Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Ushauri mwingine huu kwa Chadema, ilikuwa waanze mikutano bila vibali Corona ikaokoa jahazi
Mkuu Wakili Msomi, Petro Mselewa, Naunga mkono hoja, ushauri huu ni mzuri sana kwa Chadema kufuata sheria bila shuruti.
Chadema kama mna masikio, sikieni.

P
pascally umerogwa na nani?sheria inawataka wawe na vibari au wanatakiwa kutoa taarifa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pasco ukomboz kihistoria haujawai kupatikana kwa njia unazopendekeza. Unatakiwa kujiuliza waliotunga katiba mwaka 1977 wakaweka haki ya KUANDAMANA KWANIN WALIFANYA HIVYO. Justice is not like a silver plate bur a blood plate. Watawala wa kiafrica uwa hawaelewi somo mpk damu za watu zimwagike ndo masikio yao yanazibuka. Maandamano ni haki ya kikatiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nadhani umemtupia lawama nyingi rais kwa kumuonea ww unanajua uhalisia wa utawala wa nchi unachotaka kufanya ni kuwahadaa watu kwa ushauri wako ambao unajua hauwezi kutekelezeka ili upande wa cdm waone umewashauri vizuri na upande wa rais ujue umesema sawa
Lakini mm nionavyo ww ulipaswa kuilalamikia katiba ya nchi ambayo ndio inayompa mamlika yote ayatendayo kama ulivyosema mahakama ni kibogoyo ni kweli yy ndie mteuzi wa watafsiri sheria ktb inampa nguvu ya kuwateuwa na kuwafuta bungeni hali kadhalika chama chake ndio wengi anauwezo wa kumfuta uwanachama mbunge yeyote asiekubaliana nae
Cha msingi kama kweli huchezi na akili za watu anza harakatki za kubadili ktb hayo uliosema yanawezekana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kutoa ushauri wa bure, huu ni ushauri wa bure kwa Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba,
Hivyo nawashauri kwa dhati kabisa Chadema, haki haitafutwi kwa maandamano.

Ushauri huu bado ni valid kwa Chadema. Haki haitafutwi kwa maandamano!, bali inatafutwa kwa kufuata proper channels.

P
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kutoa ushauri wa bure, huu ni ushauri wa bure kwa Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba, kitendo cha rais Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa ni kinyume cha katiba!, rais Magufuli hana mamlaka ya kuzuia jambo lolote ambalo katiba imeruhusu, hivyo zuio la rais Magufuli kwa mikutano ya kisiasa, japo ni zuio batilii, lakini kwa vile Magufuli ndio Mkuu wa nchi, kila atakalosema, litatekelezwa tuu hata kama ni kinyume cha Katiba, mpaka pale vyombo vyenye uwezo wa kumdhibiti rais, vitakapo mdhibiti. Vyombo hivyo ni Bunge na Mahakama!. Hivyo alichokifanya rais Magufuli is nothing else Zaidi ya udikiteta at the highest nature na highest stages!. Dawa pekee ya kuzuia udikiteta huu sio maandamano, bali ni kutumia legal redress kwa Chadema kufungua shauri Mahakama Kuu, kuomba rasmi tafsiri ya kisheria ya katazo la rais kwa kutumia kitu kinachoitwa prerogative orders kinachoombwa kupitia Judicial Review.
Hizi Prerogative orders ziko 6, ila maarufu zaidi ni 3.

  • certiorari, an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
  • mandamus, an order issued by a higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
  • prohibition, directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;
  • habeas corpus, demands that a prisoner be taken before the court to determine whether there is lawful authority to detain the person;
  • quo warranto, requiring a person to show by what authority they exercise a power.
  • procedendo, to send a case from an appellate court to a lower court with an order to proceed to judgment.
Hivyo nawashauri kwa dhati kabisa Chadema, udikiteta haupingwi kwa maandamano, kama Chadema mnajipenda, tafadhalini sana msiandamane, sitisheni hiyo Operesheni UKUTA, na badala yake undeni jopo la wanasheria nguli, mfungue shauri mahakamani, badala ya kuwasumbua wanachama na wafuasi wenu kuandamana for nothing, kwa sababu kwenye udikiteta, kutumia maandamano kupingwa kuvunjwa kwa katiba, ni nothing!, mtaachieve nothing, na sana sana mtaishia kuumizwa na kuwaumiza wanachama, wapenzi na wafuasi wenu kwa kuutumia ule msemo wa Kiswahili "Mwenye nguvu mpishe", hata kama una haki, usitake kujipima nguvu kwa kutunishiana misuli na mtu mwenye nguvu zaidi yako, utaumia!. Na sio tuu mtu huyo ana nguvu zaidi yako, bali tayari, umeishajua pia kuwa ana hulka ya udikiteta, na ndio mwenye nguvu ya dola mikononi mwake!.

