Ushauri kuhusu ukuaji wa kuku wa kienyeji ndani ya wiki 4 hadi 5

Rangooo

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2022
Posts
243
Reaction score
408
Habari ndugu zangu,

Mimi ni kijana niliyeamua kujiajiri rasmi kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara kwa asilimia 100, nimeanza kwanza utafiti kwa kujarbu kusikiliza maoni ya watu ambao tayari weshawahi kufanya ufugaji na kujipatia uzoefu wa kutosha.

Miongoni mwa maswali yangu ni je inawezekana kuanza na kuku wa kienyeji ambao tayr wana wiki tano hadi sita (walioanza kukomaa) na kuanza kuwafuga kisasa (namaanisha kuwapa chakula kisasa zaidi kama kuku wa kisasa na chanjo) na ndani ya wiki nne hadi tano waweze kukua na kuingia sokoni?

Na je kama inawezekana ni hatua zipi zaidi niweze kuchukua?

Na kama haiwezekani ni kwa sababu gani?

Naombeni msaada ndugu zangu
 
Hongera kwa kuwa na wazo kama ilo

Mm nilinunua vifaranga vya kienyeji ambayo vina mwezi mmoja kama 50 then nikavifungia ndani ili vikuwe haraka maana nilikuwa nawapa chakula Cha kuku wa kisasa plus chanjo lkn baada ya week mbili wlianza kushusha mabawa na kupooza siku za mbeleni walianza kufa then walikufa kama 21

Baadae ikabid niwatowe njee Yan niwafuge nusu ndani nusu njee apo ndipo wakaanza kukua nilichogundua kwamba kuku wa kienyeji domestication Yao inachukua muda sana pia ni vigumu kukubali mazingira ya ndani kwa asilimia 100

Kuhusu kuwaingiza sokoni ndani ya week tano sio lahisi Mkuu maana kuku wa kienyeji wanakuwa tayali kuingizwa sokon ndani ya miezi sita kama wakilishwa vizuri

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Mkuu samahani Umewahi kufuga kuku wa kienyeji ila sio kibiashara, namaanisha ata nyumbani tu mmewahi kuwa na kuku?

Nimeuliza kwa sababu inaonekana huna idea kabisa kuhusu kuku wa kienyeji, huwezi kumuita kuku wa kienyeji mwenye week 6 kuwa ameanza kakomaa

Kuku wa kienyeji mwenye week 6 bado ni kifaranga na wengine ata manyoa bado hayajaota sehemu zote za mwili

Kama una uchu sana na kuku wa kienyeji basi utamla at least akiwa na miezi 4 na hapo inategemea na mbegu yake, kama ni mbegu kubwa au mbegu ndogo

Nakushauri, humu njoo kufata ushauri wa kitaalamu zaidi, ila maswali kama hayo unaweza tu kwenda kwa mtu anaefuga kuku wa kienyeji ukamuuliza akakujibu na ukajionea umri wa kuku husika na maumbo yao
 
Hongera kwa kuwa na wazo kama ilo

Mm nilinunua vifaranga vya kienyeji ambayo vina mwezi mmoja kama 50 then nikavifungia ndani ili vikuwe haraka maana nilikuwa nawapa chakula Cha kuku wa kisasa plus chanjo lkn baada ya week mbili wlianza kushusha mabawa na kupooza siku za mbeleni walianza kufa then walikufa kama 21

Baadae ikabid niwatowe njee Yan niwafuge nusu ndani nusu njee apo ndipo wakaanza kukua nilichogundua kwamba kuku wa kienyeji domestication Yao inachukua muda sana pia ni vigumu kukubali mazingira ya ndani kwa asilimia 100

Kuhusu kuwaingiza sokoni ndani ya week tano sio lahisi Mkuu maana kuku wa kienyeji wanakuwa tayali kuingizwa sokon ndani ya miezi sita kama wakilishwa vizuri

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app

Mkuu elezea kidogo hapa jinsi gani uliweza kuwalea nusu nje na nusu ndani? Maana nina makoo 5 yenye uwezo mkubwa wa kutaga na kutotoa kwa wakati mmoja, watatu kwa wakati na wawili kwa wakati.

Mara ya kwanza watatu walitoa vifaranga 39 na wawili walitoa 24 ila wengi walikufa kwa ugonjwa na kwa kuliwa na mdudu yule kama panya kwa mazingira niliyowaweka.

