Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Ushauri mwingine huu kwa Chadema, ilikuwa waanze mikutano bila vibali Corona ikaokoa jahazi
Mkuu Wakili Msomi, Petro Mselewa, Naunga mkono hoja, ushauri huu ni mzuri sana kwa Chadema kufuata sheria bila shuruti.
Chadema kama mna masikio, sikieni.

P
pascally umerogwa na nani?sheria inawataka wawe na vibari au wanatakiwa kutoa taarifa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pasco ukomboz kihistoria haujawai kupatikana kwa njia unazopendekeza. Unatakiwa kujiuliza waliotunga katiba mwaka 1977 wakaweka haki ya KUANDAMANA KWANIN WALIFANYA HIVYO. Justice is not like a silver plate bur a blood plate. Watawala wa kiafrica uwa hawaelewi somo mpk damu za watu zimwagike ndo masikio yao yanazibuka. Maandamano ni haki ya kikatiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nadhani umemtupia lawama nyingi rais kwa kumuonea ww unanajua uhalisia wa utawala wa nchi unachotaka kufanya ni kuwahadaa watu kwa ushauri wako ambao unajua hauwezi kutekelezeka ili upande wa cdm waone umewashauri vizuri na upande wa rais ujue umesema sawa
Lakini mm nionavyo ww ulipaswa kuilalamikia katiba ya nchi ambayo ndio inayompa mamlika yote ayatendayo kama ulivyosema mahakama ni kibogoyo ni kweli yy ndie mteuzi wa watafsiri sheria ktb inampa nguvu ya kuwateuwa na kuwafuta bungeni hali kadhalika chama chake ndio wengi anauwezo wa kumfuta uwanachama mbunge yeyote asiekubaliana nae
Cha msingi kama kweli huchezi na akili za watu anza harakatki za kubadili ktb hayo uliosema yanawezekana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri huu bado ni valid kwa Chadema. Haki haitafutwi kwa maandamano!, bali inatafutwa kwa kufuata proper channels.

P
 
Pascal hivi haya yanayofanyika wewe unayapenda. Kweli Pascal unayapenda ebu sema ukweli from your HEART. Au kuna kitu unakitaka, mbona umebadilika baada ya kuomba kugombea Ubunge. Au ni kwavile walikunyanganya fursa zote mpaka ukaanza kukosa namna ya kulisha familia. Kama umerudi kwa ajili ya fursa yako pmj na familia yako ni vizuri ila ni bora ukae kimya. Mateso anayoyafanya Magufuli siyo ya kawaida, siyo uongozi wa haki. Magufuli kakosea wote tulimpenda Magufuli kabla ya 2015 lkn amebadilika huyu Magufuli wa sasa siyo yule wa kipindi cha Kikwete. Magufuli wa leo ni mpenda sifa asiyetaka kumsikiliza yeyote, mpenda malipizi, asiyesamehe, mwenye chuki. Magufuli wa leo anajiona yeye ni Mungu na hakuna kama yeye. Maandamano ndio itakayoikoa Tanzania ya sasa. Ngoja tuikomboe Tanzania, baadae nyie ndio mtakuwa wa kwanza kusema Magufuli alikuwa hafahi. Haki haiwezi kuja bila kutafutwa kwa nguvu, na yote haya lazima baadhi yetu wafe kwa ajili ya wenzao. TUPO TAYARI KUANDAMANA KWA AMANI WAKIAMUA KUTUUA SAWA. LKN HAWATAFIKA MBALI KTK UTAWALA WAO. One day utaniambia
 
Ni katika kukumbushana tuu, but this time namuomba IGP, Kamanda Sirro, waruhusiwe kuandamana kupunguza tension na machungu ili kuzuia watu wasipatwe na usongo wa hasira za kuamua lolote na liwe!.

Waacheni watu waandamane kupunguza na kumaliza hasira zao za kushindwa kwenye uchaguzi mkuu huru na wa haki, maana kiukweli kuna kushindwa na kushindwa, kushindwa kungine kunatia hasira!, yaani unashindwa kwa gap kubwa ajabu mpaka unashindwa kuamini!, chaguzi za nyuma hata kama ni kuiba, ni kujiiba kwa tuwili, tutatu, lakini this time, watu wamebebelea!.
Paskali
 
we ni hovles
 
Habari njema kuhusu maandamano ya Upinzani yaliyokuwa yafanyike leo, hayatakuwepo tena.kufuatia ushauri wangu huu.

Viongozi na wahamasisha maandamano wote wamejitokeza na kujisalimisha kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, hivyo hakuna kiongozi yoyote wa kuyaongoza maandamano hayo!.

Baada ya viongozi hao wote wa maandamano, kujisalimisha, wamehifadhiwa mahala salama ili wasiandamanishe watu katika maandamano haramu yenye nia ovu iliyojificha.

