoja yalikuwa ya chai nikapoza yakabaki na uvuguvugu kidogo

Nikamuwekea mdomoni aliyafakamia kichizi na baada ya hapo akalala mpaka asubuhi nikajuwa njaaa muda wote nikimpa vimaji wife amelala kwa uchovu wakubembeleza tulikuwa tunapeana zamu

Ilipofika asubuhi nikaenda kununua maziwa special ya watoto Aspen one.kwa wachanga chini ya miezi 6 na Aspen two kwa walio zaid nikamsimulia wife yaliyotokea usiku.

Ikawa tunayaandaa maziwa na ile chupa ya kunyonya akianza kulia anapewa maziwa ananyonyaaa akishiba basi analala mpaka asubuhi

Nb: chupa yakumnyonyeshea mtoto kila siku ichemshe kwenye maji ya moto kabisa kama ya chai kuuwa vijidudu...chupa na vifaa vyake vyote.mifuniko nk.....otherwise atapata magonjwa ndani ya muda mfupi kama kuharisha au kuumwa tumbo, nk

B) Hakikisha mtoto halali na nguo mbichi zenye mkojo mkojo huwasha sana kila wakati mkaguwe awe mkavu

C) Hakikisha unampeleka hospitali kuthibitisha kweli yuko salama na hana matatizo mengine.

D) Usithubutu kulala na mwanao mchanga ukiwa umetoka kufanya mapenzi nje ya mkeo kwa wanaume hakika mtoto atawasumbuwa sana, ukifanya uchepukaji usimshike mtoto wala kulala kwenye eneo lake kaa mbali kabisa na kichanga

Kwa wanawake vilevile jitahidi kulea mtoto mpaka akuwe, ukiwa nakichanga, mpe baba halisi tu hiyo mashine sio vinginevo ukigawa kwa baba asiye wa kichanga hakika utauguza nakutaabika sana

Sielewi kwanini hii D) ni suala la itikadi na imani lakini nikweli it works 100% ukitaka uepuke mateso ya kuuguza mtoto nakukesha usiku usipuuze kwa wababa ukichepuka jitenge na mama na kichanga oga vilivyo

Kwa leo ni hayo tu ndimi mzazi mwaminifu Adolay
 
Kiu ya maji nayo inasababisha mtoto kulia usiku mwanangu akiwa na umri huo, alitusumbua sana usiku mpaka nikawa na wasiwasi na mahali nilipopanga mama yake kila akijaribu kumnyonyesha, mtoto hataki ziwa

Siku moja nikaamua kumpa maji ya kunywa, hakika hakusumbua mpaka asubuhi kawa ndo mchezo wangu akilia tu usiku, naamka kumuwekea maji kwenye chupa yake mpaka leo ana mwaka mmoja hajawahi kusumbua kwa kitu kingine zaidi ya kiu
 
Una maabara ndani au wewe ni daktari kujua kuwa hana ugonjwa wowote ushauri wangu muwahishe mtoto hospitali huko utapata majibu sahihi sio hapa pole kwa mkesha.
 
Ni kawaida ya watoto hata mwanangu alikuwa analia usiku ila saizi katulia.
 
Nakushauri yafuatayo.
Angalia mahusiano yako na mzazi au mmeo angalia uhalisia wa mtoto huyo baba yake halisi ni yupi washirikishe wazazi upande wa huyo mtoto hata kama wako mbali kuna maneno wakisema yaweza kuwa tiba si uchawi ni tamaduni tu ni ushauri siyo sheria ikufunge.
 
Mwanangu anaumri wa miezi miwili, kipindi cha nyuma mambo yalikua shwari hakua na tabia ya kulia usiku hivi karibuni tabia yake imebadilika na usiku wa kuamkia leo ndo imekua funga kazi, mtoto ameanza kulia ghafula kilio kikali kilichojaa uchungu ndani yake kwa sauti ya juu sana kitu kilichofanya mwili wake upoe na awe akitoka jasho kila sehemu ya mwili wake kama amemwagiwa maji, ilikua ni hali inayoongopesha sana maana tulibembeleza na kubembeleza. Baada ya mda mrefu alinyamaza kwa kupitiwa usingizi mwili wake ukiwa umechoka sana.
Hana ugojwa wala haumwi popote maana mda wa mchana anakua mchangamfu na mwenye afya tele ila usiku hulia kwa kiasi cha juu sana.
Naombeni ushauri kwa yeyote aliyewahi kukutana na hali hii ama mwenye kujua nini kifanyike kukomesha hali hii.
Natanguliza shukurani.
Kwanza unaishi wapi kama ni dar basi huyo mtoto hutakiwi kumvisha nguo nyingi usiku kikubwa kinacho mliza mtoto itakuwa ni joto unatakiwa kujua unavyo sikia wewe kwenye hali ya hewa na mtoto hujisikia hivyo sio wewe unasikia joto lakini mtoto unamgubika nguo nyingi kingine je anapata maziwa ya kutosha?
 
Nakushauri yafuatayo.
Angalia mahusiano yako na mzazi au mmeo. Angalia uhalisia wa mtoto huyo baba yake halisi ni yupi. Washirikishe wazazi upande wa huyo mtoto hata kama wako mbali kuna maneno wakisema yaweza kuwa tiba. Si uchawi ni tamaduni tu. Ni ushauri siyo sheria ikufunge.
Una watoto wewe?
 
Nakushauri yafuatayo.
Angalia mahusiano yako na mzazi au mmeo. Angalia uhalisia wa mtoto huyo baba yake halisi ni yupi. Washirikishe wazazi upande wa huyo mtoto hata kama wako mbali kuna maneno wakisema yaweza kuwa tiba. Si uchawi ni tamaduni tu. Ni ushauri siyo sheria ikufunge.
Duuh..! Watoto kulia ni kawaida mkuu,ampeleke tu hospital kuchekiwa

Hayo mengime hapana ni kumpoteza kabisa.
 
Pole sana, ni kawaida watoto wa rika hilo kulia usiku, ila kama waona kazidisha sana angalia mazingira anapolala, je joto sana? hewa nzito? anavalishwa nguo nyingi usiku? njaa? Maana kumbuka anakua kwahiyo ulaji nawo unaongezeka, tengeneza maziwa ya powder usiku, yawe kwenye warmer au sufiria yenye maji moto, akilia tu uumpe lazima kuna kitu kinamsumbuwa, kama siyo mikojo, haja au la tafadhali usiende kwa matapeli yaani waganga wa kienyeji, nenda kwa daktari wa watoto kwa ushauri zaidi, yataisha tu na atakua vizuri tu.
 
Nina binti angu sasa ana umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu kanatembea sasa

Nakumbuka hakuna kipindi nilichoteseka kama baba ndani pindi ana umri wa miezi mitatu,alikuwa analia balaa usiku mamake nilikuwa namwonea huruma maana halali

Ikabidi niende hospitali lakini wakaniambia hapo hana tatizo ni stage tu ya ukuuaji

Ikabidi nibadili ratiba,saa kumi na moja jioni nalala nikitoka job,saa mbili usiku naamka naanza kufanya kazi za kiofisi huku namsubiri aanzishe timbwili nianze kumbembeleza

Tabia hii ipo mpka sasa kwa umri huu wake,lakini si kama kipindi kile
 
Watoto usiku huwa wanaona mengi mkuu , vitu vya kutisha hasa wakati wa kulala uwe unampakaa wanja katika nyuso zake " mi wa kwangu pia alikuwa hivo lakini nilvokuwa nampaka wanja hakuwa anasumbua tena .
 
Back
Top Bottom