Ushauri: Kujenga nyumba mjini au nje ya mji

Ushauri: Kujenga nyumba mjini au nje ya mji

Habari wakuu,

Nahitaji ushauri wa wapi panafaa kujenga nyumba kwa ajili ya familia, option ya kwanza ni mjini,hii namaanisha sehemu ambayo haiko mbali na mjini na tayali kuna maendeleo kama barabara, umeme na huduma zingine za msingi,kero yake ni tayali kumeshabanana, utulivi hakuna na kiwanja sio kikubwa cha kuweza kujiachia au kufanya uwekezaji.

Option ya pili ni kujenga nnje ya mji,huku maendeleo bado hayajafika kama maji na umeme lkn barabara inafikika, uzuri wake kunautulivu, hali ya hewa nzuri na uwezekana wa kufanya uwekezaji mwingine upo kama vile kufuga, bustani n.k,kama ungelikuwa ni wewe ungechagua option gani na kwanini?
Kujenga mbali na mji huko mboga ni safi toka shamba na mifugo ni uhakika.
 
Raha ya nje ya mji bwana ukute miundombinu ya umeme na maji ipo upate eneo kubwa unajenga zako.pale unalima bustani za mboga mboga, unafuga kuku wako hapo unafuga samaki wako hapo, bandq la mbuzi wanne pembeni, miti ya matunda Yani Mshana Jr akija tembea anamua ale nini matunda fresh, samaki fresh, au kuku fresh au mbuzi kutoka bandani umepanda miti yako ya kimvuli basi burudani safi, ukiwa mtu vileo week end mnakaa na mama watoroo kwenye kimvuli mnanyonywa vitu taratibu na mziki kwa mbali kutoka Boys 11 men😂😂😂
 
Option ya pili ni kujenga nnje ya mji,huku maendeleo bado hayajafika kama maji na umeme lkn barabara inafikika, uzuri wake kunautulivu, hali ya hewa nzuri na uwezekana wa kufanya uwekezaji mwingine upo kama vile kufuga, bustani n.k,kama ungelikuwa ni wewe ungechagua option gani na kwanini?
Hili ndio chaguo sahihi.
 
Nje ya mji,
Jenga msingi, kisha uuache tu.
Halafu rudi mjini ujenge nyumba wa wastani tu ya makazi.
Huduma za umeme na maji ni muhimu.

Kufikia miaka kadhaa mbele, huko nje ya mji kutachangamka,
Utaendeleza ule msingi na kujenga nyumba ya malengo yako,
Kisha mjini utaweka wapangaji.
Sawa kabisa
 
Ha ha ha kustafia[emoji16]kwaweli ukishakuwa mzee stress za mjini ni za kuzikimbia,mjini tunawaacha watoto na wapangaji.
Hata huko unakokimbilia nje ya mji patakuwa mjini tu. Hakuna namna jenga nyumba kwenye eneo lenye huduma zote. Mambo ya kwenda kuhangaika na maji ya visima na umeme wa solar uzeeni ni changamoto.
 
Raha ya nje ya mji bwana ukute miundombinu ya umeme na maji ipo upate eneo kubwa unajenga zako.pale unalima bustani za mboga mboga, unafuga kuku wako hapo unafuga samaki wako hapo, bandq la mbuzi wanne pembeni, miti ya matunda Yani Mshana Jr akija tembea anamua ale nini matunda fresh, samaki fresh, au kuku fresh au mbuzi kutoka bandani umepanda miti yako ya kimvuli basi burudani safi, ukiwa mtu vileo week end mnakaa na mama watoroo kwenye kimvuli mnanyonywa vitu taratibu na mziki kwa mbali kutoka Boys 11 men[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji16]Raha sana, sema ndio upate sehemu ambayo huduma za msingi zimeshafika atleast utainjoy.
 
Hata huko unakokimbilia nje ya mji patakuwa mjini tu. Hakuna namna jenga nyumba kwenye eneo lenye huduma zote. Mambo ya kwenda kuhangaika na maji ya visima na umeme wa solar uzeeni ni changamoto.
Tatizo kupata eneo la kujiachia kwa mjini ni pesa ndefu atleast kwa nnje ya mji unaweza kupata eneo kubwa,changamoto ni kwenye huduma za msingi labda kusubiria hadi zifike au kujikaza kuishi hivyo hivyo hadi kutakapokuwa mjini
 
Tatizo ni hao majirani utakaowakuta huko nje ya mji ni shida. Utavamiwa na vibaka kila wakati mpaka utatamani kurudi mjini
 
ENEO NA BOMA LINAUZWA
KIBAHA KWA MFIPA JIRANI NA SEC.YA SIMBANI .
ENEO LINA UKUBWA WA NUSU HEKA. KUNA BOMA LA NYUMBA YA VYUMBA 3 VYOTE MASTER. SEBLE JIKO NA DINING. NIMEEZEKA VYUMBA 2. NA VYOO VYAKE TAYARI VINATUMIKA LINA TANK YA CHINI YA KUVUNIA MAJI LITA ELFU 3000.

UMEME NGUZO MBILI
MAJI NI MITA 500

km.1 kutoka main road

NATAKA ML. 18
 
Nje ya mji ni pazuri kama una access ya usafiri wako binafsi, utapata eneo kubwa lakini pia baada ya miaka kadhaa pata endelea.
Mimi ni mmoja ya waliojenga nje ya mji changamoto kubwa niliyo nayo ni ukimya wa mazingira tu na ukosefu wa majirani kwa karibu lakini mengine yote yako poa sana.

Nb: Siku zote kwa mtu ndio mbali ila kwako huwa sio mbali, jenga nje ya mji uwahi eneo ndugu.
Hili tatizo la upweke, ukiwa na pesa weka mifugo na ujenge nyumba za wadangaji kazi watakao hudumia mifugo. Hawa watakua watoto wako na majirani zako.
 
Back
Top Bottom