Ushauri kwa mliopo JKT wa kujitolea (WAZALENDO)

Ushauri kwa mliopo JKT wa kujitolea (WAZALENDO)

Kipindi nakua nilikuwa napenda sana jeshi na kwa akili zangu nilikuwa najua vitengo unajichagulia kadri upendavyo.
Hapana hujichagulii bali elimu yako na kipaji chako ndio itaamuwa pa kukupeleka...japo kuna muda huwa kuna amri za Lazima ikitokea uhitaji wawatu wenye ujuzi fulani.

Hivyo kitatafutwa kikundi cha watu wenye sifa na wasio na sifa ili wafanikishe hiyo kazi...!​
 
Duh, halafu ukipata ajira unapelekwa Congo unapigwa risasi unakufa.

Hakuna kazi sipendi kama zinazohusiana na ulinzi
kulinda amani ni miongoni mwa kazi za jeshi...jeshi ni sehemu pekee ambayo mtu anasaini hati ya kifo chake...!​
 
Halafu ukimaliza yote haya wanakutupa Suma Ukalinde mnara huko Mbinga milimani na kibegi chako na salary ya laki tatu.
wapo wanao bahatika...lakini hata huko suma kuna vitengo watu wanapiga maisha....!​
 
Hii kazi enzi zile tulikua kama umesoma kidogo tunaikimbia dah... naskia vijana siku hizi weji digiriii zao wanatoa mpaka kitu chochote wazame.
kuanzia 2010 kurudi nyuma jeshi lilikuwa na posho ndogo sana, hii iliwafanya wanajeshi waonekane watu wa kawaida sana.

ila baada ya mabomu yaliolipukaga ya mbagala, na gongo la mboto. pamoja na ujio wa Barraka Obama nchini kulibadilisha taswira ya JESHI.

posho zika pandishwa kwa asilimia 100% ikawa ni sehemu yenye mshahala mnono. taasisi zote za Ulinzi hakuna wanao wazidi wanajeshi kwa Malupu lupu... hata USALAMA wenyewe awana maisha kuwazidi wanajeshi...!

hiko ndicho kilicho pelekea jeshi kuwa kimbilio la wengi🤣🤣🤣🤣​
 
Duh, halafu ukipata ajira unapelekwa Congo unapigwa risasi unakufa.

Hakuna kazi sipendi kama zinazohusiana na ulinzi
Kabisa.... [emoji2][emoji2][emoji2] yaan tuachane na hayo ukmalza unapelekwa congo risas 1 chali ...ebana
 
Mtu katoa rushwa milioni 1-2 leo hii umwite mzalendo?

Vijana wa kujitolea JKT wote wameenda huko baada ya kutoa rushwa mikoani kwao na wengine wameenda kwa nguvu za viongozi wa mkoa na wilaya au viongozi wa jeshi ambao ni ndugu zao.

Kwahiyo hakuna mzalendo mtoa rushwa au mzalendo wa kwenda JKT kwa kimemo.

Amekwenda kwa nguvu zake na wazazi wake acha kumpangia au kujifanya kumpa ushauri.

Nimekwenda JKT miaka zaidi ya kumi imepita , hakuna mzalendo kule wote wanataka ajira na kuingia kule lazima ucheze rough.
unaweza ukacheza rough kama ulivyo sema na bado ukakosa...jeshi hutakiwi kulipenda kwa kujionyesha. lipende ndani kwa ndani ila ile dhana ya watu kuwafuata wakubwa kuwaomba nafasi ndio inayo waogopesha hao wakubwa.

usipo lipenda ukawa Normally tu amini atajitokeza mtu atajitolea kukusaidia usajiliwe. ila ni mpaka vigezo nilivyo viainisha hapo juu uwe umevizingatia.

nikumegee siri tu jeshi ni sehemu pekee ambayo taarifa huwa inatangulia kusambaa kabla mtendaji hajaonekana...!

unaweza ukafanya kituko ukidhani ni siri baina yako na na MP....au Matron kumbe wazako wakikaa sehemu zao za kujidai wanamjadiri KURUTA mmoja mmoja🤣🤣🤣​
 
Hongera kwa bandiko lako,hili bandiko lilifaa miaka iliyopita,kwa sasa inaanza connection hayo mengine ni baada ya message kuisha.Yote kwa yote wayazingatia haya uliyowaambia.
Uzalendo ilikuwa miaka hiyo sasa hivi tunasaka ajira,mtu amemaliza chuo ajira hakuna option iliyobaki ni jeshi,wazalendo wachache sana.
 
Back
Top Bottom