This time watatu wanalalia mayai jumla kama 37 na wale wawili washaanza kutetea.

Ninataka ku deal nao kwa jicho la karibu ili niweze kuwa na ukoo mkubwa.

Nipe darasa kwenye
—Magonjwa na chakula chanjo gani na baada ya muda gani?

—Malezi ya nje ndani unawafanyaje muda gani wawe nje na gani wawe ndani.

—Chakula cha kuwapa ni kipi
 
Mkuu samahani kwa kukuvamia, ila naomba nikushauri kitu ambacho kinaweza kukupa msaada wa haraka na msaada wa kudumu

baada tu ya kuku wako kuangua vifaranga, nenda Duka la madawa ya Mifugo, huko utapata ushauri wa nini ufanye na kipi ununue kwa ajili ya hao wajukuu zako na ata kuku wengine

Humu unaweza kupata msaada ila mara nyingi unakuwa sio msaada wa haraka na wa kudumu, mtu anaweza asikujibu kwa wakati na muda mwingine asikujibu kabisa ilhali wewe muda huo unahitaji msaada wake

Na kama hayo hayatoshi kuna baadhi ya watu watakujibu tu ata kama yeye mwenyewe hajui au hana uhakika na alichokujibu, either aliskia watu wanafanya au vyovyote vile maana kwenye mitandao ya kijamii kuna watu tunataka kuonekana tunajua kila kitu
 
Asante, shukran sana
 
Hongera kwa kuwa na wazo kama ilo

Mm nilinunua vifaranga vya kienyeji ambayo vina mwezi mmoja kama 50 then nikavifungia ndani ili vikuwe haraka maana nilikuwa nawapa chakula Cha kuku wa kisasa plus chanjo lkn baada ya week mbili wlianza kushusha mabawa na kupooza siku za mbeleni walianza kufa then walikufa kama 21

Baadae ikabid niwatowe njee Yan niwafuge nusu ndani nusu njee apo ndipo wakaanza kukua nilichogundua kwamba kuku wa kienyeji domestication Yao inachukua muda sana pia ni vigumu kukubali mazingira ya ndani kwa asilimia 100

Kuhusu kuwaingiza sokoni ndani ya week tano sio lahisi Mkuu maana kuku wa kienyeji wanakuwa tayali kuingizwa sokon ndani ya miezi sita kama wakilishwa vizuri

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Ndugu usi conclude jambo kirahisi hivyo.
Sio kweli kwamba kuku wa kienyeji ukiwafungia ndani hawakui vizuri.Hao vifaranga wako walipata maradhi na hii ni kawaida hata kama wangekuwa kroila ama wakisasa.

Nakushauri endelea kujifunza ufugaji,jitahidi unapopata changamoto uliza kwa ma dr ama wafugaji wazoefu.Mara nyingi tatizo kubwa kwa vifaranga ukiacha magonjwa yanayohitaji chanjo ni magonjwa ya matumbo(typhoid) na hapa nafikiri ndipo palipo kutesa wewe.

Vifaranga wanachangamoto kama usipokuwa mzoefu navyo.Lakini kama ni mzoefu vifaranga hawasumbui.

Jitahidi kutizama kinyesi chao mara kwa Mara ili iwe rahisi kutambua tatizo mapema uanze tiba kwa wakati.

Kwa mfano kinyesi cha ugoro ni dalili ya coccidiosis na kama kinyesi ni uharo mweupe wenye kung'ang'ania takoni hio ni dalili ya salmonella.

Jitahidi sana usafi wa mabanda na vyombo vyao vya chakula utapunguza kwa kiasi kikubwa maradhi.

Kuku wasipewe maji ya mvua kutoka kwenye ma tank haya maji yanaleta Sana maradhi kwa kuku hayafai.

Mimi ni mfugaji mzoefu sio dr.
Asanteni.
 
Habari ndugu zangu,

Mimi ni kijana niliyeamua kujiajiri rasmi kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara kwa asilimia 100, nimeanza kwanza utafiti kwa kujarbu kusikiliza maoni ya watu ambao tayari weshawahi kufanya ufugaji na kujipatia uzoefu wa kutosha.

