Ushauri kwa CCM - Upinzani hautakufa na Bora kuishi na mpinzani unayemfahamu kuliko ajaye usiyemjua!

Ushauri kwa CCM - Upinzani hautakufa na Bora kuishi na mpinzani unayemfahamu kuliko ajaye usiyemjua!

Ti Go

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Posts
1,062
Reaction score
1,088
Tangu mwaka 1995 mpaka Leo CCM imekuwa ikihangaika na kuua upinzani. Walianza na NCCR na kufanikiwa kuiua.

Kwa bahati mbaya ikaibuka CUF ikawa na nguvu mpaka wakasingiziwa kufanya siasa za ugaidi. Wakasingiziwa kuagiza matonteina ya majambia. Watu Zanzibar wakauawa, kwa mara ya kwanza Tanzania tukawa na wakimbizi wa kisiasa. CUF ikawasha moto kuliko wa NCCR. Chama changu cha mapinduzi kilihangaika sana kuiua CUF na wakafanikiwa.
Baada ya CUF ikaibuka CHADEMA na imekuwa moto mkali. Kwa mara ya kwanza bunge likapata wabunge zaidi ya 100 wa upinzani. Bungeni kukawaka moto.

Kwa hofu ya kutolewa madarakani CCM Sasa inatumia kila mbinu halali na haramu kuifuta CHADEMA. CHADEMA inaweza kufa, na kwa bahati mbaya ikifa, ni majanga, itaibuka sijui ACT ambayo moto wake inawezekana hautazimika.

Ushauri wangu, ni Bora ukaishi na mpinzani unayemfahamu kuliko kuja yule usiyemjua na akakuondoa kwenye uso wa Dunia. Iko siku mtanikumbuka
Asubuhi njema
 
Kinachowauma Ccm et al ni kwamba project ya kuimaliza chadema imechukua muda mrefu kuliko walivyodhania.. almost 20 years bado chadema ipo na ina exist.
 
Kifo cha CHADEMA ni ngumu sana, upendo wa wananchi kwa CDM umehama kutoka kwenye kadi kwenda mioyo....na sasa unaelekea kwenye damu....
 
Kule Zaire Mobutu alikua na vyama 200 vya mfukoni mfano wa vile vyama 18 vya CCM.

Wapinzani wake wa kweli waliuliwa au kufungwa jela. Kama haya yanayofanywa na CCM.

Lwambo Lwanzo Makiadi alitunga nyimbo za kukosoa. Alisukumizwa jela na alipotolewa kwa Nole aliimtungia Mobutu wa kampeni 1984 Mgombea namba moja Mobutu Seseko.

View: https://youtu.be/T33rO0ZgUUo?feature=shared
 
Alishindwa jiwe na minguvu yake ya ubaguzi nani mwingine ataweza?? wasira?
 
Kinachowauma Ccm et al ni kwamba project ya kuimaliza chadema imechukua muda mrefu kuliko walivyodhania.. almost 20 years bado chadema ipo na ina exist.
Iko wapi CHADEMA? Ladba debris tu wanayogawana
 
Dawa ni kumrudia Mungu na kujutia UOVU walioufanya hadi kumwaga damu za watu
Tukumbuke haya yanayoendelea ni kwa kuwa walishakula nyama za watu na wanaendelea kula!
Ubaya una mwisho na mwisho wake ni mwanzo wa mateso kwao.
 
Back
Top Bottom