Habari zenu wana JF,
Mimi ni mgeni humu nimekuja kwenu kuomba ushauri na mawazo yenu maana humu kuna wataalamu mbalimbali.
Mama watoto wangu ni mjamzito wa takribani miezi 8 na point na amekuwa akihudhuria kilinic vizuri kabisa.
Alitakiwa kujifungua 09.02.2019 kwa mujibu wa maelezo ya kliniki yake lakini mnamo tarehe 29.01.2019 nikiwa sipo nyumbani alinipigia simu usiku akilalamika kuwa hajamsikia mtoto akicheza tumboni siku nzima.
Nilimpa ushauri awahi hospital haraka na ndipo kesho yake alifanya hivyo lakini baada ya kufanyiwa vipimo iligundulika kiumbe alichobeba kilikuwa tayari kimepoteza maisha.
Daktari alimwambia arudi kwanza nyumbani ili kusubiri siku zake za kujifungua zifike. Hivyo mpaka sasa nabaki njia panda. Je, kama kiumbe tayari kishafia tumboni ina maana ukuaji wake hauendelei mwanamke anawezaje kuja pata uchungu na akajifungua?
Je, hali hiyo ya kukaa na kiumbe mfu tumboni haiwezi mletea madhara mama huyu? Je, hakuna njia nyingine rahisi ya kutumia kuweza kukitoa kuliko kusubiri siku yake ya kujifungua kufika?
Naimani JamiiForums iko na watu wa kila aina na pengne wapo ambao washakumbana na tatizo hili hivyo naombeni ushauri wenu mwenzenu niko njia panda.
Sent using Jamii Forums mobile app