Miongoni mwa maswali yangu ni je inawezekana kuanza na kuku wa kienyeji ambao tayr wana wiki tano hadi sita (walioanza kukomaa) na kuanza kuwafuga kisasa (namaanisha kuwapa chakula kisasa zaidi kama kuku wa kisasa na chanjo) na ndani ya wiki nne hadi tano waweze kukua na kuingia sokoni?

Na je kama inawezekana ni hatua zipi zaidi niweze kuchukua?

Na kama haiwezekani ni kwa sababu gani?

Naombeni msaada ndugu zangu
Vipi maendeleo?
 
Kazi unayo Jiandae kupata hasara kubwa ya chakula
Ila kuku watakua tu sawa
 
Hongera kwa kuwa na wazo kama ilo

Mm nilinunua vifaranga vya kienyeji ambayo vina mwezi mmoja kama 50 then nikavifungia ndani ili vikuwe haraka maana nilikuwa nawapa chakula Cha kuku wa kisasa plus chanjo lkn baada ya week mbili wlianza kushusha mabawa na kupooza siku za mbeleni walianza kufa then walikufa kama 21

Baadae ikabid niwatowe njee Yan niwafuge nusu ndani nusu njee apo ndipo wakaanza kukua nilichogundua kwamba kuku wa kienyeji domestication Yao inachukua muda sana pia ni vigumu kukubali mazingira ya ndani kwa asilimia 100

Kuhusu kuwaingiza sokoni ndani ya week tano sio lahisi Mkuu maana kuku wa kienyeji wanakuwa tayali kuingizwa sokon ndani ya miezi sita kama wakilishwa vizuri

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Wewe ni mfugaji kweli .
Na mimi nilinunua kuku wa kienyeje 100 nikawajengea banda nikawa nawapa chakula cha kisasa ila ukweli ni kuwa wakawa wanataga ila kuatamia wakawa wanaharibu mayai sana na walipofanikiwa walau kutoa hata vifaranga bado vilishusha mabawa na kufa .

Lakini pia kuku hao hao majogoo kwa matetea walishuka sana uzito tofauti na walivyo kuja mwisho nikaelewa kuwa kuku wa kienyeji hafugwi kisasa kabisa anahitaji atafute mwenyewe , anahitaji azurule sana , anahitaji azunguke kwenye majumba ya watu kusalimia na ndiyo aweze kuishi kwa afya na maendeleo .

Basi nikaamua kuwaachia wafurahi na roho zao , kiukweli sasa ni wanene na wana afya nzuri kikubwa nazingatia chanjo maana najua wanakutana na waathirika wengi wa magonjwa mtambuka huko mtaani ila naona afya zao zimeimarika na utagaji na uatamiaji uko juu sana .

Asante.
 
Hellow, msaada maana nahisi akili sio sawa

Mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji (kuwafungulia nje)

Kukatisha tu maelezo, mara ya kwanza nmetotolesha mayai 60 wakaangua vifaranga 50 wakafa 5, vkabaki 45 baada ya miezi mitano nkawauza wote hao wa awamu ya kwanza,

Awamu ya pili nkatotolesha hivyohvyo mayai 50 vkaangua 40,, vkafa 6...nkauza waliobaki

Awamu ya tatu hivyohvyo...

Awamu ya nne nmetotolesha mayai 100 vkaangua 90 mpaka wiki ilopita vlkuwa 88 mchana, usiku wa jpl, nikiwa na cheki nikaona kama kuku woteee wanasinzia, hapa iliwahi kutokea nkatwanga aloevera week tu ile hali ya kuanzia ikaisha,(nkafanya hivyohvyo)

Kuamkia juzi nkakuta vifaranga 10 wamekufa , leo hii mpk sasahvi wote wamekufa(haijawahi tokea)

Wakawa wamebaki kuku wakubwa kama kumi na tano , jana ikabd wale 5 nimwambie mama achinje angalau wasife wote

, leo hivi wakubwa walobaki wamesnzia wote sasa nnavyoandika wameshakufa watano wamebaki tano

Ina maana banda la kuku zaidi ya mia wamebaki 5 nmehisi kustack kwa kweli na nguvu sina tena

Wamenishauri nmwite bwana mifugo lakini wakuu kuku5? Nmemwita kesho aje lkn kabla hajaja kwa kuku wa kienyeji nani iliwahi mtokea hili, nmebaki nguvu sina mimi
Nmeshtuka hadi period ikaja isiyo

Nimekosea wapi au ni ugonjwa gani,tokea nmeanza kufuga SJAWAHI patwa hili so sad😭😭😭😭😭😭😭
 
Mkuu elezea kidogo hapa jinsi gani uliweza kuwalea nusu nje na nusu ndani? Maana nina makoo 5 yenye uwezo mkubwa wa kutaga na kutotoa kwa wakati mmoja, watatu kwa wakati na wawili kwa wakati.