Misingi ya Katiba na The Rule of Law
Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya katiba na sheria, (the rule of law) ambapo nchi inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na sio kwa matamko ya viongozi yanayokwenda kinyume cha katiba!. Tangu rais Magufuli ameingia madarakani, ameisha onyesha kwa kauli na matendo kuwa kwake Katiba sio kitu!, it is nothing!, dawa ya mtu wa aina hii ni kuitumia katiba kumuwajibisha kwa kumfikisha mahakamani, akumbushwe kuwa nchi haindeshwi kwa matakwa binafsi ya mtu, bali inaendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni kama zilivyoainishwa kwenye katiba. Rais Magufuli atakumbushwa kuwa, kwa vile aliapishwa kuifuata, kuilinda na kuitekeleza katiba ya JMT, then ni lazima akiheshimu kiapo chake, kinyume cha hapo ni udikiteta tuu huu!.

The Doctrine of Separation of Powers With Check and Balance.
Nchi yetu ina mihmili mikuu mitatu, Serikali, (the executive), Bunge (The Legislature) na Mahakama (The Judiciary). Mihimili hii yote mitatu, ina nguvu za mamlaka sawa zinazojitegemea, bila kuingiliana, (powers), lakini nguvu hizo zinatenganishwa ili nguvu ya mamlaka moja isiingilie nguvu ya mamlaka nyingine, (separation of powers), huku kila mhimili ukiwa ni mwangalizi na mlinzi wa mhimili mwingine usivuke mipaka ya nguvu na mamlaka yake, kwa kufanya checks and balance, yaani ku act as a watchdog wa muhimili mingine.

Serikali yenye Nguvu, Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo!.
Mihimili hii, inaongozwa na viongozi ambao wana mamlaka kuu kuhusu mihimili yao. President ndio mkuu wa The Executive, Spika ndio mkuu wa The Legistlature, na Jaji Mkuu, ndie mkuu wa The Judiciary, lakini pamoja na nia njema kuwa mihimili yote ina mamlaka na hakuna mhimili wowote unaopaswa kujiinua juu Zaidi na kuwa na mamlaka kuu kuliko mhimili mwingine in theory, lakini kiukweli in practical, mhimili wa The Executive ndio mhimili mkuu unaomiliki vyombo vya dola na kuitawala mihimili mingine yote!, hivyo mkuu wa The Executive, yaani rais, ndio kila kitu!, akisema!, amesema!. Rais anaingilia Bunge, Bunge lipo na linaingiliwa huku linatazama tuu na linanyamaza, hili ni Bunge gani kama sio Bunge Butu?!, rais anaingilia mhimili wa Mahakama, Mahakama ipo na ina meno, lakini haiwezi kung'ata, hii ni Mahakama gani kama sio Mahakama Kibogoyo?, ila yote ni tisa kumi ni sisi wananchi, ndio wenye katiba, ndio tuliomuajiri rais Magufuli awe rais wetu kwa kura zetu, hivyo sisi ndio mabosi wake!. Serikali ipo kwa ajili yetu, Bunge lipo kwa ajili yetu, na mahakama ipo kwa ajili yetu, ila nasi kwa sababu hatujui wajibu wetu, nasi tupo tuu tumenyamaza tunaangalia!.

Rais Magufuli na Uvunjaji wa Katiba.
Tuambiane ukweli, tangu rais Magufuli ameingia madarakani, sio mara moja au mbili amekuwa akitoa kauli tata, zinazokwenda kinyume cha katiba, na kinyume cha kanuni ya the separation of powers kwa kuiamumuru mihimili ya Bunge na Mahakama kufanya hiki au kile, wakati mihimili hiyo ilipaswa kuingilia kati kwa kuicheck serikali kwa kumcheck mkuu wa the executive, lakini vyombo hivyo vimekaa kimya hivyo kumfanya rais ajisikie kuwa he is eveything, the big boss and he is always right! kwa kanuni ya "the boss is always right!". Njia pekee kuzuia uvunjwaji huu wa katiba ni kupitia mahakama.

Udikiteta wa Magufuli.
Hoja kama Magufuli ni dikiteta au la, haina mjadala, Magufuli ni dikiteta wa ukweli ambaye hana mswalie Mtume, na alipoingia tuu madarakani, alianza kuonyesha udikiteta wake right away kwa kuliingilia bunge na mahakama kuziweka chini ya amri zake!. Lile katazo lake la watumishi wa umma hawaruhusiwi kusafiri safari za nje bila kibali chake kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, liliwahusu watumishi wote wa serikali, likiwemo wabunge na watumishi wa bunge, wakiwemo majaji na watumishi wa mahakama!, just imagine Jaji Mkuu na Spika wa bunge wakapige magoti kwa rais kuomba kibali cha kutimiza wajibu wao!, huu sui tuu ni udikiteta, pia ni udhalilishaji wa bunge na mahakama!.