Hivyo sisi wakazi wa Dar, tuendelee na shughuli zetu kama kawaida.
P
 
mkuu Asante kwa kutambua uvunjifu wa Katiba lakin unataka waende mahakamani ambako nako kumetekwa unazani nani asie jipenda atasikiliza shauri lao na kutoa maamuzi
 
Nilidhani watu kupata haki yao kikatiba ndio sawa kumbe leo hii ni hisani ati watoe frustrations ?
 
Japo hili ni bandiko la siku nyingi, leo nimefarijika sana baada ya kusoma post hii
Siku zote nilidhani Chadema walisitisha maandamano yale baada ya kusoma bandiko hili, kumbe sababu sio hili bandiko bali ni ushauri huu wa Mkuu wa KKKT, Baba Askofu Dr. Shoo, ila kitendo cha mimi kutoa ushauri huu in public, halafu kuja kugundua kumbe na Baba Askofu alitoa ushauri kama huu, makes one feel good.

Asante sana Baba Askofu Dr. Shoo.
P
 
Tofauti yako na Dr Shoo ni hii , wewe ulikuwa unaitisha Chadema kwa kuamini kwamba Magufuli alikuwa na nguvu sana , wakati ulijua ana matatizo ya moyo , HAKUNA MGONJWA MWENYE NGUVU HATA MARA MOJA , nguvu za huyu zilitegemea genge lake pamoja na kikundi cha polisi , lakini Dr Shoo alimshawishi Mbowe kusitisha Maandamano
 
Mkuu Erythrocyte , kwanza wangapi walijua JPM had some serious underlying health issues?. Ni ukweli usiofichika JPM was very powerful na alikuwa ana nguvu sana!. The essence ya bandiko hili ni kuwaomba na kuwashawishi Chadema wasitishe maandamano yao ya UKUTA ili wasiumie . Nilichokifanya mimi ni kushawishi wasigomekuepishasinishasareandwasinwasis kuepusha shari nandicho kile kile alichokifanya Baba Askofu Dr. Shoo, kumkabili Freeman Mbowe na kumshawishi wasitishe maandamano yao wasiwaumize wanachama wao.

Tofauti ya ushauri wangu huu kwa Chadema na ushauri wa Baba Askofu Dr. Shoo, mimi ni nobody na nimewasisitiza wasisitishe maandamano kwa kuwatisha kuwa watakula kichapo ili waogope, Baba Askofu, kwanza yeye ni somebody, pili hajawatisha bali ametumia convincing power kwa Mwenyekiti wao, na Mbowe akakubali wakasitisha maandamano na kuepusha shari.

Baraka za karma kwa Baba Askofu kuwanusuru Chadema na shari, pia zinakuja kwangu kwasababu karma haina cha somebody wala nobody ndio maana hata naniliu, ni karma imekula kichwa.

Kitu muhimu kwa Chadema hapa ni
P
 
Paskali mbona sikuelewi, wewe unakataa Chadema wasijieleze na wewe huyohuyo unataka uhuru wa kujieleza uwepo! Unajipa upopo huku ukiwa mwanasheria.
Mkuu elvischirwa, mimi ni mtetezi wa freedom of expression, ukinikumbusha ni wapi nililataa Chadema wasijieleze, nitakushukuru sana!.
Kwenye bandiko hili nimetoa ushauri wa kisheria legal opinion bure kwa Chadema!, ushauri kama huu, unalipiwa!.

P
 
Mkuu elvischirwa, mimi ni mtetezi wa freedom of expression, ukinikumbusha ni wapi nililataa Chadema wasijieleze, nitakushukuru sana!.
Kwenye bandiko hili nimetoa ushauri wa kisheria legal opinion bure kwa Chadema!, ushauri kama huu, unalipiwa!.

P
Unatoaje ushauri kwa chama usichokitambua kuwa kipo! Bara umesema ipo CCM tu na visiwani CCM na ACT Wazalendo, labda tukianzia hapa tutaelewana.
 
Was this a right legal opinion pascal? Kwamba unashauri watu waache haki yao ya kikatiba ya kuandamana kisa tu watakutana na kipigo kikali? Kwa nini hukutumia nguvu yako kubwa hii kumshauri huyu aliyekuwa akisigina katiba kwa kumpa legal opinion? 'Mayala maana yake njaa' , hii kauli bado ina wasifu sahihi wa muandishi wa makala.
Mkuu elvischirwa, mimi ni mtetezi wa freedom of expression, ukinikumbusha ni wapi nililataa Chadema wasijieleze, nitakushukuru sana!.
Kwenye bandiko hili nimetoa ushauri wa kisheria legal opinion bure kwa Chadema!, ushauri kama huu, unalipiwa!.

P
 
Paskali siku zote huwa hapendi haki kwa wachache japo ni haki yao waipate, he was born to be a Great Dictator bahati nzuri mkono wa Bwana ulifanya kazi yake. Huyu mheshimiwa husema angependa awe kwama mhe. Lakha bila kujua mwenzake hakujali wingi au rangi, alijali haki ya kikatiba. Mimi huyu sitamsahau kwa kauli yake kuhusu mhe. Mbowe huko Mwanza hata baada ya kesi kufutwa, najua anajua maana ya kesi kufutwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…