Mara ya kwanza watatu walitoa vifaranga 39 na wawili walitoa 24 ila wengi walikufa kwa ugonjwa na kwa kuliwa na mdudu yule kama panya kwa mazingira niliyowaweka.

This time watatu wanalalia mayai jumla kama 37 na wale wawili washaanza kutetea.

Ninataka ku deal nao kwa jicho la karibu ili niweze kuwa na ukoo mkubwa.

Nipe darasa kwenye
—Magonjwa na chakula chanjo gani na baada ya muda gani?

—Malezi ya nje ndani unawafanyaje muda gani wawe nje na gani wawe ndani.

—Chakula cha kuwapa ni kipi
Hongera sana. Umepiga hatua. Mimi huwa nafanya hivi. Nawasubirisha mitetea itage na kuatamia kwa wakati mmoja. Wakishatotoa, nachagua tetea moja lenye umbo kubwa na mpole nampatia vifaranga wote..mf 20. Kisha vifaranga nawalisha STARTER kwa muda wa wiki mbili wakiwa na mama yao. Maji natumia multvitamin na glucose. Kumbuka pia kuwachanja chanjo ya kideri wakiwa na wiki moja,,kisha gumboro wakiwa na wiki mbili.
Baada ya wiki mbili, vifaranga wanakuwa wameota manyoya mazuri tu. Namtoa yule mlezi wao na kuwaacha peke yao wakiendelea kula STARTER mpaka wanafikisha mwezi mmoja. Baada ya hapo, Nawafuga nje ndani,,yaani nawatoa nje saa nne asubuhi juwa likishakuwa limewaka kukausha umande. Nawapa chakula na maji wakiwa nje. ( Binafsi natumia uzio wa waya ili kuwakinga na vicheche) Halafu jioni wakirudi tena ndani wanakutana na dinner yao. Baada ya hapo, naendelea kuwapa chakula cha kutengeneza kilicho na protins mf. Dagaa, uduvi, soya pamoja na mahindi ya kuparaza.
Hivyo, niliwahi kuweza kufikia kuuza kuku mwenye miezi mitano(Jogoo). Tsh. 20,000.
Ila itabidi mchanganyiko wako wa chakula usiwe pumba nyingi kuliko protins na calcium, ili kupata matokeo bora.
Kila la kheri katika harakati zako. Kila siku jifunze mbinu mpya, tutafika tu
 
Ndugu usi conclude jambo kirahisi hivyo.
Sio kweli kwamba kuku wa kienyeji ukiwafungia ndani hawakui vizuri.Hao vifaranga wako walipata maradhi na hii ni kawaida hata kama wangekuwa kroila ama wakisasa.

Nakushauri endelea kujifunza ufugaji,jitahidi unapopata changamoto uliza kwa ma dr ama wafugaji wazoefu.Mara nyingi tatizo kubwa kwa vifaranga ukiacha magonjwa yanayohitaji chanjo ni magonjwa ya matumbo(typhoid) na hapa nafikiri ndipo palipo kutesa wewe.

Vifaranga wanachangamoto kama usipokuwa mzoefu navyo.Lakini kama ni mzoefu vifaranga hawasumbui.

Jitahidi kutizama kinyesi chao mara kwa Mara ili iwe rahisi kutambua tatizo mapema uanze tiba kwa wakati.

Kwa mfano kinyesi cha ugoro ni dalili ya coccidiosis na kama kinyesi ni uharo mweupe wenye kung'ang'ania takoni hio ni dalili ya salmonella.

Jitahidi sana usafi wa mabanda na vyombo vyao vya chakula utapunguza kwa kiasi kikubwa maradhi.

Kuku wasipewe maji ya mvua kutoka kwenye ma tank haya maji yanaleta Sana maradhi kwa kuku hayafai.