Baada ya katazo lile, checks and balance zingepaswa kuanzia hapo kwa Jaji Mkuu kumweleza rais huko ni kuingilia uhuru wa mahakama (the independence of the judiciary) hivyo muhimili wa mahakama haukupaswa kujisubmit chini ya the executive, bali mamlaka hayo ya kuzuia safari za nje, Spika alipaswa kuwa nayo kudhibiti safari za mhimili wa bunge, na Jaji Mkuu alipaswa kuwana nayo kudhibiti safari za mhimili wa mahakama, lakini mihimili hii ilikaa kimya kwa kujisubmit chini ya the executive, hivyo kumfanya rais kuwa ndio kila kitu!.

Hivyo sasa rais Magufuli ndio kila kitu, hakuna cha bunge, mahakama, wala katiba, amri ya rais ndio kila kitu na ndio sheria kuu!, hivyo nawashauri Chadema kwa dhati kabisa, wasitishe maandamano yao, wasifanye kabisa mchezo wa kumjaribu Ngosha, wataumia bure!, na badala yake waitumie mahakama kutoa tafsiri ya katazo la rais na sio kushindana nae au kutaka kupimana naye kwa kutunishiana msuli!.

Hili la udikiteta wa rais Magufuli, tumeisha lizungumza sana humu
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...
Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa ...

Dawa ya Udikiteta
Dawa pekee dhidi ya Udikiteta ni kupitia a legal redress kwa kufungua shauri mahakama kuu itoe tafsiri rasmi ya kisheria kama rais anavunja katiba au laa, kama amevunja katiba, then mahakama kuu kupitia prerogative orders, inamuamuru rais kwa kumlazimisha lazima afuate katiba, hivyo analazimishwa kufuta tamko lake, apende asipende, atake asitake, katiba ndio iko juu ya kila kitu, hata rais wa JMT, yuko chini ya katiba!.

Kama Chadema wanavyojinasibu wana wanasheria manguli, huo unguli wao kwenye sheria ni unguli wa kwenye nini kama serious issues kama hizi za kukiukwa kwa katiba, wanazipinga kwa maandamano na mikutano?!. Sio kila kitu kinapingwa kwa maandamano, na mikutano ya hadhara. Kuna wakati CHADEMA mnahamasisha maandamano ya kijingajinga. Sometimes Chadema wawe wanachukua ushauri kwa wenye busara wao kabla hawajafanya maandamano. Sikumbuki ni lini Moshi wamewahi kuandamana. Hii maana yake Ndesamburo ni miongoni mwa wenye busara wachache ndani ya Chadema. Sikumbuki kuwahi kumuona Ndesamburo, Prof. Beregu, Prof. Safari na Mzee Victor Kimesera wakishiriki maandamano yeyote zaidi ya yale ya Arusha. Hivyo sio kila kitu ni maandamano tuu!.

Uzuri wa Magufuli
Ila kitu kimoja kuzuri kuhusu udikiteta wa rais wetu, ni Rais Magufuli, japo ni dikiteta kweli na amevunja katiba kuzuia mikutano ya hadhara, yeye sio mwanasheria, hivyo baada ya kuchaguliwa rais, anajua yeye ndio kila kitu!, wala hajui kuwa mamlaka yake yana mipaka, hajui kuna vitu anaweza kufanya na kuna vitu hawezi, yeye anajua maadam ameshinda urais, na yeye ndio rais, hivyo anajiamini kyeye ndio kila kitu na anaweza kufanya chochote!, hivyo amefanya hayo ya nia njema, na dhamira safi hivyo ni dikiteta mzalendo!, mwenye uchungu na umasikini wa nchi hii, mwenye nia njema ya kusafisha uozo wote wa uzembe, rushwa na ufisadi, na kulikomboa taifa letu toka kwenye lindi la umasikini uliotopea na kuwa nchi ya maziwa na asali kupitia uchumi wa gesi na viwanda.

Mungu mbariki Magufuli!.

Mungu ibariki Tanzania.

Wasalaam.

Paskali
Rejea za shauri za bure
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa ...
Ushauri wa Bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared for ...
Ushauri wa Bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako ...
Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep ...
Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb)-Kwa Hili la ...
Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Zitto on Escrow Report: Please Keep Quite ...
Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Magufuli, Futilia Mbali Utawala wa Sheria ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Usikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.
Ushauri wa Bure kwa Dr. Shein: Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ...
Ushauri wa Bure kwa Magufuli, DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...

