aliyetegwa
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 313
- 486
Mwanangu anaumri wa miezi miwili, kipindi cha nyuma mambo yalikua shwari hakua na tabia ya kulia usiku hivi karibuni tabia yake imebadilika na usiku wa kuamkia leo ndo imekua funga kazi, mtoto ameanza kulia gafla kilio kikali kilichojaa uchungu ndani yake kwa sauti ya juu sana.
Kitu kilichofanya mwili wake upoe na awe akitoka jasho kila sehemu ya mwili wake kama amemwagiwa maji, ilikua ni hali inayoongopesha sana maana tulibembeleza na kuembeleza baada ya mda mrefu alinyamaza kwa kupitiwa usingizi mwili wake ukiwa umechoka sana.
Hana ugojwa wala haumwi popote maana mda wa mchana anakua mchangamfu na mwenye afya tele ila usiku hulia kwa kiasi cha juu sana naombeni ushauri kwa yeyote aliyewahi kukutana na hali hii ama mwenye kujua nini kifanyike kukomesha hali hii.
Natanguliza shukurani.