Ushauri kwa Lissu: Kutana na makundi maalumu!

Ushauri kwa Lissu: Kutana na makundi maalumu!

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Ni kawaida kwa kampeni za siasa za Marekani kwa mgombea kukutana na makundi maalumu ya watu, nadhani wanaita Town Hall meetings, na kuzungumzia mambo maalumu ya kisera. Halafu mgombea unatumia nafasi hiyo kutoa ‘major speech’.

Uzuri wa mfumo huu unasaidia kufocus kwenye jambo moja, mfano elimu, afya, usalama wa taifa, sheria, utawala wa sheria, nk.

Kwa hiyo unaweza kuandaa mkutano wa ndani na wanafunzi wa vyuo vikuu ukazungumzia suala la elimu kwa ujumla. Ukapokea maswali na hoja za wanafunzi. Vivyo hivyo, ukakutana na wajasiriamali wadogo ukazungumzia masuala ya kodi, biashara. Ukaenda kukutana na wakulima, nk.

Binafsi ningependa kuona unaandaa mkutano na watu wenye ulemavu, kuanzia albinos, viziwi, na ulemavu wa viungo vya mwili na kusikiliza matatizo yao na wewe kueleza jinsi utakavyoyatatua.

Unaweza kutumia mkutano kama huo kuelezea kwa kina masaibu uliyopitia na jinsi ulivyo recover. Wakumbushe Watanzania kuhusu FDR, Rais pekee wa Marekani aliyeongoza kwa awamu 3 na labda ni pekee aliyekuwa mlemavu. Hili kundi siyo kubwa sana ila inaweza kuwa nafasi ya pekee sana kuteka hisia za watu wengi.

Mikutano hii ni ya ndani. Kwa kuwa media kubwa zimedhibitiwa, itakiwa ni jukumu la CHADEMA kusambaza short clips za mambo muhimu yaliyojadiliwa. Hapo utaweza kuteka social media kwa wiki nzima kwa tukio la siku moja.

Bado mikutano mikubwa itaendelea kufanyika kwa sababu na yenyewe ina nafasi yake muhimu kwenye kampeni.

Jambo muhimu lingine ni kutengeneza na kununua TV Ads hata za dakika moja moja hasa katika prime time, mfano kabla tu au baada ya taarifa za habari. Hizi zina impact kubwa kwenye kampeni ingawa kwa Tanzania bado ni jambo geni. CCM wameshawahi kuzitumia huko nyuma ila sina kumbukumbu ya kuona wapinzani wakifanya hivyo.
 
Hoja zako ni nzuri sana kiukweli,kama anasikia atazingatia na kuzifanyia kazi.
 
CC:
Erythrocyte ; Naomba uwatagi akina Lema, T. Makene, J. Mrema et al. Pia nasikia we pia ni MTU wa jikoni peleka hii habari. CCM wasipate dohani ya kutokea
 
Ni mambo mazuri sana na kama siyo siasa kuzuiwa kwa miaka mitano, hii kitu ingetakiwa ianze 2016! Lakini bado tunaweza kupambana, naomba mlio karibu na viongozi mchukue maoni huku na kuongezea kwenye mawazo yenu mazuri.
 
Back
Top Bottom