Ushauri: Kujenga nyumba mjini au nje ya mji

Kujenga mbali na mji huko mboga ni safi toka shamba na mifugo ni uhakika.
 
Raha ya nje ya mji bwana ukute miundombinu ya umeme na maji ipo upate eneo kubwa unajenga zako.pale unalima bustani za mboga mboga, unafuga kuku wako hapo unafuga samaki wako hapo, bandq la mbuzi wanne pembeni, miti ya matunda Yani Mshana Jr akija tembea anamua ale nini matunda fresh, samaki fresh, au kuku fresh au mbuzi kutoka bandani umepanda miti yako ya kimvuli basi burudani safi, ukiwa mtu vileo week end mnakaa na mama watoroo kwenye kimvuli mnanyonywa vitu taratibu na mziki kwa mbali kutoka Boys 11 men😂😂😂
 
Hili ndio chaguo sahihi.
 
Sawa kabisa
 
Ha ha ha kustafia[emoji16]kwaweli ukishakuwa mzee stress za mjini ni za kuzikimbia,mjini tunawaacha watoto na wapangaji.
Hata huko unakokimbilia nje ya mji patakuwa mjini tu. Hakuna namna jenga nyumba kwenye eneo lenye huduma zote. Mambo ya kwenda kuhangaika na maji ya visima na umeme wa solar uzeeni ni changamoto.
 
[emoji23][emoji16]Raha sana, sema ndio upate sehemu ambayo huduma za msingi zimeshafika atleast utainjoy.
 
Hata huko unakokimbilia nje ya mji patakuwa mjini tu. Hakuna namna jenga nyumba kwenye eneo lenye huduma zote. Mambo ya kwenda kuhangaika na maji ya visima na umeme wa solar uzeeni ni changamoto.
Tatizo kupata eneo la kujiachia kwa mjini ni pesa ndefu atleast kwa nnje ya mji unaweza kupata eneo kubwa,changamoto ni kwenye huduma za msingi labda kusubiria hadi zifike au kujikaza kuishi hivyo hivyo hadi kutakapokuwa mjini
 
Tatizo ni hao majirani utakaowakuta huko nje ya mji ni shida. Utavamiwa na vibaka kila wakati mpaka utatamani kurudi mjini
 
ENEO NA BOMA LINAUZWA
KIBAHA KWA MFIPA JIRANI NA SEC.YA SIMBANI .
ENEO LINA UKUBWA WA NUSU HEKA. KUNA BOMA LA NYUMBA YA VYUMBA 3 VYOTE MASTER. SEBLE JIKO NA DINING. NIMEEZEKA VYUMBA 2. NA VYOO VYAKE TAYARI VINATUMIKA LINA TANK YA CHINI YA KUVUNIA MAJI LITA ELFU 3000.

UMEME NGUZO MBILI
MAJI NI MITA 500

km.1 kutoka main road

NATAKA ML. 18
 
Hili tatizo la upweke, ukiwa na pesa weka mifugo na ujenge nyumba za wadangaji kazi watakao hudumia mifugo. Hawa watakua watoto wako na majirani zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…