Ushauri kwa NECTA: Usimamizi wa mitihani kwa shule za Sekondari na Msingi

Ushauri kwa NECTA: Usimamizi wa mitihani kwa shule za Sekondari na Msingi

Sasa wasiokuwa na ajira wana izoefu gani katika hiyo kazi?? Maana kusimamia mtihani sio kama kusimamia mafundi ujenzi site.Halafu asokuwa naa ajira huwezi kumbana hata akiharibu kazi maana kwanza hana cha kupoteza,liwalo naa liwe.Kazi za anwani ya makazi mmeboronga sana,jamaa wanajutia sana.
Safi saana
 
Mkuu nakubaliana na wewe, nilikuwa kwenye usimamizi wa mtihani darasa la Saba mwaka huu, Mkuu wa shule niliyokuwepo alilalamika sana kusikia kuwa wasimamizi wake Ni walimu wa sekondari, hii Ni kutokana na mazoea ya wakuu kutegemea cheating wakati wa mitihani, nakubaliana na necta , huu mfumo Ni mzuri kwa 99.999%
Aisee naona ilikuwa ndio tabia zao Bora mfumo wa Sasa kama ndio hivyo
 
1. Walimu wa sekondari ni wasimamiz wakuu katika mitihani YOTE,, walimu wa msingi ni wasimamiz wa ndani/ mikondo.. Hiyoo senario ya huyo mtoto inamuhusu msimamizi wa mkondo
2. Huo usomaji wa hizo imla unafanywa na wasimamizi wa mikondo ambao ni walimu msingi
3.Mtihani wa msingi hufanyika kwa siku 02. Na sekondari hufanyika kwa 7-21,, hiyoo gharama ya huduma ni kubwa
4..walimu wa msingi hushirikiana katika wizi wa mtihani,, kwa hii miaka miwili wizi w mitiah umepungua kwa asilimia kubwa
NB.NECTA KKAZENI HAPO HAPO DAWA INAINGIA
Mwaka huu wasimamizi wote wa darasa la nne na saba ni walimu toka sec.tofauti na mwaka jana wasimamizi wa mikondo darasa la saba walikuwa kutoka msingi na wasimamizi wakuu sec
 
Habari watanzania!

Hivi karibuni Katibu mkuu wa NECTA aliyepita sasa ni naibu katibu mkuu TAMISEMI, ametuachia jambo geni kwenye usimamizi wa mitihani.anyway labda lina tija au wapo kwenye utafiti wa mfumo sijui kwanza nikwamba zamani ilikuwa walimu wa SEKONDARI walisimamia mitihani ya SEKONDARI na msingi walimu wao ndio walikuwa wasimamizi,

Hivi karibuni ni mwaka wa tatu sasa wasimamizi wa mitihani imekuwa mabadilishano wa msingi wanasimamia SEKONDARI na wa SEKONDARI wanasimamia shule za msingi.

Yaani darasa la nne na la saba wasimamizi ni walimu wa sekondari
Na kidato cha pili na cha nne wasimamizi ni walimu wa shule za msingi. Sina shida na kiwango cha elimu Bali uzoefu wao na wanafunzi wao nikigezo cha kuzingatia.

Yawezekana ni kwa sababu ya sera ya Elimu msingi inajumuisha elimu ya msingi na Sekondari.

Sasa tashwishi imekuwa ni kupungua kwa usimamizi madhubuti, (learner)kutokana na kukosea kwa wasimamizi katika kufanya mambo yao ya usimamizi ndani ya chumba cha mtihani,

Chanzo changu kimebaini makosa yafuatayo.

1. Wasimamizi wengi wa sekondari wanashindwa kusoma habari au imla kama inayo paswa kwa wanafunzi wa darasa la nne au la saba hivyo kupeleka swali hilo wanafunzi wengi kukuosa ama kupata alama za chini yaani msimamizi anasoma kwa slang ,kumeza Maneno au kwa fonolojia sasa wanafunzi hao na umri wao si sawa pace inatakiwa iwe ndogo na taratibu kwa kusoma neno kama lilivyo.

2. Nyaraka za mitihani zinazo tumika msingi ni tofauti na SEKONDARI hivyo kupata makosa mengi kama yaliyotokea hivi karibuni huko chalinze.
Yule binti alimwambia msimamizi hii si namba yangu lakini yawezekana msimamizi alimdharau mtahiniwa kwa kuwa ni darasa la saba na mdogo na yeye ni msomi wa DIPLOMA au degree so ataniambia mini huyu.
Pia yawekana aliingia hofu kwamba pengine ni mbona za wizi ndo maana alikomaa ni mawazo yangu.

3. Haiba na wasifu wa walimu wa SEKONDARI nikuona mwanafunzi anafuata maelekezo kwa ufasaha na ni wakali kutokana na wanafunzi wanaowafundisha wakiwa adolescent age huko SEKONDARI sasa hawa huku wa msingi ni wadogo saana hivyo mtoto akikosea jambo au kutofuata maelekezo ya mitihani sauti zao ni kali hivyo kuleta hofu na woga hasa darasa la nne ambao umri wa ni miaka 9, au 10 hadi 11 ni wadogo hivyo kupelekea kufanya vibaya ama chini ya kiwango hata kama watafauli

Huko SEKONDARI wasimamizi kutoka msingi (walimu) wanalazimika kujionesha kama wanajua kwa kuanza kutafasiri maswali ndani ya chumba cha mtihani badala ya kusimamia tu .
Kwa wema tu na uzalendo

naomba utaratibu huu uvunjwe urudi kama kawaida zamani msingi wasimamie msingi na SEKONDARI wasimamie sekondari due to experience ya hao wasimamizi.