Pascal hivi haya yanayofanyika wewe unayapenda. Kweli Pascal unayapenda ebu sema ukweli from your HEART. Au kuna kitu unakitaka, mbona umebadilika baada ya kuomba kugombea Ubunge. Au ni kwavile walikunyanganya fursa zote mpaka ukaanza kukosa namna ya kulisha familia. Kama umerudi kwa ajili ya fursa yako pmj na familia yako ni vizuri ila ni bora ukae kimya. Mateso anayoyafanya Magufuli siyo ya kawaida, siyo uongozi wa haki. Magufuli kakosea wote tulimpenda Magufuli kabla ya 2015 lkn amebadilika huyu Magufuli wa sasa siyo yule wa kipindi cha Kikwete. Magufuli wa leo ni mpenda sifa asiyetaka kumsikiliza yeyote, mpenda malipizi, asiyesamehe, mwenye chuki. Magufuli wa leo anajiona yeye ni Mungu na hakuna kama yeye. Maandamano ndio itakayoikoa Tanzania ya sasa. Ngoja tuikomboe Tanzania, baadae nyie ndio mtakuwa wa kwanza kusema Magufuli alikuwa hafahi. Haki haiwezi kuja bila kutafutwa kwa nguvu, na yote haya lazima baadhi yetu wafe kwa ajili ya wenzao. TUPO TAYARI KUANDAMANA KWA AMANI WAKIAMUA KUTUUA SAWA. LKN HAWATAFIKA MBALI KTK UTAWALA WAO. One day utaniambia
 
Ni katika kukumbushana tuu, but this time namuomba IGP, Kamanda Sirro, waruhusiwe kuandamana kupunguza tension na machungu ili kuzuia watu wasipatwe na usongo wa hasira za kuamua lolote na liwe!.

Waacheni watu waandamane kupunguza na kumaliza hasira zao za kushindwa kwenye uchaguzi mkuu huru na wa haki, maana kiukweli kuna kushindwa na kushindwa, kushindwa kungine kunatia hasira!, yaani unashindwa kwa gap kubwa ajabu mpaka unashindwa kuamini!, chaguzi za nyuma hata kama ni kuiba, ni kujiiba kwa tuwili, tutatu, lakini this time, watu wamebebelea!.

we ni hovles
 
Habari njema kuhusu maandamano ya Upinzani yaliyokuwa yafanyike leo, hayatakuwepo tena.kufuatia ushauri wangu huu.

Viongozi na wahamasisha maandamano wote wamejitokeza na kujisalimisha kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, hivyo hakuna kiongozi yoyote wa kuyaongoza maandamano hayo!.

Baada ya viongozi hao wote wa maandamano, kujisalimisha, wamehifadhiwa mahala salama ili wasiandamanishe watu katika maandamano haramu yenye nia ovu iliyojificha.

Hivyo sisi wakazi wa Dar, tuendelee na shughuli zetu kama kawaida.
P
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, japo mimi ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, naomba kutoa ushauri huu wa bure kwa Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba yetu, haki hiyo ilifutwa kwa tangazo la rais Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa, japo ni kinyume cha katiba!, lakini rais Magufuli ana mamlaka yote ya kuzuia jambo lolote kwa Maslahi ya taifa hata kama jambo hilo limeruhusiwa na katiba, hivyo zuio la rais Magufuli kwa mikutano ya kisiasa, japo ni zuio linalokwenda kinyume cha katiba, lakini sio zuio batili kwasababu rais Magufuli ndio Mkuu wa nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, kila atakalosema, automatically linakuwa ni sheria na linafuatiwa na utekelezwaji tuu hata kama ni kinyume cha Katiba, mpaka pale vyombo vyenye uwezo wa kumdhibiti rais, vitakapo mdhibiti. Vyombo hivyo ni Bunge na Mahakama!.

Hivyo alichokifanya rais Magufuli is japo ni kama udikiteta fulani at the highest nature na highest stages, lakini as long as amefanya kwa nia njema, then rais Magufuli is doing the right thing, although in a wrong way.

Dawa pekee ya kuzuia udikiteta huu sio maandamano, bali ni kutumia legal redress kwa Chadema kufungua shauri Mahakama Kuu, kuomba rasmi tafsiri ya kisheria ya katazo la rais kwa kutumia kitu kinachoitwa prerogative orders kinachoombwa kupitia Judicial Review.
Hizi Prerogative orders ziko 6, ila maarufu zaidi ni 3.

