Ushauri kuhusu mabinti wawili nilio nao kwenye mahusiano

Ushauri kuhusu mabinti wawili nilio nao kwenye mahusiano

Wakuu habarini za asubuhi.

Kama kijielezavyo kichwa cha habari hapo juu, hekima zenu zinahitajika kutoa ushauri juu ya jambo naloenda lielezea hapa chini.

Mathalan una mchumba na umekwishamtolea barua na ushaanza mlipia mahari lakini siku zijazo ukakutana na binti mwenye sifa kuliko mchumba uliyemtolea barua.

Na huyo binti akakupenda akawa radhi kuolewa hata mke wa pili au wa tatu, pia kwa uwezo aliokuwa nao ni binti aliyeonesha willing ya kukusapoti katika harakati zako za kibiashara na akaanza kufanya hivyo kwa kuwekeza fedha zake kwako na akawa yuko willing kukupa uongoze anavyomiliki.

- Binti wa pili uliyekutana nae sifa zake ni uzuri, familia yenye nguvu kiuchumi, yeye mwenyewe ana nguvu kiuchumi pia yuko romantic kupitiliza. Ila kiumri amekuzidi kama miaka miwili. Kasoro zake ni anadeka sana na yuko sensitive sana kitu kidogo analia, pia mkigombana hachelewi kujaribu kujiua yani ana maamuzi ya kujiumiza.

- Na kwa yule binti unayetarajia kumuoa uliyemposa ni mzuri pia, uchumi hana yeye wala familia yake, ni mdogo sana kiumri kwako yani ni teenager (miaka 19) pia hata kimaamuzi ni mdogo/mtoto.
Kasoro zake ana maamuzi ya kukurupuka, ana mihemko sana, mropokaji pia ana hasira kupitiliza.
Kwa wewe utachukua uamuzi upi? Je, utaendelea na mbachao ama utafuata mswala upitao uufanye mbachao!?

Na ukizingatia bado miezi mitano ndoa yako na uliyemposa ifanyike.

Na uliyekutana nae licha ya kujua una mtu tena umemwambia una mke kabisa yeye ameridhia kuwa mke wa pili.
-'Na kwa yule binti unayetarajia kumuoa'...

Mtu unayemuongelea ni wewe mwenyewe, sasa kwanini unatubebesha mzigo sisi tusiohusika na hiyo stori?
 
-'Na kwa yule binti unayetarajia kumuoa'...

Mtu unayemuongelea ni wewe mwenyewe, sasa kwanini unatubebesha mzigo sisi tusiohusika na hiyo stori?
Mkuu si utoe maoni?
Ila mie nishaoa mkuu japo sijajaaliwa mtoto.
Ila huu mkasa kuna mtu umemkuta nikaona niulete humu.
 
Nafikiria ningekua mimi ningefanyaje? Ila mkuu angalia huyo aliyekuzidi umri, unaweza kuta anafanya vile aingie kwenye ndoa tu, then aoneshe makucha yake. Kingine huyo mdogo kama anakupenda usimteme ni utoto tu bado unamsumbua. Ila huyo mwingine namashaka naye kwanza usikute kashaharibu alikotoka anataka closure tu kwako.
 
Ukimkuta mwanaume anauliza nani amuoe huyo jua sifa za kiume zimeondoka kabisa mwanaume hutumia akili Kwa Kila jambo ila mwanamke hutumia hisia

Sasa huyu mwenzetu kashakuwa ke tunamsaidiaje arudie tabia za kiume
 
Wako wawili tu kaka mwenye umri mkubwa na mdogo ambaye ameshachumbiwa na kutolewa posa.
Hizo ni sifa zao za hao wawili.
 
Ukimkuta mwanaume anauliza nani amuoe huyo jua sifa za kiume zimeondoka kabisa mwanaume hutumia akili Kwa Kila jambo ila mwanamke hutumia hisia

Sasa huyu mwenzetu kashakuwa ke tunamsaidiaje arudie tabia za kiume
Kwani mkuu mwanaume huwezi ukakanganywa kihisia na ukawa kizani kiasi ukahitaji ushauri?
 
Umemuongelea vizuri sana huyo mwenye uchumi ila huyo teenager umemuongelea kihisia tuu [emoji23]
 
Back
Top Bottom