Ushauri kwa mliopo JKT wa kujitolea (WAZALENDO)

Aaah sio kweli...hapa bongo usalama ndo wanaongoza kwa mshahara na malupulupu
usiishi kwa kukalili... Jeshi wapo juu...na wana favor nyingi kuliko wote...inawezekana unapima uwezo wa mtu kwakuwa ni kiongozi huko USALAMA...

anzia posho za askari wa chini PRIVATE...​
 
walau umenielewa... asante kwa appreciate yako...! japo ulicho kiandika ndio uhalisia...!​
 
Jeshini tulifundishwa Somo la ujanja wa porini, umuone adui kabla hajakuona na hapo unaruhusiwa Ata kutoroka kwenye kazi ila hakikisha hawajakuona, Sasa Kila kitu wewe unakuwa kimbelembele utasota Sana, na utajila na kujivuna Hadi uchakae
 
Nilikuja kulujua hilo baadae sana, binafsi nilikuwa napenda sana u sniper, nilikua nasema lazima nikikua nitaenda kuwa sniper kumbe najidanganya
 
Jeshini tulifundishwa Somo la ujanja wa porini, umuone adui kabla hajakuona na hapo unaruhusiwa Ata kutoroka kwenye kazi ila hakikisha hawajakuona, Sasa Kila kitu wewe unakuwa kimbelembele utasota Sana, na utajila na kujivuna Hadi uchakae
MMU huwezi kuiapply kwenye maisha harisi ya kambini ama mafunzoni...utapotea na awato kwambia kuwa umepotea...!​
 
Hello brother, nimatumaini yangu uko salama
Naomba niulize kuhusu JWTZ

1. NI LAZIMA UPITE JKT KWENDA JWTZ?
2. NI LAZIMA UKAE JKT MIAKA 2 NDIO UWEZE KWENDA JWTZ?
3. KIPINDI CHA KOZI YA JKT UNAWEZA PATA FURSA YA KUINGIA JWTZ ?
JE MINIMUM NI BAADA YA MDA GANI IZO FURSA ZA JWTZ HUANZA KUJA KAMBINI?
4. UKIPATA FURSA YA KUJIUNGA JWTZ UNAENDA MAFUNZO KWA MDA KIAS GANI?
5.BAADA YA KUPATA MAFUNZO YA AWALI JWTZ KWA KAWAIDA UNAKUA KWENYE LEVEL IPI YA JESHI?
6. UKIWA JWTZ UNAWEZA KWENDA KUSOMA NDANI AU NJE YA TANZANIA?
7. IF YES NI BAADA YA MDA GANI WA KUWA JWTZ UTAWEZA KUENDELEA NA MASOMO?
8. JWTZ UKIWA MASOMO BADO UTAINGIZIWA SALARY YAKO YA KILA MWEZI?

NI HAYO TU BROTHER KWA LEO
THANKS YOU IN ADVANCE!
 
ndugu yangu usikilizi hata vyombo vya habari🤣🤣🤣

1. bunge la mwaka huu limeamua kuondoa kigezo cha JKT kwenye ajira za majeshi yote. hivyo kupata usajili ndani ya JWTZ hakutegemei uwe na JKT.

2.Hapana... kigezo hiki kimepitwa na wakati kimetenguliwa na bunge.

3. Ndio unaweza kukutana na fursa kama ukibahatika kuingia Jkt fursa ikakukuta huko huko...hazina muda maalum japo ni mpaka pale kuruta wa JKT watakapo fuzu na kuwa service man/girl... muda wowote nafasi zikitoka unafanya interview ukibahatika unasajiliwa jeshini..!

4. mafunzo ya JWTZ huwa ni miezi 3. level za juniors kuna level 1,2 na 3... kila level inapigwa kwa muda wake tofauti ila mafunzo ya awali ni miezi 3 tu...!

5. unatambulika kama junior au private...!

6. ukisha sajiliwa jeshini sahau kuhusu safari za nje ya nchi... japo unaweza kwenda kusoma popote ulimwenguni kama jeshi likikutuma...! elimu unazoweza kusoma nje ya nchi ni elimu maalum za Jeshi...!

7. kusoma unasoma muda wowote endapo utakuwa na nafasi hiyo... maana kuna vitengo vinabana jeshini unaweza kujikuta unapata muda wa kulala tu ukiamka kazini🤣🤣🤣 hivyo ukiweza kukimbizana na muda wa kijeshi unaruhusiwa kusoma elimu za hapa hapa nchini kwa elimu zetu hizi za kiraia sijui, certificate, diploma, degree au master's...! japo jeshini napo kuna elimu zao... maalum ambazo huwezi kuzisoma kama wewe sio mwanajeshi...! mfano kurusha ndege za kivita... sayansi za kivita, sayansi ya utengenezaji wa silaha... elimu za kijeshi pia zina certificate, diploma, degree, masters na kuendelea usimuone mtu kawa mkuu wa Majeshi ukamchukulia poa...!

8. sijalielewa... ila kwa kifupi ukishasajiliwa hapo hapo unaanza kupata posho... hadi pale utakapo hitimu...!
 
Pamoja na kutokupenda kazi inayohusu mafunzo ya jeshi pia huwa sipendi kazi ya kumlinda mwenzangu hata kidogo.

Yaani nisifikirie kuzungukwa na walinzi nianze kupitia usumbufu woote huo eti ili nikamlinde mwenzangu (kuwa kwenye msafara)?
 
Pamoja na kutokupenda kazi inayohusu mafunzo ya jeshi pia huwa sipendi kazi ya kumlinda mwenzangu hata kidogo.

Yaani nisifikirie kuzungukwa na walinzi nianze kupitia usumbufu woote huo eti ili nikamlinde mwenzangu (kuwa kwenye msafara)?
sio kila unacho tarajia unakipata... maisha ni kama tairi... ni rahisi kuwa chini au juu ina tegemea mzinguko,🤭🤭🤭​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…