Ushauri kwa kijana mwenzetu

Miaka 29 unahangaika na jimama ambalo lilikwishaolewa na kuwa-widowed WHY?

Kama ni tamaa ya mali za marehemu mwambie aendelee; kama ni kutaka mke wa kuoa mwambie tamaa itampeleka pabaya!
Nadhani si tamaa amempenda tu!mwambie amuoe tu jamani kama moyo wake una mpenda,heri ya huyo aliyeolew ndoa moja iliyo rasmi kuliko hao wengine ambao walishaolewa ndoa kumi zisizo rasmi.....heri ya huyo mwenye mtoto mmoja aliye hai kuliko wale waliojiozesha ndoa zisizo rasmi na k
uwauawa watoto kadhaa wakiogopa kashfa ya kukosa waume wa halali kwa kuwa wana watoto!
halafu huyo dada hakuachwa bali mumewe alifariki....inaonekana alikuwa na tabia nzuri ndio maana kifo kiliwatenganisha...
 

roselyne1 nimetafuta kidude cha thanks bwana nimekikosa ila kula hiyo :thumb::happy:
 

Hilo ni swali la kujiuliza sababu wengine wako kwenye mahusiano halafu wanapata watoto then mmoja wao anafariki sasa sijui hapa huyu aliyefiwa naye anakuwa hana right ya kuolewa swali jingine ambalo nimekuwa nikijiuliza sana ni kwanini mwanaume awe older than mwanamke na sio mwanamke awe older than mwanaume maana watu wakisikia mwanaume ana umri wa miaka 29 halafu mwanamke ana miaka 35 mwanaume utasemwa mpaka kwamba umechukua mzee :confused2:
 
Mbona mama kashamaliza? Labda unahitaji ufafanuzi wa maneno ya huyu mama, maana kaona kitu. Au kijana huyu anahitajika kufanya nini ili afanikiwe katika safari yake. Vinginevyo, he must meet at least the standards of the late husband, otherwise things will not be right as such...!
 

Roselyne1, nimekuelewa vizuri tu. Inawezekana wengi tumeathirika na mfume dume na kuishia kuwa wabaguzi kama unavyosema. Labda tumtendee haki aliyeleta mada badala ya kuendelea kubishana kwenye mambo ambayo zaidi ni 'maoni' na sio 'hoja'. Mpe maoni (views) yako kama alivyoomba. Mimi yangu yalikuwa haya hapa chini (Post#85) na kama kwayo kunanifanya nionekane 'mbaguzi 'hilo nipo tayari kulibeba:

 
Wakuu kwa upande wangu naona imekaa njema tu.Kwani unaweza ukawa umepata mke ambaye hajazaa lakini kitu yake inavidonda kwani imechubuliwa na watu zaidi ya mia nane.Cha msingi na maelewana ndani ya nyumba,vile vile pengine huwezi jua huyo mtoto inaweza ikawa ni msaada wake hapo baadaye kwani mimi na wewe hatujui kesho iko vipi.Mimi naishi na mke ambaye alikuwa amesha zaa ila kwa bahati mbaya wakati wa kuzaa alipata kifafa cha mimba mtoto akafariki ila alikuwa hajaolewa (bado alikuwa kwa wazazi wake) na jamaa alimwambia kuwa yeye ndie atakuwa mke wake wa ndoa kumbe jamaa alikuwa na mke na alipogundua ikiwa bado mjamzito wakaachana.Nilipo kutana nae nikaa nae tukaya weka mezani mambo yetu wote kwa pamoja na tuka yajadili kwa marefu na mapana tukayamaliza na mwanaume nikalidhia.Mpaka leo mwaka wa pili niko nae tuna mtoto wa kike mmja tuna mpenda na tuna wapwndana sana.nashukuru Mungu kwani kila mtu yupo wazi kwa mwenzie hata simu tuna tumia pamoja ila kuepuka usumbufu hawezi akapokea namba za ofisini ila nyingine ni ruksa.Unaweza ukasema wewe mjanja unataka kitu chako npeke yako kumbe ukiondoka tu majamaa yanapanga foleni.Kaka mjane huyo usimwache kwani anajua maisha ni nini na pale alipokuwa anakosea kwa marehemu mume wake atakuwa amejirekebisha.Na pia yatakiwa kujua kuwa ndani ya nyumba kuna mgongano wa mawazo kama hakuna ujue uliye naye hazimtoshi kwa lugha rahisi ni bendera hufuata upepo ila ni kwa mgongano wa kimaendeleo.Tuchangie kwa kutumia uzoefu,na kusikia pia.Inawezekana asilimia kubwa ya hao wanaopinga wana kaka au dada zao ambao kabla ya mama zao kuolewa na baba zao alisha wapata kwa baba wengine.Je mama zenu hawakuwa na haki ya kuolewa tena?
 

mmoja wapo mie, nimeolewa na mwanaume ambae alikuwa na mtoto tayari, nampenda, namlea kama mwanangu, hapa ndio nimeona eti itakuwa shida kulea mtoto asie wako, eti atabadilishwa jina au vipi, kama BelindaJocob bac mama akiolewa aitwe Belinda(jina la huyo aliemuoa mama yako) kuna viswali huelewi mtu anafikiria nini kuuliza swali kama hilo....BJ well said ma...Be blecd.
 

Inafika wakati mtu unataka kuoa/kuolewa uangalie nini kinakufurahisha,kupishana umri kidogo siyo mbaya hata kama mwanamke ni mkubwa kama kwa miaka 3 dhidi ya mwanaume!..ukisikiliza watu/dunia utaishi kufuata watakavyo sivyo utakavyo!!
Kama mmoja wa wanandoa amefariki na ana mtoto,kuingia tena ndoani inawezekana akipata mtu ampendae!..maisha mafupi kutafuta right person wakati mtu uko wrong!!..
 

Dear ulifanya la maana ilhali ulimpenda mpenzi wako ambae ndo mumeo sasahivi, hongera kwa upendo na kukubaliana na hali halisi!! Na mtu asiyeweza kumlea mwanae ataweza kumlea nani?!ni ngumu sana pia kuna maswali mengine ni kutibuana kama siyo kuchanganya au muda mwingine mtu ana majibu anakutega tu!!
Kaa salama mamii..God bless!!!!
 
...aaah,
acha upoe tu bana, Uji wenyewe umejaa pili pili manga! :coffee:

Awww!!..mie nahema juu hapa, futari ndo inashuka na uji ule mpaka jasho jepesi lilinitoka..leo sili daku,lol
 
Kwa vile huyo mama alijiweka wazi, sioni tatizo, ila awe mwangalifu vya kutosha. Kwa vyovyote ndoa hiyo ni tofauti na ndoa MPYA. Hata hivyo hakuna kikwazo. Atamsaidia sana huyo mjane kusahau msiba wake. Ila ampe muda wa kutosha wa uchumba ili amfahamu.
 
Hapa sioni shaka yoyote,, Asiogope kuoa wa nafsi yake. muhimu ajiulize kama kweli amempenda!! kulea watoto wa wenzetu iwe tabia yetu. hakika hakuna anaependa kufiwa na pia watoto wa marehemu wanathamini sa malezi bora wakipewa..

huyo huyo wala usijiangaishe. mikosi na balaa yapatikana pia kwa hao vipusa.

Angalizo!!! kama vipi mkapime kwanza HIV kabla hamjaanza kujiachia huru. Maana vijana wa siku hizi 29 huenda ashatembea na videmu 29. asije kumlaumu jimama kumbe yeye!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…