  • certiorari, an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
  • mandamus, an order issued by a higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
  • prohibition, directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;
  • habeas corpus, demands that a prisoner be taken before the court to determine whether there is lawful authority to detain the person;
  • quo warranto, requiring a person to show by what authority they exercise a power.
  • procedendo, to send a case from an appellate court to a lower court with an order to proceed to judgment.
Hivyo nawashauri kwa dhati kabisa Chadema, udikiteta haupingwi kwa maandamano, kama Chadema mnajipenda, tafadhalini sana msiandamane, sitisheni hayo maandamano, na badala yake undeni jopo la wanasheria nguli, mfungue shauri mahakamani, badala ya kuwasumbua wanachama na wafuasi wenu kuandamana for nothing, kwa sababu kwenye mazingira haya kama ya udikiteta fulani, kutumia maandamano kupinga kuvunjwa kwa katiba, ni nothing!, mtaachieve nothing, na sana sana mtaishia kuumizwa na kuwaumiza wanachama, wapenzi na wafuasi wenu kwa kuutumia ule msemo wa Kiswahili "Mwenye nguvu mpishe", hata kama una haki, usitake kujipima nguvu kwa kutunishiana misuli na mtu mwenye nguvu zaidi yako, utaumia!. Na sio tuu mtu huyo ana nguvu zaidi yako, bali tayari, umeishajua pia kuwa ana hulka ya udikiteta, na ndio mwenye nguvu ya dola mikononi mwake!.

Misingi ya Katiba na The Rule of Law
Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya katiba na sheria, (the rule of law) ambapo nchi inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na sio kwa matamko ya viongozi yanayokwenda kinyume cha katiba!. Tangu rais Magufuli ameingia madarakani, ameisha onyesha kwa kauli za maneno na matendo kuwa kwake katiba sio kipaumbele chake, hivyo sio kitu kivile!, it is nothing.

Dawa ya mtu wa aina hii ni kuitumia katiba kumfanyia checks and balance kwa kuomba tafsi rasmi mahakamani, akumbushwe kuwa nchi haindeshwi kwa matakwa binafsi ya mtu, bali inaendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni kama zilivyoainishwa kwenye katiba. Rais Magufuli atakumbushwa kuwa, kwa vile aliapishwa kuifuata, kuilinda, kuitetea na kuitekeleza katiba ya JMT, then ni lazima akiheshimu kiapo chake, kinyume cha hapo ni udikiteta tuu, japo udikiteta wake ni udikiteta Mzalendo, a benevolent dictatorship!.

The Doctrine of Separation of Powers With Checks and Balance.
Nchi yetu ina mihmili mikuu mitatu, Serikali, (the executive), Bunge (The Legislature) na Mahakama (The Judiciary). Mihimili hii yote mitatu, ina nguvu za mamlaka sawa zinazojitegemea, bila kuingiliana, (powers), lakini nguvu hizo zinatenganishwa ili nguvu ya mamlaka moja isiingilie nguvu ya mamlaka nyingine, (separation of powers), huku kila mhimili ukiwa ni mwangalizi na mlinzi wa mhimili mwingine usivuke mipaka ya nguvu na mamlaka yake, kwa kufanya checks and balance, yaani ku act as a watchdog wa muhimili mingine.

Serikali yenye Nguvu, Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo!.
Mihimili hii, inaongozwa na viongozi ambao wana mamlaka kuu kuhusu mihimili yao. President ndio mkuu wa The Executive, Spika ndio mkuu wa The Legistlature, na Jaji Mkuu, ndie mkuu wa The Judiciary, lakini pamoja na nia njema kuwa mihimili yote ina mamlaka na hakuna mhimili wowote unaopaswa kujiinua juu Zaidi na kuwa na mamlaka kuu kuliko mhimili mwingine in theory, lakini kiukweli in practical, mhimili wa The Executive ndio mhimili mkuu unaomiliki vyombo vya dola na kuitawala mihimili mingine yote!, hivyo mkuu wa The Executive, yaani rais, ndio kila kitu!, akisema!, amesema!. Rais anaingilia Bunge, Bunge lipo na linaingiliwa huku linatazama tuu na linanyamaza, hili ni Bunge gani kama sio Bunge Butu?!, rais anaingilia mhimili wa Mahakama, Mahakama ipo na ina meno, lakini haiwezi kung'ata, hii ni Mahakama gani kama sio Mahakama Kibogoyo?, ila yote ni tisa kumi ni sisi wananchi, ndio wenye katiba, ndio tuliomuajiri rais Magufuli awe rais wetu kwa kura zetu, hivyo sisi ndio mabosi wake!. Serikali ipo kwa ajili yetu, Bunge lipo kwa ajili yetu, na mahakama ipo kwa ajili yetu, ila nasi kwa sababu hatujui wajibu wetu, nasi tupo tuu tumenyamaza tunaangalia!.

