Habari wakuu,
Nahitaji ushauri wa wapi panafaa kujenga nyumba kwa ajili ya familia, option ya kwanza ni mjini,hii namaanisha sehemu ambayo haiko mbali na mjini na tayali kuna maendeleo kama barabara, umeme na huduma zingine za msingi,kero yake ni tayali kumeshabanana, utulivi hakuna na kiwanja sio kikubwa cha kuweza kujiachia au kufanya uwekezaji.
Option ya pili ni kujenga nnje ya mji,huku maendeleo bado hayajafika kama maji na umeme lkn barabara inafikika, uzuri wake kunautulivu, hali ya hewa nzuri na uwezekana wa kufanya uwekezaji mwingine upo kama vile kufuga, bustani n.k,kama ungelikuwa ni wewe ungechagua option gani na kwanini?