Ushauri kuhusu biashara ya bodaboda ‘za mkataba’

Ushauri kuhusu biashara ya bodaboda ‘za mkataba’

Biashara pasua kichwa hiyo ni sawa na kujaza maji kwenye tenga.
Ipo hivi pikipiki aina ya boxer inauzwa mil 2.8, hesabu ya siku unaletewa elfu 10 na mkataba kwa kawaida ni miezi 13..ukiwa unaletewa kila siku elfu 10 kwa mwezi utakuwa umeingiza laki 3,laki 3*13=3900000
3900000-2800000=1100000
Faida kwa mwaka mzima unapata mil 1.1
1100000÷13=84615...
Unatoa mil 2.8 mfukoni halafu kwa mwezi faida unaingiza elfu 84615 kama sio utahaira ni nini? Na mwisho wa siku pikipiki inakuwa sio yako tena

NB: Hapo bado haujapewa taarifa ya kuibiwa pikipiki, service ikiwa kubwa ni juu ya boss
Kichaa kwelikweli
 
Back
Top Bottom