Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Paskali umenishangaza unajua na umekiri wazi mahakama haipo huru na tunajua majaji wanateulewa na mwenyekiti wa ccm. Sasa chadema wakafungue kesi wapi? Mbinguni mm nawashauri chadema waandae maandamano nchi nzima
 
Paskali umenishangaza unajua na umekiri wazi mahakama haipo huru na tunajua majaji wanateulewa na mwenyekiti wa ccm. Sasa chadema wakafungue kesi wapi? Mbinguni mm nawashauri chadema waandae maandamano nchi nzima
 
Paskali umenishangaza unajua na umekiri wazi mahakama haipo huru na tunajua majaji wanateulewa na mwenyekiti wa ccm. Sasa chadema wakafungue kesi wapi? Mbinguni mm nawashauri chadema waandae maandamano nchi nzima
 
Sijatisha mtu, huu ndio ukweli wenyewe.
P
Acha kila mmoja ajichagulie njia yake, wewe jisemee kama wewe na wengine pia watajisemea wao kama wao,
Usijivike haki za wengine bila wao kukupa ruhusa,
Moyo wa mtu ni kichaka hakuna anayejua mwingine anawaza nini ,tusubiri tuone nini kitatokea
 
Acha kila mmoja ajichagulie njia yake, wewe jisemee kama wewe na wengine pia watajisemea wao kama wao,
Usijivike haki za wengine bila wao kukupa ruhusa,
Moyo wa mtu ni kichaka hakuna anayejua mwingine anawaza nini ,tusubiri tuone nini kitatokea
Binadamu tumetofautiana uwezo na uwezo wa uelewa, kuna watu wanamacho lakini hawaoni, na wana masikio lakini hawasikii, sasa wewe ukiwa ni miongoni mwa wenye macho, na ukaona kuna kundi kubwa la kipofu anawaongoza watu kuvuka barabara, na wao pia wamefunga macho, lakini wewe unawaona kabisa, anakowapeleka siko kwa sababu mbele kuna shimo, jee utawaacha tuu wakatumbukie kwenye shimo?. No mtu anayejali, akiona kuna hatari yoyote, inayomnyemelea mtu yoyote, atamsaidia kumuepushia na hiyo hatari.

Hivyo ninachofanya hapa ni kuwaamsha wana Chadema wasiojitambua, wasikubali kuswagwa kama mbuzi au kuwa kama nyumbu, kwa kuongozwa na vipofu kuishia kuwadumbukiza kwenye shimo kwa kuwagutusha tuu kuwa kiongozi wao wanaemtegemea ni kipofu hawezi kuwavusha, ili wale wenye macho, wafungue macho, walione hilo shimo, wasimame wasitumbukie shimoni!.

Udikiteta wowote wa the head of state ni something very serious, haupingwi kwa mandamano na mikutano ya hadhara.
P
 
Du!, leo limeshuka karipio kali kupiga marufuku maandamano, bado kuna mtu kweli ataandamana?.
 
Hongera kwa uchambuzi wako Ndugu Pascal Mayala. Nadhani watu wengi hawaelewi maana au dhana ya "Separation Of Powers" Swala la Rais kuagiza watu wasisafiri nje haliusiani na mwingiliano wa kiutendaji katika mihimili hii mitatu. Rais ndiye Mkuu wa Ajira katika Utumishi wa Umma. Japo yeye mwenyewe anawateuwa baadhi ya watu lakini kwa sheria zilizopo hawezi watoa kama atavyotaka hapana. Ila atabaki kuwa Mkuu wa Utumishi wa Umma. Iwapo anaona kuna jambo haliendi vizuri kwa mamlaka aliyo nayo anahaki ya kulinda maslahi ya nchi. Uwezi mlinganisha Jaji, Spika na Rais.

Rais ni Nembo ya Taifa, Nembo ya Dora na Nembo ya nchi. Ndo maana hata mapokezi ya Rais wa Taifa uwa ni tofauti na Jaji na Spika. Hivyo amri ya Rais ilikuwa ni halali kwani hakuingilia maamuzi au utendaji wa kimahakama, alichozuia ni utumiaji ovyo wa fedha ya serikali ambayo bajeti ikipangwa Mahakama haiitwi Bungeni kuwasilisha bajeti yake binafsi, pia kwa Bunge. Hizi zote uwasilishwa na Mawaziri husika katika wizara hizo. Leo hii kukitokea ubadhirifu katika Mahakama au Bunge mara nyingi anaeangaliwa ni mkuu wa nchi. Tazama Mahakama imekuwainaongoza kwa Rushwa siku zote inalaumiwa serikali kushindwa kudhibiti mianya ya rushwa si Jaji mkuu, kwasababu Serikali ndiyo iliyo na vyombo vya kuchunguza na kuzuia Rushwa wala si Bunge. Hivyo Rais yupo sawa kuzuia safari isipokuwa kwa kibari.