Rais Magufuli na Uvunjaji wa Katiba.
Tuambiane ukweli, tangu rais Magufuli ameingia madarakani, sio mara moja au mbili amekuwa akitoa kauli tata, zinazokwenda kinyume cha katiba, na kinyume cha kanuni ya the separation of powers kwa kuiamumuru mihimili ya Bunge na Mahakama kufanya hiki au kile, wakati mihimili hiyo ilipaswa kuingilia kati kwa kuicheck serikali kwa kumcheck mkuu wa the executive, lakini vyombo hivyo vimekaa kimya hivyo kumfanya rais ajisikie kuwa he is eveything, the big boss and he is always right! kwa kanuni ya "the boss is always right!". Njia pekee kuzuia uvunjwaji huu wa katiba ni kupitia mahakama.

Udikiteta wa Magufuli ni Dikiteta Mzalendo, A benevolent dictatorship
Hoja kama Magufuli ni dikiteta au la, haina mjadala, Magufuli ni dikiteta wa ukweli ambaye hana mswalie Mtume, ila dikiteta Mzalendo anayefanya udikiteta kwa nia njema, na tangu alipoingia tuu madarakani, alianza kuonyesha udikiteta wake right away kwa kuliingilia bunge na mahakama kuziweka chini ya amri zake!. Lile katazo lake la watumishi wa umma hawaruhusiwi kusafiri safari za nje bila kibali chake kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, liliwahusu watumishi wote wa serikali, likiwemo wabunge na watumishi wa bunge, wakiwemo majaji na watumishi wa mahakama!, just imagine Jaji Mkuu na Spika wa bunge wakapige magoti kwa rais kuomba kibali cha kutimiza wajibu wao!, huu sui tuu ni udikiteta, pia ni udhalilishaji wa bunge na mahakama!.

Baada ya katazo lile, checks and balance zingepaswa kuanzia hapo kwa Jaji Mkuu kumweleza rais huko ni kuingilia uhuru wa mahakama (the independence of the judiciary) hivyo muhimili wa mahakama haukupaswa kujisubmit chini ya the executive, bali mamlaka hayo ya kuzuia safari za nje, Spika alipaswa kuwa nayo kudhibiti safari za mhimili wa bunge, na Jaji Mkuu alipaswa kuwana nayo kudhibiti safari za mhimili wa mahakama, lakini mihimili hii ilikaa kimya kwa kujisubmit chini ya the executive, hivyo kumfanya rais kuwa ndio kila kitu!.

Hivyo sasa rais Magufuli ndio kila kitu, hakuna cha bunge, mahakama, wala katiba, amri ya rais ndio kila kitu na ndio sheria kuu!, hivyo nawashauri Chadema kwa dhati kabisa, wasitishe maandamano yao, wasifanye kabisa mchezo wa kumjaribu Ngosha, wataumia bure!, na badala yake waitumie mahakama kutoa tafsiri ya katazo la rais na sio kushindana nae au kutaka kupimana naye kwa kutunishiana msuli!.

Hili la udikiteta wa rais Magufuli, tumeisha lizungumza sana humu
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...
Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa ...

Dawa ya Udikiteta

Dawa pekee dhidi ya Udikiteta ni kupitia a legal redress kwa kufungua shauri mahakama kuu itoe tafsiri rasmi ya kisheria kama rais anavunja katiba au laa, kama amevunja katiba, then mahakama kuu kupitia prerogative orders, inamuamuru rais kwa kumlazimisha lazima afuate katiba, hivyo analazimishwa kufuta tamko lake, apende asipende, atake asitake, katiba ndio iko juu ya kila kitu, hata rais wa JMT, yuko chini ya katiba!.

Kama Chadema wanavyojinasibu wana wanasheria manguli, huo unguli wao kwenye sheria ni unguli wa kwenye nini kama serious issues kama hizi za kukiukwa kwa katiba, wanazipinga kwa maandamano na mikutano?!. Sio kila kitu kinapingwa kwa maandamano, na mikutano ya hadhara. Kuna wakati CHADEMA mnahamasisha maandamano ya kijingajinga. Sometimes Chadema wawe wanachukua ushauri kwa wenye busara wao kabla hawajafanya maandamano. Sikumbuki ni lini Moshi wamewahi kuandamana. Hii maana yake Ndesamburo ni miongoni mwa wenye busara wachache ndani ya Chadema. Sikumbuki kuwahi kumuona Ndesamburo, Prof. Beregu, Prof. Safari na Mzee Victor Kimesera wakishiriki maandamano yeyote zaidi ya yale ya Arusha. Hivyo sio kila kitu ni maandamano tuu!.