Kama hili linatija basii napendekeza

1. Semina za usimamizi ziongezwe muda walau siku tatu 3 ama nne 4 ili wahusika wapate uzoefu na elimu ya kutosha ili kwa malachi ya taifa tufanye vizuri kabisa pasipo kumuonea huyu mwanafunzi

2. Kuwe na mitihani katika semina ili wanaofauli ndo wapitishwe kusimamia maana walimu wanatofautiana uelewa na ushapu wa ku grasp knowledge hao watakao feli wasipewe nafasi mpaka watakapo elewa.

Nakaribisha mawazo ili chombo hiki ambacho ni mhimili wa taaruma nchini kiweze kuandaa kizazi kijacho kwa maslahi ya nchi pia kama wamefanya utafiti sawa kila raheli sasa itabidi yale mapungufu yarekebishwe.

Naomba kuwasilisha.
wizi wa mitihani ni utamaduni
kuongeza muda wa semina kuna husiana vipi na wizi wa mitihani?
kuweka mitihani kwa wasimamizi yote hayo porojo tu
issue pale ni suala la UADILIFU na UTAMADUNI BASI
 
Utaratibu huo uendelee wizi umepungua sana huko primary,nilisikia kuna semina moja walimu wa primary wanalazimisha kuwa imla inatakiwa kusomwa mara nne,kitu ambacho waseminishaji walipinga na kuagiza imla isomwe kulingana na maelekezo ya mtihani husika badala ya kukalili kuwa lazima iwe mara 4,aliyeleta utaratibu huu ni muungwana kwani amepunguza mazoea katika kazi.
 
Sanyambila,
Lengo pekee la NECTA kubadili utaratibu wa usimamizi wa upimaji na mitihani ya Taifa ni kudhibiti udanganyifu katika mitihani ambao ni pamoja wizi wa mitihani unaopelekea kuvuja kwa mitihani kwa njia ya kuwapatia majibu watahiniwa.

Japokuwa tatizo hili limekuwepo kwenye karibia levo nyingi za elimu, shule za msingi tatizo ni kubwa zaidi kuliko levo nyingine.

Ni rahisi kuwakuta vijana wanaoingia kidato cha kwanza hawajui kusoma wala kuandika na wanasema bila kuficha kuwa walipatiwa majibu ya maswali ya mtihani na walimu wao.

Katika kukabiliana na janga hili, NECTA walifanya majaribio kupima ufanisi kwa kuafanya mabadiliko hayo. Na huu si mwaka wa tatu bali ni wa pili.

Yaani wanaohusika kumuandaa mwanafunzi darasani wasihusike pia kuwasimamamia wanapofanya mitihani.

Na hii imeleta tija kubwa kuliko mapungufu.

Walimu wa shule za msingi wanawasaidia wanafunzi wao hata ndani ya chumba cha mtihani. Mtihani unaweza usivuje ngazi zote lakini ukaenda kuvujia ndani ya chumba cha mtihani kwa mwalimu kutoa majibu kwa wanafunzi.

Na imebainika kupitia majaribio haya kubadili mfumo wa usimamizi kuwa si rahisi sana mwalimu wa shule ya msingi anaweza kutoa majibu kwa mitihani ya sekondari.

Na mwalimu wa sekobdari hana haja ya kumpatia majibu mtahiniwa wa darasa la nne au saba ili aje kumpokea sekondari akiwa hajui kusoma na kuandika.

Changamoto ulizozitaja zinatatulika kupitia miongozo na semina zinazotolewa na Kamati za mitihani ambapo mwalimu harusiwi kupewa jukumu la kusimamia ikiwa hajapata semina.

Utaratibu huu uendelee, jukumu la mwalimu liwe kumuandaa nwanafunzi wake lakini la kumsimamia mtihani lifanywe na mwalimu kutoka ngazi nyingine.

Changamoto iliyopo ni kwamba idadi ya shule za msingi ni nyingi kuliko za sekondari, hii inaleta mgongano wa kimaslahi kwakuwa kuna uwezekano mkubwa walimu wengi wa sekondari wakapata nafasi ya kusimamia shule za msingi na idadi ndogo ya walimu wa shule za msingi ikapata fursa hiyo na hivyo kujenga uhasama baina ya ngazi hizo.
 
Mwaka huu wasimamizi wote wa darasa la nne na saba ni walimu toka sec.tofauti na mwaka jana wasimamizi wa mikondo darasa la saba walikuwa kutoka msingi na wasimamizi wakuu sec
Sio kweli,mbona me wa sec but wasimamiz wangu wa ndani walikuwa s/m kasoro mmoja tu wa sec.
 
Necta wamefanya vizuri sana,kama utaratibu ni huo waendelee nao wasibadilishe..
 
Sio kweli,mbona me wa sec but wasimamiz wangu wa ndani walikuwa s/m kasoro mmoja tu wa sec.
Halmashauri yetu darasa la nne na saba wasimamizi wote ni kutoka sec na kidato cha pili na nne wasimamizi wakuu ni kutoka sec wasimamizi wasaidizi kutoka shule za msingi mwaka 2022.
 
Back
Top Bottom