Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,992
- 22,396
Salaam kwenu wakuu,
Mimi sijihusishi na siasa za Tanzania kidhati ya moyo, nimekuwa ni mfuatiliaji tu wa namna mambo yanavyokwenda/yanavyoendeshwa ndani ya nchi yetu. Niliwahi kuwa mwanachama wa CUF Habari mwanzoni mwa miaka ya 2010 na kadi yangu nilipewa na Julius Mtatiro, hata hivyo nilihamia CCM imara muda mfupi baadae baada ya kugundua hakukuwa na upinzani Imara nchini kwetu. Maamuzi hayo yalichagizwa na ule msemo wa "if you can't beat them, join them". Fikra kuu ni ile fikra ya aliemtoa gerezani ndugu Nelson Mandela, President FW De Klerk na namna alivyofika kuwa pale.
Ila rasmi baada ya kesi maarufuu visiwani Zanzibar ya mwaka 2013 kuanza niliamua rasmi kuachana na mambo ya siasa na kujikita kwenye kushughulikia mambo yangu na familia yangu huku nikiamini ni mimi, na ni mimi tu ambae ningeweza kuikomboa familia yangu nyonge kutoka kwenye umaskini na wala sio wana-siasa.
Yakawa yaliyokuwa na uchaguzi wa mwaka 2015 ukafika, kwa vile wengine tulikuwa kiakili kabla ya ki-umri tukakaa pembeni na kuangalia mambo yatakavyokuwa. Muda wa kwenda kwenye mikutano ya kampeni tukatumia kuzalisha mali huku fikra zetu pevu zikituambia hata kama CUF watashinda uchaguzi basi hawatopewa nchi kuiongoza (na hivyo ndivyo ilivyokuwa).
Uchaguzi ukafanyika, Jecha akaufuta, Maalim akahangaika mpaka kwa wadhamini wa demokrasia (Ulaya na Marekani) lakini hakuna lililokuwa. Kijambo kilikuwa kipo, mpaka leo tumefikia tunaingia tena kwenye uchaguzi na "kijambo kimeyayuka". Hii kamwe haimaanishi kukejeli harakati za Maalim katika kupigania demokrasia Zanzibar au kupigania haki ya Wazanzibar la hasha! Napenda kutambua mchango mkubwa wa Mh. Maalim Seif Shariff Hamad katika harakati za demokrasia nchini Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Mafanikio yake ni makubwa mno na hata kama atafariki leo basi Maalim ataiaga dunia hii akiwa mshindi. Kuipata SUK Zanzibar si mafanikio ya kubeza hata kidogo.
Kwa jitihada tu za Maalim na timu yake, leo hii hata wanaoitwa "wapinzani" watakuwemo kwenye baraza la mawaziri la Serikali ya Zanzibar kuanzia November mwaka huu In Shaa Allah. Haya ni mafanikio makubwa sana ambao wanasiasa wa Tanganyika na sehemu nyengine nyingi za Afrika hawajaweza kuyafikia bila umwagaji damu.
Mbali ya mafanikio haya, yapo makosa makubwa sana ya ki-msingi ambayo Maalim pengine na chama waliyafanya ambayo yanagharimu harakati hizi za kiukombozi wa demokrasia Zanzibar na Tanzania kwa ujumla mpaka leo hii. Na hili ndilo lililonisukuma kuandika makala hii ili iwe funzo kwa Maalim na chama cha ACT Wazalendo katika uchaguzi huu ujao. Labda tu kwa uchache niainishe ninayoyaona makosa makuu aliyoyafanya maalim hapo mwaka 2015 au kabla ambayo sasa yanagharimu harakati za ukombozi wa kidemokrasia kama ifuatavyo
1) Kukataa kurudia uchaguzi wa Mwezi Machi 2016- Hili lilipelekea Baraza la wawakilishi kuwa na wawakilishi kutoka chama kimoja tu, na tumshukuru Mungu kwamba walibaki kuwa wazalendo kwa Zanzibar yao maana kwa hali ile wangeweza kupitisha sheria kandamizi dhidi ya vyama vya upinzani na Wazanibar kwa ujumla na kwenda kinyume na yote yale ambayo CUF kipindi hicho walijinasibu kuyapigania.
2) Kutoandaa na/au kumtambulisha mtu ambae angekuwa/atakuwa mrithi wake baada ya yeye kuondoka kwenye siasa kwa namna yoyote ile i.e kifo, afya, umri n.k
NOTE: Kwa wanaojua habari za siasa hususan za Zanzibar, wanaelewa kwamba hayo hapo juu ni makosa ambayo yanagharimu harakati za kidemokrasia Zanzibar mpaka leo.
USHAURI:
1) Uchaguzi una kushinda na kushindwa, halafu hapa Tanzania kuna kupewa na kutopewa. Imani ya wengi ni kwamba Maalim amekuwa akishinda kila chaguzi lakini hapewi na hakuna chochote kiwacho, hivyo sitakosea kusema anaweza akashinda mwaka huu na pia asipewe vile vile, ushauri wangu ni kwamba hata asipopewa basi akubali kushindwa huko na atengeneze SUK pamoja na CCM kama ilivyokuwa mwaka 2010. Hii itasaidia kufanya upinzani ushiriki katika kuwatumikia wananchi katika level nyengine kabisa na pia itatoa nafasi ya wapinzania ndani ya Zanzibar kuwa na nafasi nzuri ya kuwashawishi viongozi wengine watakaotoka CCM masuala yahusuyo Zanzibar kila itokeapo (naamini nimeeleweka).
Lazima safari hii wapinzania wakubali kushiriki kutengeneza serikali maana heri nusu shari kuliko shari kamili.
2) IKitokea upinzania umeshindwa au umeshinda halafu hawakupewa basi Maalim Seif Shariff Hamad na chama chake cha ACT Wazalendo wamteue mtu mwengine mbali na Maalim kuwa Makamu wa kwanza wa Rais. Hili nadhani katiba ya Zanzibar inaliruhusu. Hii itatoa nafasi kwa huyo mteuliwa Mfano Nassor Mazrui au rafik yangu Mh. Mansoor Himid kuandaliwa kwa kipindi cha miaka 5 ijayo ili aweze kuwa mgombea tofauti (na Maalim) kwa mara ya kwanza tangu siasa za vyama vinig zilipoanzishwa nchini (maana Maalim amekuwa mgombea wa upinzani tangu 1995 na ni hakika hatoweza kusimama tena majukwaani ifikapo 2025).
Maalim asikubali kujiaminisha kwamba ni yeye tu ndie ataweza kuwa Rais Zanzibar kutokea upinzani maana hilo litakuwa ni kosa kubwa na itaendelea kuwa dosari kama ilivyo dosari sasa hivi katika harakati hizi za ukombozi wa kidemokrasia.
Naamini Zitto kama kiongozi mkuu wa chama mtaufikiria ushauri huu na kuufanyia kazi.
NB: Kwa wale wana-CCM mnaofuata tu mkumbo, sisi wengine ni wanachama halali wa CCM na tuna kadi za chama kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Tumeamua tu kutumia akili zetu kufikiria.