Uzuri wa Magufuli na Udikteta Wake.
Ila kitu kimoja kuzuri kuhusu udikiteta wa rais wetu, ni Rais Magufuli, japo ni dikiteta kweli na amevunja katiba kuzuia mikutano ya hadhara, yeye sio mwanasheria, hivyo baada ya kuchaguliwa rais, anajua yeye ndio kila kitu!, wala hajui kuwa mamlaka yake yana mipaka, hajui kuna vitu anaweza kufanya na kuna vitu hawezi, yeye anajua maadam ameshinda urais, na yeye ndio rais, hivyo anajiamini kyeye ndio kila kitu na anaweza kufanya chochote!, hivyo amefanya hayo ya nia njema, na dhamira safi hivyo ni dikiteta mzalendo!, mwenye uchungu na umasikini wa nchi hii, mwenye nia njema ya kusafisha uozo wote wa uzembe, rushwa na ufisadi, na kulikomboa taifa letu toka kwenye lindi la umasikini uliotopea na kuwa nchi ya maziwa na asali kupitia uchumi wa gesi na viwanda.

Mungu mbariki Magufuli!.

Mungu ibariki Tanzania.

Wasalaam.

Paskali
Rejea za shauri za bure
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa ...
Ushauri wa Bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared for ...
Ushauri wa Bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako ...
Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep ...
Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb)-Kwa Hili la ...
Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Zitto on Escrow Report: Please Keep Quite ...
Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Magufuli, Futilia Mbali Utawala wa Sheria ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Usikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.
Ushauri wa Bure kwa Dr. Shein: Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ...
Ushauri wa Bure kwa Magufuli, DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...
mkuu Asante kwa kutambua uvunjifu wa Katiba lakin unataka waende mahakamani ambako nako kumetekwa unazani nani asie jipenda atasikiliza shauri lao na kutoa maamuzi
 
Ni katika kukumbushana tuu, but this time namuomba IGP, Kamanda Sirro, waruhusiwe kuandamana kupunguza tension na machungu ili kuzuia watu wasipatwe na usongo wa hasira za kuamua lolote na liwe!.

Waacheni watu waandamane kupunguza na kumaliza hasira zao za kushindwa kwenye uchaguzi mkuu huru na wa haki, maana kiukweli kuna kushindwa na kushindwa, kushindwa kungine kunatia hasira!, yaani unashindwa kwa gap kubwa ajabu mpaka unashindwa kuamini!, chaguzi za nyuma hata kama ni kuiba, ni kujiiba kwa tuwili, tutatu, lakini this time, watu wamebebelea!.
Paskali
Nilidhani watu kupata haki yao kikatiba ndio sawa kumbe leo hii ni hisani ati watoe frustrations ?
 
Wanabodi,

japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba yetu, haki hiyo ilifutwa kwa tangazo la rais Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa.

Kama Chadema wanavyojinasibu wana wanasheria manguli, huo unguli wao kwenye sheria ni unguli wa kwenye nini kama serious issues kama hizi za kukiukwa kwa katiba, ndizo zinazohitaji manguli wa sheria, lakini wao wanazipinga kwa maandamano na mikutano?!.
Sio kila kitu kinapingwa kwa maandamano, na mikutano ya hadhara. Kuna wakati CHADEMA mnahamasisha maandamano ya kijingajinga
Sometimes Chadema wawe wanachukua ushauri kwa wenye busara wao kabla hawajafanya maandamano.
Sikumbuki ni lini Moshi wamewahi kuandamana. Hii maana yake Ndesamburo ni miongoni mwa wenye busara wachache ndani ya Chadema. Sikumbuki kuwahi kumuona Ndesamburo, Prof. Beregu, Prof. Safari na Mzee Victor Kimesera wakishiriki maandamano yeyote zaidi ya yale ya Arusha. Hivyo sio kila kitu ni maandamano tuu!.

Mungu ibariki Tanzania.

Wasalaam.

Paskali
Japo hili ni bandiko la siku nyingi, leo nimefarijika sana baada ya kusoma post hii
DR Shoo ametoboa siri kwamba yeye na maaskofu wenzake ndio waliomuita na ndio waliomshauri Mbowe kusitisha operesheni UKUTA ili kuepusha mauaji ya Raia wasio na hatia na akatii na kusitisha maandamano yale , Bila kumung'unya maneno Askofu Shoo amesikitishwa sana na kitendo cha Mbowe kusingiziwa Ugaidi.
Siku zote nilidhani Chadema walisitisha maandamano yale baada ya kusoma bandiko hili, kumbe sababu sio hili bandiko bali ni ushauri huu wa Mkuu wa KKKT, Baba Askofu Dr. Shoo, ila kitendo cha mimi kutoa ushauri huu in public, halafu kuja kugundua kumbe na Baba Askofu alitoa ushauri kama huu, makes one feel good.

