Kinjekitile Jr
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 566
- 1,583
me pia nipo kwenye hali kama ya kwako mkuu........kuna binti mzuri kiukweli ana miaka 20[ninamzidi kama miaka 5] kwa sasa ila ananipenda sana na yupo radhi afanye chochote ili tu kunifurahishaWakuu habarini za asubuhi.
Kama kijielezavyo kichwa cha habari hapo juu, hekima zenu zinahitajika kutoa ushauri juu ya jambo naloenda lielezea hapa chini.
Mathalan una mchumba na umekwishamtolea barua na ushaanza mlipia mahari lakini siku zijazo ukakutana na binti mwenye sifa kuliko mchumba uliyemtolea barua.
Na huyo binti akakupenda akawa radhi kuolewa hata mke wa pili au wa tatu, pia kwa uwezo aliokuwa nao ni binti aliyeonesha willing ya kukusapoti katika harakati zako za kibiashara na akaanza kufanya hivyo kwa kuwekeza fedha zake kwako na akawa yuko willing kukupa uongoze anavyomiliki.
- Binti wa pili uliyekutana nae sifa zake ni uzuri, familia yenye nguvu kiuchumi, yeye mwenyewe ana nguvu kiuchumi pia yuko romantic kupitiliza. Ila kiumri amekuzidi kama miaka miwili. Kasoro zake ni anadeka sana na yuko sensitive sana kitu kidogo analia, pia mkigombana hachelewi kujaribu kujiua yani ana maamuzi ya kujiumiza.
- Na kwa yule binti unayetarajia kumuoa uliyemposa ni mzuri pia, uchumi hana yeye wala familia yake, ni mdogo sana kiumri kwako yani ni teenager (miaka 19) pia hata kimaamuzi ni mdogo/mtoto.
Kasoro zake ana maamuzi ya kukurupuka, ana mihemko sana, mropokaji pia ana hasira kupitiliza.
Kwa wewe utachukua uamuzi upi? Je, utaendelea na mbachao ama utafuata mswala upitao uufanye mbachao!?
Na ukizingatia bado miezi mitano ndoa yako na uliyemposa ifanyike.
Na uliyekutana nae licha ya kujua una mtu tena umemwambia una mke kabisa yeye ameridhia kuwa mke wa pili.
ana mambo ya kitoto kidogo kwa mfano hawezi kukushauri jambo lolote la kimaisha zaidi akili yake ime-base kwenye sex tu na kuwaza mambo mengi kuhusu kuoana
ila kuna pisi nyingine ni mwalimu wa secondary na inanipenda kuliko maelezo ananisaidia mambo mengi sana,jana katoka kunilipia ada ya masomo ili niendelee na masomo.......kiukweli ni mtu anaye nipa kampani sana kwenye harakati zangu za kimaisha na kamwe hawezi kuniona nasononeka kivyovyote vile........bado sijamwambia kuwa alinikuta na mahusiano mengine ila ashanifumania nachat na kale kabint aliumia sana,akanambia nifanye yote ila nisijaribu kumuacha
kiukweli nipo njia panda kama ya kwako