Ushauri kwa makampuni ya simu nchini na TCRA jambo hili

Ushauri kwa makampuni ya simu nchini na TCRA jambo hili

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2020
Posts
888
Reaction score
821
Baada ya sheria ya mitandao nchini kuanza kazi, na makampuni ya simu kuweka no 106 kama njia ya kuhakiki namba uliyosajiri kwa mfumo wa finger print.

Basi nashauri hivi:
ingekuwa vyema makampuni pamoja na TCRA wangeweka option ya mtu kuikataa namba ambayo anataka iondolewe ili kukidhi takwa la kisheria la LAINI MOJA MTANDAO MMOJA

Pale pale kwenye no 106.

Hii itasaidia kuondoa gharama pamoja na mda wakwenda kujipanga kwa wakara au ofisi za makampuni ya simu.

Lakini pia, huduma hii itaondoa usumbufu kwa wananchi walioko pembezoni na miji au wale wasio na fedha za kijigaramia kufika maeneo husika.

Ikumbukwe kuwa zoezi la kusajiri line kwa vitambulisho vya taifa wananchi wengi mijini na vijijini walitapeliwa na vitambulisho vyao kutumiwa na watu wasiokuwa wema.
Ndio maana mataperi wa nitumie pesa katika namba hii hawajaisha.

Lakini pia ikiwa ushauri wangu utazingatiwa niwazi kuwa italeta maana ya wananchi kuhamasishwa matumizi ya technology zaidi .

Pamoja nahayo! Nataka kuwakumbusha makampuni ya simu na TCRA kwa ujumla yakuwa! Bado selikari na wizara ya afya inahamasisha swala la kujikinga na kuzingatia ushauri wa wizara ya afya kuhusu COVID-19.

Niwazi kuwa ukibonyeza no *106# ok nakisha kuchagua hakiki no ulizosajiri niwazi utamalizia na ujumbe wakukuambia niwajibu wako kufika katika ofisi ya kampuni yako kufuta namba usiyoitambua

Kwahiyo ujumbe huu unahamasisha mikusanyiko na usumbufu zikiwemo gharama bila sababu endapo tungebuni na kuhamasisha matumizi ya mtandao.

Dawa ya matapeli wa nitumie pesa ktk namba hii wakihitaji makampuni au TCRA basi waniletee wito maarumu nikawape.
Hamtawasikia tena.

Enzi na Enzi
Dar es salaam.
July 2020.
 
hivi utaratibu wa kumiliki laini moja kwa kila mtandao ni kwaajili tu ya kudhibiti wale jamaa wa tuma pesa kwenye namba hii?
 
Safi sana hilo Wazo nzuri mno maana nimeanza kuona foleni kama kipindi hicho cha Nida. Watuwekee hiyo option ya kufuta namba tu sio mpaka kukimbizana kwenye maofisi yao.
 
hivi utaratibu wa kumiliki laini moja kwa kila mtandao ni kwaajili tu ya kudhibiti wale jamaa wa tuma pesa kwenye namba hii?

Moja ya malengo yao nikuthibiti watanzania kusajiliana line za simu pamoja na kuwathibiti hawa jamaa japo naamini wale wanitumie pesa ktk namba hii hawatadhibitiwa kwa njia hii.
 
Msemaji Wa TCRA Katoa Ufafanuzi Kuhusu Hili Jambo Kuwa Na Line Zaidi Ya Moja Haina Shida Yoyote Isipokuwa Watu Ndiyo Hatujaelewa!!!
Unakwenda Kujaza Form Basi Unaendelea Na Matumizi Kama Kawaida
 
Msemaji Wa TCRA Katoa Ufafanuzi Kuhusu Hili Jambo Kuwa Na Line Zaidi Ya Moja Haina Shida Yoyote Isipokuwa Watu Ndiyo Hatujaelewa!!!
Unakwenda Kujaza Form Basi Unaendelea Na Matumizi Kama Kawaida

Kaka kujaza form nikwawale wenye uhitaji!
Kumbuka kunawatu walitapeliwa mjini na vijijini.
Nahao usishangae hata huyo msemaji hawajui hata kama yupo.

Unadhani mmatengo wa wilaya ya nyasa huko kizota anajua hilo.
 
Piga *106# kuhakiki namba ulizosajili kwa alama ya Vidole. Endapo hutofahamu namba yeyote kwenye orodha, tafadhali tembelea duka la Voda lililo karibu nawe.
 
Moja ya tatizo kubwa tulilonalo Tanzania ni kutotilia mkazo gharama ya muda na bila kujirekebisha hatutaendelea wala hatutapata wawekezaji makini kila ukienda kwenye huduma za umma au serikali ni lazima upoteze nusu siku au siku nzima
 
Wale matapeli wa nitumie pesa katika namba hii hawataisha kama sheria hii imetungwa kuwathibiti

Bali mtamaliza watu kuwafunga magerezani maana mtu wakulipa hayo mamilioni ya faini niwachache sana.

kwanini nasema hivyo.
iko hivi! Namba za simu sasa hivi ziko mbali mno!
Kiasi kwamba mtu akibuni namba! Mfano 0767xxxxxx hii ukiipiga au kuiandikia ujumbe utakuta inamtu .

Kwahiyo mataperi hawapati shida.
Namba zao ndo zawale waliotapeliwa mjini na vijijini ambao hawana hata habari ya matangazo ya TCRA.

Lakini pia kuna watu wanapoteza vitambulisho na baadae kuviona kumbe kunamtu kanakiri namba nakukiachaa.

Wanawake na wanaume wanaokutana na wapenzi wasio waaminifu ambao wanawachukulia vitambulisho bila kujua.

Hii niwazi matapeli hawataisha ila hao DAWA YAO MIMI Enzi na Enzi ninayo hamtakaa muwasikie milele zote. TCRA au makampuni wanitafte
 
Moja ya tatizo kubwa tulilonalo Tanzania ni kutotilia mkazo gharama ya muda na bila kujirekebisha hatutaendelea wala hatutapata wawekezaji makini kila ukienda kwenye huduma za umma au serikali ni lazima upoteze nusu siku au siku nzima

Fact.
Kunasiku napiga simu EWURA nataka kujua bei ya unit moja ya maji kwa matumizi ya majumbani baada ya kuhisi DAWASA wananipiga nashangaa naambiwa niende Ewura kijitonyama!

Nikamwambia jambo kama hili nifunge safari kwenda huko! Wakati Ewura ndi inasimamia nishati zote yakiwemo maji!
Nilikata simu.

Kiukweli bila kuzingatia mda tutapata taabu sana nchi hii.
 
Back
Top Bottom