Funzadume,
Hapa sijaona mtu ambaye anasema kuwa mwanamke aliyefiwa na mume hafai au hatakiwi kuolewa. Jamaa ameomba ushauri/maoni na ndiyo tunayompatia. Yanaweza kuwa sawa na alivyotegemea au kinyume. Binafasi nimeeleza na hata Baba Enock pia, kwamba ingekuwa vizuri mtu ambaye keshaonja maisha ya ndoa akampata mwenzie ambaye tayari naye keshapitia. Hao watakuwa kwenye level moja. Lakini katika hii case, hawa watu wako kwenye levels tofauti na kwa hiyo wana uzoefu totafauti. Inawezekana pia wanawazia mambo tofauti na wana mategemeo tofauti ingawa kwa sasa wote wanaona kwamba wanapendana. Mambo ya unyumba na ndoa ni magumu sana na kwa hiyo lazima utegemee tofauti kama hizi. Kwa sababu tumekulia katika mazingira tofauti, na uzoefu wetu, wishes zetu n.k vinatofautiana pia. Binafsi mwanangu akinijia na case kama hii nitasikitika sana ila sitamkataza. Nitajaribu kumweleza fika kile ninachokijua ili aweze kujua haswa haswa maana ya ndoa tena ambayo mmoja wao ana-score goli la pili. Kwa hiyo huo ni ushauri wetu kwa mleta mada ukizingatia hata mama yake huyo kijana hakuzipokea taarifa za uhusiano wao kwa mikono miwili. Pia hadi kulete hii mada hapa, huyu kijana inawezekana ameanza kuwa mbayu wayu na amini usiamini baada ya haya mawazo ya wadau, he will never be the same as he used to be.