Mimi ni mfugaji mzoefu sio dr.
Asanteni.
Kweli kabisa ndugu. Kwa vifaranga,,ukiweza kudhibiti unyevu na baridi bandani mwao. Unatoboa mpaka hautoamini.
Ukija kwenye lishe usiwe mbahili kama una malengo ya soko zuri la kuku wako. Wape lishe nzuri watakufurahisha. Chagua mbegu kubwa hususani pia mitetea,,maana wengi hudhani madume pekee ndio huleta matokeo chanya katika uzao wa kifaranga, la hasha tukumbuke pia ukubwa wa kiini cha yai anachokitengeneza tetea,kina determine ukubwa wa kifaranga. Nilishawahai kujaribu Cross breed ya sasso majike na majogoo ya kienyegi. Nilipata breed nzuri tu ambayo sokoni haikunisumbua. Ninachoamini kila siku ni kujifunza mbinu mpya. Pia kuku wanahitaji airtime kubwa sana,,ukiwasahau kidogo tu utakuta matokeo ya kusikitisha.
Kila mara fanya ukaguzi wa banda, pamoja na kuku wako. Kinyesi kitakupa alert bandani kwako kuna nini.
 
Hellow, msaada maana nahisi akili sio sawa

Mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji (kuwafungulia nje)

Kukatisha tu maelezo, mara ya kwanza nmetotolesha mayai 60 wakaangua vifaranga 50 wakafa 5, vkabaki 45 baada ya miezi mitano nkawauza wote hao wa awamu ya kwanza,

Awamu ya pili nkatotolesha hivyohvyo mayai 50 vkaangua 40,, vkafa 6...nkauza waliobaki

Awamu ya tatu hivyohvyo...

Awamu ya nne nmetotolesha mayai 100 vkaangua 90 mpaka wiki ilopita vlkuwa 88 mchana, usiku wa jpl, nikiwa na cheki nikaona kama kuku woteee wanasinzia, hapa iliwahi kutokea nkatwanga aloevera week tu ile hali ya kuanzia ikaisha,(nkafanya hivyohvyo)

Kuamkia juzi nkakuta vifaranga 10 wamekufa , leo hii mpk sasahvi wote wamekufa(haijawahi tokea)

Wakawa wamebaki kuku wakubwa kama kumi na tano , jana ikabd wale 5 nimwambie mama achinje angalau wasife wote

, leo hivi wakubwa walobaki wamesnzia wote sasa nnavyoandika wameshakufa watano wamebaki tano

Ina maana banda la kuku zaidi ya mia wamebaki 5 nmehisi kustack kwa kweli na nguvu sina tena

Wamenishauri nmwite bwana mifugo lakini wakuu kuku5? Nmemwita kesho aje lkn kabla hajaja kwa kuku wa kienyeji nani iliwahi mtokea hili, nmebaki nguvu sina mimi
Nmeshtuka hadi period ikaja isiyo

Nimekosea wapi au ni ugonjwa gani,tokea nmeanza kufuga SJAWAHI patwa hili so sad😭😭😭😭😭😭😭
Dada uko wapi? I wish tungewasiliana tukashea mawili matatu
 
Wewe ni mfugaji kweli .
Na mimi nilinunua kuku wa kienyeje 100 nikawajengea banda nikawa nawapa chakula cha kisasa ila ukweli ni kuwa wakawa wanataga ila kuatamia wakawa wanaharibu mayai sana na walipofanikiwa walau kutoa hata vifaranga bado vilishusha mabawa na kufa .

Lakini pia kuku hao hao majogoo kwa matetea walishuka sana uzito tofauti na walivyo kuja mwisho nikaelewa kuwa kuku wa kienyeji hafugwi kisasa kabisa anahitaji atafute mwenyewe , anahitaji azurule sana , anahitaji azunguke kwenye majumba ya watu kusalimia na ndiyo aweze kuishi kwa afya na maendeleo .

Basi nikaamua kuwaachia wafurahi na roho zao , kiukweli sasa ni wanene na wana afya nzuri kikubwa nazingatia chanjo maana najua wanakutana na waathirika wengi wa magonjwa mtambuka huko mtaani ila naona afya zao zimeimarika na utagaji na uatamiaji uko juu sana .

Asante.
kuku wa kienyeji hafugwi kisasa kabisa anahitaji atafute mwenyewe , anahitaji azurule sana , anahitaji azunguke kwenye majumba ya watu kusalimia😅🤣
 
Back
Top Bottom