Binafsi ni shabiki damu wa Diamond pamoja na kwamba huwa napata wasaa wa kusikiliza kazi za wasanii wengine nje ya WCB ili kuonja radha tofauti ya bongo Fleva.
Diamond kafanya mengi ya msingi na muhimu katika tasnia hii ya burudani, Diamond kaiambia dunia kuna nchi Inaitwa Tanzania ina mziki wake unaitwa Bongo Fleva na dunia ikapokea kwa mikono miwili kile ilicho ambiwa na Diamond.
Sio unafiki, wasanii wengi walikata tamaa na huu mziki, hata huyu Kiba wa Cinderella, Msiniseme, MC Muga na nyinginezo alikata tamaa na huu mziki ni Diamond alive mrudisha kwenye game.
Diamond Kama ilivyo kwa akina Sugu, Prof Jay, Solothang, na wakali wengine aliwaaminisha wazazi wengi Kuwa BongoFleva siyo uhuni, aliwashape vijana wengi waichukulie fani hii Kama kazi ambayo inaweza wajengea heshima na kuwapa kipato cha kuweza kutengeneza kesho yao na familia zao. Binafsi Nina mkubali sana huyu kijana, kuna wakati nilitamani hata mwanangu nimpeleke kwenye shule zinazo toa elimu ya Music, lakini hiki anacho anza kukifanya hivi karibuni sio tu kinakatisha tamaa bali kinafedhesha.
Diamond anatufedhesha Mashabiki na wapenzi wa sanaa yake, sijajua haya mabadiliko yanatokana na nini ukizingatia anaofanya nao kazi sasa, ndio hao hao waliomfikisha hapo!
Diamond wa leo anashindwa itumia vyema mitandao ya kijamii kama alivyokuwa akifanya awali, kuna kipindi aliwahi mtuhumu Wema kuwa anapenda sana kuweka mambo yao ya faragha hadharani binafsi nilimuelewa sana, leo anafanya yale aliyokuwa akiyachukia kipindi cha nyuma!
Pages za Diamond kwenye mitandao ya kijamii zilijaa kazi, leo yupo States, mara yupo London kesho yupo SA, hii ilikuwa inatupa Motisha kuwa Mwenyezi Mungu anabariki kazi ya mikono ya huyu kijana. Lakini leo hii Diamond kawa wa kupost MATUSI KWENYE KURASA ZAKE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII!
Mimi sitaki zungumzia alichofanya hivi karibuni dhidi ya mshindani wake ambaye mimi binafsi siamini kama ni mshindani wake (Diamond akirudi kwenye my number one, nataka kulewa na kutupa radha ile ya Tatizo kwetu Mbagala, Nitarejea sioni mshindani wowote kati ya hawa vijana)
Diamond alimuacha mbali sana Kiba, leo hii kaamua kumfanya Kiba mshindani wake kwa makosa madogo ambayo yanarekebishika lakini kinyume chake yeye anapalilia hayo makosa.
MFANO:
Diamond siyo wa kwanza kupewa skendo za kuzalisha mabinti na kukataa majukumu, na akumbuke yeye siyo mume wa Zari labda kama tumefichwa, lugha aliyoitoa dhidi ya wanao mshutumu kukataa majukumu yake kwa Hamisa imechefua walio wengi sana hasa wanawake ambayo ndio wapenzi hasa wa BONGO FLEVA.
Diamond amesahau ama hajui HULKA YA MWAFRIKA KAMA SIYO MTANZANIA kuwa hapendi kuona kiwango cha mafanikio ya MTU na hasa kama anafahamu yeye ndio sababu ya wewe kuwa na mafanikio hayo. Watu wa namna hii hupenda kukuonyesha kuwa wao ndio kila kitu katika maisha yako na ukitaka kuwaonyesha kuwa ni BIDII YAKO KATIKA MAISHA wataanza kukutengenezea visa waku_prove wrong! Na nini ndicho wanachofanya Watanzania dhidi ya huyu kijana. Diamond alipaswa kuweka kando maisha yake binafsi, lakini hili nalo mdogo wangu hajaliona.
Ofisini:
Bila kupepesa macho, Prodyuza wa WCB Ndugu Laizer kaelemewa, ana majukumu mengi sasa WCB ina member sio chini ya 6 na hawa wanategemea ubongo wa Laizer ufanye ubunifu wa kimataifa kama alivyofanya na anavyofanya kwa Bosi wao! Hili jambo haliwezekani. Diamond sishauri umkimbie huyu kijana mwenzio bali muongezee nguvu, mtafutie MTU wa kumsiadia baadhi ya vitu kama mixing na mengineyo, lakini pia sio mbaya kama ukiwachukua marodyuza wakali kama Mika Mwamba, Master Jay, Enrico na kuwaomba waje wakufanyie kazi kwenye ofisi zako.
Chunguza melody na vionjo vya kazi zenu karibia nyingi sasa mnafanana hii inachosha na inaudhi mashabiki.
Management:
Sitaki Mzungumzia sana Tale huyu ni mswahili kama waswahili wengine hasa nikiliangalia kundi la Tip Top Connection, mtazame Salam sijajua kapatwa na nini ila binafsi naona kama naye kalewa MAFANIKIO YAKO, ama kuna jambo nyuma ya pazia. Diamond sijasikia mashudu ama mapovu toka kwa Binti Seven Mosha juu ya hili bifu lenu, unadhani hakupondi?
Lakini tazama anachofanya Meneja wako anakuchoresha sana, anakuingiza kwenye kumi na nane za wakuchukiao 100% jaribuni kuliepuka hili.
Please nakuomba hiyo Tarehe 1 September usilete uswahili fanya kazi kama zamani haya mengine waachie mashabiki waamue SIYO kama anavyosema Meneja na wakati huo huo anafanya upumbavu