Ushauri kwa manufaa ya jamii nzima

Ushauri kwa manufaa ya jamii nzima

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kwa kipindi hiki ambapo uhalifu umeongezeka Mtaani waelimishe yafuatayo wanaoshinda nyumbani.

1. Wasiwaamini wasiwaruhusu kuingia ndani wauza urembo.waokota makopo,watembeza nguo na wanaosajili line za simu.

2. Tusiwaamini/tusiwakaribishe ndani warembaji wa kucha na wasugua miguu.

3.Tusiwaamini/tusiwakaribishe ndani wanaopita na bidhaa wakikopesha ili baadae wafuate elfu Moja kila siku.

4.Tusiruhusu maeneo ya jirani na nyumba zetu kuwepo na vijiwe vya bangi.

5.Wenye nyumba za kupangisha Tuwachunguze wapangaji wanaohamia na Vyombo vichache mfano godoro,Jiko na sufuria mbili tu.

6.Toa taarifa ya viashiria vyovyote vya wizi.

7.usiilaze Simu kwenye charge au sehemu ya wazi. Usisahau kuwa na filimbi ndani
8.Usiweke kiasi kikubwa Cha pesa nyumbani.

9. Usiweke vitambulisho vyako muhimu kwenye pochi.

10.Anayeondoka mapema nyumbani asisahau kuwaamsha wenzake ilu wafunge milango kwa mda

11.Punguza Ulevi au acha pombe kabisa.

12.Kwa wenye nyumba ndogo ukienda huko fanya kilichokupeleka tu---

Usimhadidhie siri zako zote mchepuko wako.ikiwemo biashara zako faida, kiasi Cha pesa ulichonacho nyumbani password za ATM namba za siri za M pesa tigo nk huwezi kujua mko wangapi.
 
1. Wasiwaamini wasiwaruhusu kuingia ndani
wauza urembo.waokota makopo,watembeza nguo na wanaosajili line za simu.
2. Tusiwaamini/tusiwakaribishe ndani warembaji wa kucha na wasugua miguu.
Mimi binafsi nimesikia na kuelewa sijui wewe mwenzangu
 
Najua hata kwako huu ushauri huwezi kuufata, au nasema uongo ndugu yangu [emoji38]

Ukinogeshwa mwenyewe tu utaropoka ukute she mwenyewe ni huyu

View attachment 1807228
Najua hata kwako huu ushauri huwezi kuufata, au nasema uongo ndugu yangu [emoji38][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Furaha inatoka wapi kama unaandika mambo ya uhalifu kuongezeka kwa kasi!???

Hii si ni dalili ya kuanza kuishi kwa hofu

Mbona unajikanganya kwenye maelezo mkuu
Uhalifu ni uhalifu na furaha ni furaha usijaribu kuchanganya hivi vitu viwili.. Nilichotoa ni ushauri wa kuongezeka uhalifu si kwamba uhalifu umekuwa tishio..
Hapo kabla uhalifu ulikuwepo na ulifanywa na mamlaka kwa hiyo kilichopo sana ni change of scene
 
Kwa kipindi hiki ambapo uhalifu umeongezeka Mtaani waelimishe yafuatayo wanaoshinda nyumbani.

1. Wasiwaamini wasiwaruhusu kuingia ndani wauza urembo.waokota makopo,watembeza nguo na wanaosajili line za simu.

2. Tusiwaamini/tusiwakaribishe ndani warembaji wa kucha na wasugua miguu.

3.Tusiwaamini/tusiwakaribishe ndani wanaopita na bidhaa wakikopesha ili baadae wafuate elfu Moja kila siku.

4.Tusiruhusu maeneo ya jirani na nyumba zetu kuwepo na vijiwe vya bangi.

5.Wenye nyumba za kupangisha Tuwachunguze wapangaji wanaohamia na Vyombo vichache mfano godoro,Jiko na sufuria mbili tu.

6.Toa taarifa ya viashiria vyovyote vya wizi.

7.usiilaze Simu kwenye charge au sehemu ya wazi. Usisahau kuwa na filimbi ndani
8.Usiweke kiasi kikubwa Cha pesa nyumbani.

9. Usiweke vitambulisho vyako muhimu kwenye pochi.

10.Anayeondoka mapema nyumbani asisahau kuwaamsha wenzake ilu wafunge milango kwa mda

11.Punguza Ulevi au acha pombe kabisa.

12.Kwa wenye nyumba ndogo ukienda huko fanya kilichokupeleka tu---

Usimhadidhie siri zako zote mchepuko wako.ikiwemo biashara zako faida, kiasi Cha pesa ulichonacho nyumbani password za ATM namba za siri za M pesa tigo nk huwezi kujua mko wangapi.
Usalama wa taifa hili ni jukumu la kila mtanzania. Hakika wewe umetimiza wajibu wako wa kutukumbusha sisi raia wema. thanks brother.
 
Back
Top Bottom