Ushauri kwa mkuu wa shule ya sekondari Nyiendo, wilayani Bunda

Ushauri kwa mkuu wa shule ya sekondari Nyiendo, wilayani Bunda

Salaam zikufikie mkuu wa shule ya Sekondari Nyiendo halmashauri ya mji wa Bunda.Kwanza hongera sana kuwabwaga wapinzani wako wa kitaaluma ambao wana kila kitu(Raslimali fedha,walimu wa kutosha,vitendea kazi vya kutosha,majengo ya kutosha nk)BUNDA HIGH SCHOOL katika matokeo ya mtihani wa ukamilifu(mock)kidato cha pili 2023 ambapo shule yako imekuwa ya 04 katika shule 17 zilizo ndani ya halmashauri huku wapinzani wako wakiwa namba 07 .Jambo jema umekuwa namba 02 kwa shule za serikali katika halmashauri.Unastahili Pongezi sana wewe mama,ukweli unapambana sana!Wanaosema umefeli kusimamia taaluma kwa hili nitawapinga kwa Kila namna!Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.Madam Pongezi pia kwa walimu wako wa kidato cha pili kufanikisha kuudondosha mbuyu(BUNDA HIGH SCHOOL) ambao mara kwa mara wamekuwa wakiwakejeli nyie miaka na miaka Kwa kuwapachika jina la Chuo cha Mapenzi.

Binafsi kwangu wewe ni kiongozi mzuri sana Tena sana katika historia ya shule tangu kujengwa kwake 2005 mpaka sasa ila kuna mambo yafuatayo yazingatie ili uzime kelele za wanaokupiga vita na kuongeza ufanisi wa shule.

1.Tahadhali ya kwanza;kuwa makini na mmoja kati ya wasaidizi wako (washauri)wa juu anayetoka kati ya ofisi mojawapo kati ya hizi(Ofisi ya makamu,Taaluma na malezi).Huyu anakufanyia unafiki sana anapokuwa na jamii anakupiga vita sana na hupendelea kutumia maneno "Huyu mama kazeeka awaachie wengine mambo mengi anatufelisha yeye"ila wewe ukiwa nae mnasocialize vizuri huku akikupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.Imefikia hatua watu wameanza kuamini yeye ndie kila kitu katika shule kiasi kwamba bila yeye shule haiwezi kusonga mbele.

2.Penda wale unaoaminishwa ni maadui zako.Walimu wanaohoji hadharani ndani ya vikao siyo maadui kama watu wanaokuzunguka wanavyokuaminisha.

3.Walimu wako wanalalamika unakuwa parade Kila siku kuliko hata mwalimu wa zamu.Hii pia linakupunguzia uzito.Tokea parade wakati wa matukio nyeti tunili kulinda hadhi yako isizoeleke ovyo.

4.Usiingize urafiki kwenye maamuzi.Kuna mwanafunzi(jina kapuni) aliiba vifaa vya Maabara (reagents)ila uliweka ngumu asifukuzwe bali apewe uhamisho huku watoto wengine wa wasio na watetezi wakifukuzwa.Katika kuchunguza ilibainika ni mtoto wa swaiba wako.Hii imekuongezea wakosoaji wengi!Siyo fair madam!

5.Punguza machawa ambao wameanza kukuharibia madam.Kuna mwalimu mmoja wa kike jumatatu wiki iliyopita wakati wa chai alimweleza mwenzake kama ana hoja ampe yeye(chawa)Kisha chawa ataiwasilisha kwako personally maana anakumudu mno anapongea na wewe huwezi kukataa!

6.Fursa zako sasa hivi kwa walimu zinatabirika kabisa.Wape nafasi na wale ambao umeaminishwa ni maadui ili wakusaidie hasa wale 3 dadaz ambao umewatupa!

7.Next time angalia sana umakini katika kuteua bodi ya shule.Jiulize wanakusaidia nini zaidi ya kukuachia mzigo wa mambo mengi huku wao wakinyemelea tu posho!Mbaya zaidi na wao wakiwa nje huku wanasema hushauriki

8.Wajali walimu wa kujitolea(Part time teachers)hawa japo hujawagundua wanapiga kazi sana kuliko walimu wako wa kuajiriwa.Hamasa ya wanafunzi kutoa pesa Kwa ajili ya hawa walimu haipo.Miezi mitatu iliyopita mlikusanya 64000=mkawaita hawa walimu ambao idadi yao ni walimu nane mkawagawanyisha 8000\=kwa kila mmoja hii siyo haki. Wewe au walimu wako ni nani kati yenu anaweza kuishi Kwa 8000 Kwa mwezi?Pia mmewatenga sana huku mkiwazuia kutoa adhabu Kwa watoto wakorofi matokeo yake wanaishi na wanafunzi kama 'chibaba na chimamy' wake. Kauli zako maarufu "wewe chapa tu likikufika utalimaliza mwenyewe"

9.Kama utaweza vunja ofisi ya taaluma weka wapya.Hapa sihitaji kukufafanulia zaidi ila ivunje kwa maslahi ya shule au wabadilishie idara.Pkease vunja hii ofisi,usiogope kuanza upya

10.Washauri walimu wako wawe pia wanahudhuria vikao vya ofisini(staff meetings)badala ya kuvipuuza na kuishia kulalamika tu.


Bado nina imani nawe Kwa 100% pia naamini Shule ya Sekondari Nyiendo chini ya uongozi wako ipo kwenye mikono salama kabisa.Wewe ni kiongozi mzuri na Bora kabisa mamaangu ila unamruhusu shetani akushinde!Badilika ili ule ukale pensheni yako vizuri na wajukuu siku za baadae kule same kwenye milima ya "upareni"
Huyo mwalimu yupo humu?
 
Back
Top Bottom