Mcqueenen
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 6,843
- 11,702
Aaah sio kweli...hapa bongo usalama ndo wanaongoza kwa mshahara na malupulupuWANAJESHI kwenye mishahala wapo juu fuatilia vizuri wame wazidi taasisi zote za Ulinzi...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aaah sio kweli...hapa bongo usalama ndo wanaongoza kwa mshahara na malupulupuWANAJESHI kwenye mishahala wapo juu fuatilia vizuri wame wazidi taasisi zote za Ulinzi...
Aaah sio kweli...hapa bongo usalama ndo wanaongoza kwa mshahara na malupulupu
Hongera kwa bandiko lako,hili bandiko lilifaa miaka iliyopita,kwa sasa inaanza connection hayo mengine ni baada ya message kuisha.Yote kwa yote wayazingatia haya uliyowaambia.
Uzalendo ilikuwa miaka hiyo sasa hivi tunasaka ajira,mtu amemaliza chuo ajira hakuna option iliyobaki ni jeshi,wazalendo wachache sana.
Posho zote wanazopewa jeshi na usalama wanapewa, ila usalama Wana posho zingine nyingi ambazo jeshi hawapewiusiishi kwa kukalili... Jeshi wapo juu...na wana favor nyingi kuliko wote...inawezekana unapima uwezo wa mtu kwakuwa ni kiongozi huko USALAMA...
anzia posho za askari wa chini PRIVATE...
Kimbilio la walioshindwa maisha hilo.Hii kazi sijui mnaipendea nini walahi..🙌😂😂😂
Aisee watu tumetofautiana...
Wamewazidi hao wenzao wa ulinziWANAJESHI kwenye mishahala wapo juu fuatilia vizuri wame wazidi taasisi zote za Ulinzi...
Nilikuja kulujua hilo baadae sana, binafsi nilikuwa napenda sana u sniper, nilikua nasema lazima nikikua nitaenda kuwa sniper kumbe najidanganyaHapana hujichagulii bali elimu yako na kipaji chako ndio itaamuwa pa kukupeleka...japo kuna muda huwa kuna amri za Lazima ikitokea uhitaji wawatu wenye ujuzi fulani.
Hivyo kitatafutwa kikundi cha watu wenye sifa na wasio na sifa ili wafanikishe hiyo kazi...!
Jeshini tulifundishwa Somo la ujanja wa porini, umuone adui kabla hajakuona na hapo unaruhusiwa Ata kutoroka kwenye kazi ila hakikisha hawajakuona, Sasa Kila kitu wewe unakuwa kimbelembele utasota Sana, na utajila na kujivuna Hadi uchakae
Hello brother, nimatumaini yangu uko salamaNdugu zangu kwanza niwapongeze sana kwa moyo wenu wa pekee wa kutamani kwa dhati kabisa kuitumikia nchi yetu richa ya JESHI LA KUJENGA TAIFA kujidhatiti dhahiri kuwa awatoi Ajira😭😭😭
Kitendo cha JKT kutoa Rai kuwa awatoi Ajira huo ni kama mchujo wa kwanza tunaita🤣🤣🤣🤣 kwa ambae hatolizika maana yake hato jiunga, kwa MZALENDO wa dhati atapiga hatua mbele bila kujali kuwa hato pata Ajira.
Ili uweze kufanikiwa JKT kuna vitu vichache ambavyo ukivizingatia huwezi kurudi nyumbani bila ajira.
Ieleweke kuwa mchujo wawatu watakao sajiliwa kwenye ajira huanzia pale utakapo karibishwa ndani ya kambi ya JKT uliyo pangiwa. vitu vingi uzingatiwa
i. Kwenda na muda ulio pangwa kuwasili kambini ukichelewa itakula kwako bora uwahi.
ii. Kuwa na vifaa vinavyo endana sawa sawa na ulivyo agizwa ili kuruka kiunzi hiki ni bora ukabeba pesa na kwenda kununua vifaa huko huko kambini uliko pangiwa. maduka yaliyopo jirani na kambi huwa na vifaa vyote vinavyo hitajika.
iii. Kutokubeba vitu vya ziada ambavyo hujaagizwa.
Baada ya kupokelewa kwenye kambi za JKT kuna makatazo na sheria za JKT mtasomewa na kueleweshwa hizo ni za kuzizingatia sana kwani ndio zitakazo waongoza maisha yenu yote ndani ya kambi.
ukifanikiwa kuruka kiunzi cha hapo juu bado utatakiwa kuyaishi maisha vizuri ndani ya kambi kama ifuatavyo.
1. UTIIFU unapo pangiwa kazi fanya kama mtumwa maliza kazi ya watu mapema huku mwili wako ukiwa teyari kusubiri order nyingine. USIONYESHE umechoka though ni kweli kuwa wewe sio mashine ila jifunze kumtumikia kafiri upate mradi wako.
2. SUBIRA kuna muda ndani ya kambi inaweza kutolewa order na afande tumwite Coplo kuwa msiondoke hadi atakapo rudi kwa kihere here baada ya masaa mengi kupita mkidhani amewasahau mnaamu kutawanyika😭😭😭 mchujo unaanzia hapo
3. NIDHAMU uoga na nidhamu ni vitu viwili tofauti askari yeyote anafundishwa ujasiri sio uoga. kutokana na sababu mbali mbali kwenye kambi za JKT kumekuwa na madalaja yamewekwa kati ya viongozi wa kati ndani ya kambi na viongozi waandamizi. viongozi wa Kati ambao ndio wapo field muda wote na Kuruta huwa awapendi sana KURUTA wasogelee au kuzoea sehemu za viongozi WAANDAMIZI jambo hili huwafanya KURUTA kuwa na uoga pindi wakutanapo na viongozi WAANDAMIZI.