Asante sana Baba Askofu Dr. Shoo.
P
 
Japo hili ni bandiko la siku nyingi, leo nimefarijika sana baada ya kusoma post hii

Siku zote nilidhani Chadema walisitisha maandamano yale baada ya kusoma bandiko hili, kumbe sababu sio hili bandiko bali ni ushauri huu wa Mkuu wa KKKT, Baba Askofu Dr. Shoo, ila kitendo cha mimi kutoa ushauri huu in public, halafu kuja kugundua kumbe na Baba Askofu alitoa ushauri kama huu, makes one feel good.

Asante sana Baba Askofu Dr. Shoo.
P
Tofauti yako na Dr Shoo ni hii , wewe ulikuwa unaitisha Chadema kwa kuamini kwamba Magufuli alikuwa na nguvu sana , wakati ulijua ana matatizo ya moyo , HAKUNA MGONJWA MWENYE NGUVU HATA MARA MOJA , nguvu za huyu zilitegemea genge lake pamoja na kikundi cha polisi , lakini Dr Shoo alimshawishi Mbowe kusitisha Maandamano
 
Mkuu Erythrocyte , kwanza wangapi walijua JPM had some serious underlying health issues?. Ni ukweli usiofichika JPM was very powerful na alikuwa ana nguvu sana!. The essence ya bandiko hili ni kuwaomba na kuwashawishi Chadema wasitishe maandamano yao ya UKUTA ili wasiumie . Nilichokifanya mimi ni kushawishi wasigomekuepishasinishasareandwasinwasis kuepusha shari nandicho kile kile alichokifanya Baba Askofu Dr. Shoo, kumkabili Freeman Mbowe na kumshawishi wasitishe maandamano yao wasiwaumize wanachama wao.

Tofauti ya ushauri wangu huu kwa Chadema na ushauri wa Baba Askofu Dr. Shoo, mimi ni nobody na nimewasisitiza wasisitishe maandamano kwa kuwatisha kuwa watakula kichapo ili waogope, Baba Askofu, kwanza yeye ni somebody, pili hajawatisha bali ametumia convincing power kwa Mwenyekiti wao, na Mbowe akakubali wakasitisha maandamano na kuepusha shari.

Baraka za karma kwa Baba Askofu kuwanusuru Chadema na shari, pia zinakuja kwangu kwasababu karma haina cha somebody wala nobody ndio maana hata naniliu, ni karma imekula kichwa.

Kitu muhimu kwa Chadema hapa ni
P
 
Paskali mbona sikuelewi, wewe unakataa Chadema wasijieleze na wewe huyohuyo unataka uhuru wa kujieleza uwepo! Unajipa upopo huku ukiwa mwanasheria.
Mkuu elvischirwa, mimi ni mtetezi wa freedom of expression, ukinikumbusha ni wapi nililataa Chadema wasijieleze, nitakushukuru sana!.
Kwenye bandiko hili nimetoa ushauri wa kisheria legal opinion bure kwa Chadema!, ushauri kama huu, unalipiwa!.

Unatoaje ushauri kwa chama usichokitambua kuwa kipo! Bara umesema ipo CCM tu na visiwani CCM na ACT Wazalendo, labda tukianzia hapa tutaelewana.
 
Was this a right legal opinion pascal? Kwamba unashauri watu waache haki yao ya kikatiba ya kuandamana kisa tu watakutana na kipigo kikali? Kwa nini hukutumia nguvu yako kubwa hii kumshauri huyu aliyekuwa akisigina katiba kwa kumpa legal opinion? 'Mayala maana yake njaa' , hii kauli bado ina wasifu sahihi wa muandishi wa makala.
Mkuu elvischirwa, mimi ni mtetezi wa freedom of expression, ukinikumbusha ni wapi nililataa Chadema wasijieleze, nitakushukuru sana!.
Kwenye bandiko hili nimetoa ushauri wa kisheria legal opinion bure kwa Chadema!, ushauri kama huu, unalipiwa!.

P
 
Was this a right legal opinion pascal? Kwamba unashauri watu waache haki yao ya kikatiba ya kuandamana kisa tu watakutana na kipigo kikali? Kwa nini hukutumia nguvu yako kubwa hii kumshauri huyu aliyekuwa akisigina katiba kwa kumpa legal opinion? 'Mayala maana yake njaa' , hii kauli bado ina wasifu sahihi wa muandishi wa makala.
Paskali siku zote huwa hapendi haki kwa wachache japo ni haki yao waipate, he was born to be a Great Dictator bahati nzuri mkono wa Bwana ulifanya kazi yake. Huyu mheshimiwa husema angependa awe kwama mhe. Lakha bila kujua mwenzake hakujali wingi au rangi, alijali haki ya kikatiba. Mimi huyu sitamsahau kwa kauli yake kuhusu mhe. Mbowe huko Mwanza hata baada ya kesi kufutwa, najua anajua maana ya kesi kufutwa.
 
Back
Top Bottom