Swala la kuzuia mikutano ya siasa, nadhani mikutano haijazuiwa ila kinachotakiwa ni kufuata taratibu, hivi leo tukisema kwakuwa katiba inaruhusu watu kufanya mikutano ya kisiasa kusiwe na utaratibu sidhani kama kutakuwa na kuelewana. Kila mtu atafanya atakalo. Katiba inatoa huo uhuru lakini Pascal weye ni mwanasheria, kumbuka mbali yakuwa na sheria mama, lazima utunge kanuni au muongozo wa namna ya kutekeleza sheria mama. Katiba imeainishwa kwa kuwepo sheria mbalimbali katika kuweka utaratibu na kukidhi malengo ya sheria. Kwa watu wanao taka kuandamana. Katiba inaruhusu maandamano. Lakini kunataratibu na sheria zinazoelezea utaratibu wa maandamano uweje! Lazima kutolewe taarifa ya maandamano husika. polisi au vyombo vya ulinzi vinamamlaka ya kuangalia je jambo linalotakiwa kufanywa ni lakuvunja amani au siyo. Hapo inaweza zuia au ruhusu. Mafano maandamano ya tarehe 26/04/2018 nia ni kumpinga Rais na kutaka kumuondoa madarakani ipo wazi kwa mhamasishaji wa maandamano hayo anavyo dai. Pascal nambie Katiba ya nchi inaruhusu kumtoa Rais madarakani kwa utaratibu wa maandamano? Nadhani katiba imeeleza wazi namna ya kutokuwa na imani na Rais hatimaye kumuondoa. Afrika ya Kusini walitumia utaratibu kwa Mujibu wa katiba kumuondoa Rais wao. Lakini tunatofautiana pia kimuundo namna ya kumpata Rais.

Hivyo kinachotaka kufanyika ni uhaini na ni kinyume cha Katiba na Watu wakiandamana kwa kigezo hicho wao ndo wanavunja katiba ya nchi na ni vema hatua kali zichukuliwe dhidi yao. Nampongeza Rais kutamka wazi, na kuwaonya kwani watanzania tunafikiri kwa kuwa katiba inaruhusu maandamano basi unaweza amka nyumbani kwako ukaandamana bila sababu maalumu. Kuwe na sababu ya msingi isiyotaka vunja amani ya nchi. Vyombo vya Ulinzi na usalama vimeapa kulinda amani ya nchi. Hivyo ni wito wangu kwa wananchi kutulia na kuheshimu katiba. Watu mnadai Magufuri anaingilia Bunge hivi lini na ushahidi upo wapi Rais Magufuri kaingilia Bunge je kuna jambo au muswada wakati wa mjadala Rais aliingilia na kuweka mchango wake? Bado tukumbuke Miswada inapojadiliwa Bungeni wa mwisho kuipitisha ili iwe sheria ni Rais na wala si Spika wala wabunge. Hivyo Rais anamamlaka zaidi ya tudhaniavyo. Watanzania kuna watu wachache wanao taka kupotosha na kuharibu taswira ya Rais na nchi yetu kwa maslahi yao. Hivi kipi kibaya Rais kafanya, kusema watu walipe kodi? nchi gani wananchi wake hawalipi kodi? Kupinga Rushwa? Kuongeza utendaji na uwajibikaji wa serikali? Ebu watanzania tutulie tufanye kazi hata Marekani na nchi za Ulaya zilipata maendeleo wakati huo Demokrasia zao hazikuwa kama hivi leo. Marekani wanawake wameruhusiwa kupiga kula miaka ya sitini. Maamuzi mengi Ulaya yaliendeshwa kwa nguvu za viongozi wa wakati huo ndiyo maana nchi ziliendelea. Hii demokrasia ya Tanzania ni watu kutaka kupiga dili wameshindwa sasa wanaghadhabu na Rais. Poleni! Mhe Rais fanya kazi tuko nawe. Wabane na hujavunja katiba, watu wliingia katika siasa kwa maslahi binafsi sasa wanaonja joto ya jiwe. Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais Magufuri na mwezeshe kutuvusha salama. Amen.
 
"Hakuna dhambi mbaya kama uoga" Godbless Lema

Acha tuandamane tutapambana barabarani na polisi.

Makamanda tujiandae kuingia barabarani nawaomba Mbowe na Lowassa pamoja na Sumaye tuwe pamoja kwenye maandamano.
Mkuu mliandamana kwani? Mimi nilikuwa maporini sijui nini kiliendelea.
 
Yap! Wapo wengi watakaoandamana. Hasa wale wanaokandamizwa. Of course wewe najua upokazini . Believe me kuna watu ambao wako tayari kwa any consquences
Hakuna mtu ndani ya ardhi ya Tanzania wa kuandamana hiyo siku.

Mengine ni stori tu na kujifurahisha huku muanzilishi akijiongezea followers kwenye social media ajiongezee kipato.

Every social event is a lucrative business opportunity.
 
Ushauri mwingine huu kwa Chadema, ilikuwa waanze mikutano bila vibali Corona ikaokoa jahazi
Mkuu Wakili Msomi, Petro Mselewa, Naunga mkono hoja, ushauri huu ni mzuri sana kwa Chadema kufuata sheria bila shuruti.
Chadema kama mna masikio, sikieni.

P
 
Ushauri mwingine huu kwa Chadema, ilikuwa waanze mikutano bila vibali Corona ikaokoa jahazi
Mkuu Wakili Msomi, Petro Mselewa, Naunga mkono hoja, ushauri huu ni mzuri sana kwa Chadema kufuata sheria bila shuruti.
Chadema kama mna masikio, sikieni.

P
Mkuu Pascal Mayalla: Naomba uirejeshe kile kipindi chako cha KITI MOTO japo humu JF. Nilikipenda sana kile kipindi. Samahani Waheshimiwa kwa kuwatoa nje ya mstari. Haya ni yangu na P.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…