Ushauri kwa NECTA: Usimamizi wa mitihani kwa shule za Sekondari na Msingi

Safi saana
 
Aisee naona ilikuwa ndio tabia zao Bora mfumo wa Sasa kama ndio hivyo
 
Mwaka huu wasimamizi wote wa darasa la nne na saba ni walimu toka sec.tofauti na mwaka jana wasimamizi wa mikondo darasa la saba walikuwa kutoka msingi na wasimamizi wakuu sec
 
wizi wa mitihani ni utamaduni
kuongeza muda wa semina kuna husiana vipi na wizi wa mitihani?
kuweka mitihani kwa wasimamizi yote hayo porojo tu
issue pale ni suala la UADILIFU na UTAMADUNI BASI
 
Utaratibu huo uendelee wizi umepungua sana huko primary,nilisikia kuna semina moja walimu wa primary wanalazimisha kuwa imla inatakiwa kusomwa mara nne,kitu ambacho waseminishaji walipinga na kuagiza imla isomwe kulingana na maelekezo ya mtihani husika badala ya kukalili kuwa lazima iwe mara 4,aliyeleta utaratibu huu ni muungwana kwani amepunguza mazoea katika kazi.
 
Sanyambila,
Lengo pekee la NECTA kubadili utaratibu wa usimamizi wa upimaji na mitihani ya Taifa ni kudhibiti udanganyifu katika mitihani ambao ni pamoja wizi wa mitihani unaopelekea kuvuja kwa mitihani kwa njia ya kuwapatia majibu watahiniwa.

Japokuwa tatizo hili limekuwepo kwenye karibia levo nyingi za elimu, shule za msingi tatizo ni kubwa zaidi kuliko levo nyingine.

Ni rahisi kuwakuta vijana wanaoingia kidato cha kwanza hawajui kusoma wala kuandika na wanasema bila kuficha kuwa walipatiwa majibu ya maswali ya mtihani na walimu wao.

Katika kukabiliana na janga hili, NECTA walifanya majaribio kupima ufanisi kwa kuafanya mabadiliko hayo. Na huu si mwaka wa tatu bali ni wa pili.

Yaani wanaohusika kumuandaa mwanafunzi darasani wasihusike pia kuwasimamamia wanapofanya mitihani.

Na hii imeleta tija kubwa kuliko mapungufu.

Walimu wa shule za msingi wanawasaidia wanafunzi wao hata ndani ya chumba cha mtihani. Mtihani unaweza usivuje ngazi zote lakini ukaenda kuvujia ndani ya chumba cha mtihani kwa mwalimu kutoa majibu kwa wanafunzi.

Na imebainika kupitia majaribio haya kubadili mfumo wa usimamizi kuwa si rahisi sana mwalimu wa shule ya msingi anaweza kutoa majibu kwa mitihani ya sekondari.

Na mwalimu wa sekobdari hana haja ya kumpatia majibu mtahiniwa wa darasa la nne au saba ili aje kumpokea sekondari akiwa hajui kusoma na kuandika.

Changamoto ulizozitaja zinatatulika kupitia miongozo na semina zinazotolewa na Kamati za mitihani ambapo mwalimu harusiwi kupewa jukumu la kusimamia ikiwa hajapata semina.

Utaratibu huu uendelee, jukumu la mwalimu liwe kumuandaa nwanafunzi wake lakini la kumsimamia mtihani lifanywe na mwalimu kutoka ngazi nyingine.

Changamoto iliyopo ni kwamba idadi ya shule za msingi ni nyingi kuliko za sekondari, hii inaleta mgongano wa kimaslahi kwakuwa kuna uwezekano mkubwa walimu wengi wa sekondari wakapata nafasi ya kusimamia shule za msingi na idadi ndogo ya walimu wa shule za msingi ikapata fursa hiyo na hivyo kujenga uhasama baina ya ngazi hizo.
 
Mwaka huu wasimamizi wote wa darasa la nne na saba ni walimu toka sec.tofauti na mwaka jana wasimamizi wa mikondo darasa la saba walikuwa kutoka msingi na wasimamizi wakuu sec
Sio kweli,mbona me wa sec but wasimamiz wangu wa ndani walikuwa s/m kasoro mmoja tu wa sec.
 
Necta wamefanya vizuri sana,kama utaratibu ni huo waendelee nao wasibadilishe..
 
Sio kweli,mbona me wa sec but wasimamiz wangu wa ndani walikuwa s/m kasoro mmoja tu wa sec.
Halmashauri yetu darasa la nne na saba wasimamizi wote ni kutoka sec na kidato cha pili na nne wasimamizi wakuu ni kutoka sec wasimamizi wasaidizi kutoka shule za msingi mwaka 2022.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…