Kuruta atashindwa hata kujieleza pindi akutanapo na kiongozi MUANDAMIZI ndani ya kambi. mimi nikuondoe hofu ukipata nafasi ukakutana na kiongozi MUANDAMIZI kambini usiogope kuzungumza nae kwa NIDHAMU. anaweza akaja Afande akakupiga bila sababu ama akakupa adhabu matharani ya kupiga push_up au kuibeba dunia fanya hiyo adhabu uliyo pewa bila manung'uniko na usijenge chuki na mkufunzi yeyote kambini hata kama ana kuonyesha chuki ya Wazi kabisa.
Ndani ya kambi mpende sana yule Afande atakae jitolea kukuchukia kwa kukupa adhabu, kukutukana, kukukejeli ama kukusimanga. Afande huyu ndie mwenye funguo za AJIRA yako.
Ila muogope sana AFANDE ambae ukifanya kosa atakufundisha namna ya kuchomoka kwenye hilo kosa bila kukupa Adhabu,
Muogope afande ambae anaweza akakuona unapita kwenye njia zisizo Rasmi {UNAJONGOMEA} na aka kuacha kama ajakuona...😭😭😭 huyu atakumaliza chini kwa chini na huto fika popote.
Ikitokea umekamatwa pengine ukawekwa mahabusu au umekutwa na kosa lolote lile ambalo limepelekea upewe adhabu hakikisha unaifanya hiyo adhabu bila kuonyesha kuwa umeonewa na baada ya kuimaliza hiyo adhabu kaa mbali na jambo lililokufanya upewe adhabu kifupi badilika ili ata yule alie kupa adhabu aone kuwa adhabu yake imekubadili tabia na kuwa mtu bora zaidi. usipo badilika watakuacha na utajipotezea muda bure.
Jitahidi sana kwenye roll call za usiku, siku za sikukuu ama Ijumaa, Jumaamosi na Jumaapili usikosekane. ukitokea mmepewa kazi nzito siku hiyo kimbilia kufanya hiyo kazi ama chochote kitakacho fanywa siku hizo hakikisha unashiriki.
✓ Muda wa kupumzika mkiwa mmechoka kweli kweli ghafra wakiitwa watu 20 pangeni foleni. piga ua gara gara hakikisha kwenye hilo kundi uwepo.
✓ Mkiwa kwenye starehe zenu akaja Afande akaomba askari 30 waende kumsaidia kushusha magunia ya mahindi jitahidi uwe miongoni mwa hilo kundi.
Hivyo ndivyo watu hupoteaga na wasionekane siku unakuja kukutana nae yupo kwenye msafara wa viongozi unabaki mdomo wazi🤭🤭🤭🤭
N.B
kwenye haya maisha yetu kitu ukikipenda sana hukipati.
hivyo jitahidi ukilipenda sana jeshi wakufunzi wako wasijue kwani wakijua kuwa wewe ni mfia jeshi possibility za kukosa huwa ni kubwa.
lipende jeshi ndani ya moyo sio nje ya moyo... ukilipenda nje ya moyo kila mtu atajua na huo ndio mwanzo wa kulikosa.
inajulikana kuwa WANAJESHI WA KWELI, WANAO LIPENDA JESHI KWA DHATI KABISA WAPO MITAANI, awajawahi kusajiliwa😭😭😭😭
ndugu yangu usikilizi hata vyombo vya habari🤣🤣🤣Hello brother, nimatumaini yangu uko salama
Naomba niulize kuhusu JWTZ
1. NI LAZIMA UPITE JKT KWENDA JWTZ?
2. NI LAZIMA UKAE JKT MIAKA 2 NDIO UWEZE KWENDA JWTZ?
3. KIPINDI CHA KOZI YA JKT UNAWEZA PATA FURSA YA KUINGIA JWTZ ?
JE MINIMUM NI BAADA YA MDA GANI IZO FURSA ZA JWTZ HUANZA KUJA KAMBINI?
4. UKIPATA FURSA YA KUJIUNGA JWTZ UNAENDA MAFUNZO KWA MDA KIAS GANI?
5.BAADA YA KUPATA MAFUNZO YA AWALI JWTZ KWA KAWAIDA UNAKUA KWENYE LEVEL IPI YA JESHI?
6. UKIWA JWTZ UNAWEZA KWENDA KUSOMA NDANI AU NJE YA TANZANIA?
7. IF YES NI BAADA YA MDA GANI WA KUWA JWTZ UTAWEZA KUENDELEA NA MASOMO?
8. JWTZ UKIWA MASOMO BADO UTAINGIZIWA SALARY YAKO YA KILA MWEZI?
NI HAYO TU BROTHER KWA LEO
THANKS YOU IN ADVANCE!
Pamoja na kutokupenda kazi inayohusu mafunzo ya jeshi pia huwa sipendi kazi ya kumlinda mwenzangu hata kidogo.
Yaani nisifikirie kuzungukwa na walinzi nianze kupitia usumbufu woote huo eti ili nikamlinde mwenzangu (kuwa kwenye msafara)?
Ila wanasema huko kuna maslahi makubwaKazi ya watu walioshindwa maisha ,hiyo ndio option yao ya mwisho.
Mateso kibao,kuvuliwa utu wako unakuwa mtu wa kunyenyekea muda wote kamshahara kenyewe ni kaduchu.
Ila wanasema huko kuna maslahi makubwa
Ila wanasema huko kuna maslahi makubwa
Ila wanasema huko kuna maslahi makubwa