Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Nilichoona na kuamua kuzinduka ni kwamba ukiwa na hoja yoyote kwenda popote basi taarifa inafika vizuri, haraka na kwa uzito kupitia Jamiiforums kuliko njia zingine za kiprotokali zinazowekwa na wahusika
Leo naomba NMB wachuje ushauri huu
1. Mtu akifanya miamala kwa nmb mkononi huwa mnatoa risiti on the spot, jambo jema sana hili. Lakini hebu muwe mnaonesha na salio lililopo kabisa (balance) kwenye hiyo risiti
2. Mtu anaweza kukopa mshiko Fasta tena na tena huku bado ana deni ilimradi tu hajavuka kiwango cha kiasi anachostahili kukopa, ni nzuri pia hii. Kwenye kulipa madeni haya yanaainishwa yote kila moja na tarehe yake ya mwisho pia unaweza kulipa sehemu ya deni husika au ukalipa deni lote, hii pia nzuri sana. Lakini ukitaka kulipa yote kwa pamoja hakuna sehemu ya jumla ya madeni yote ili kurahisisha kulipa madeni yote kwa mara moja hii kidogo inaleta usumbufu tafadhali wekeni hicho kipengele
3. Kwenye mikopo hapohapo kuna kausumbufu kengine unakuta unalipa deni lakini ukiingia kwenye menu ya madeni bado deni lile lipo kwenye list. Hali hii inasumbua kidogo hasa pale ambapo una videni kadhaa na unataka kuvilipa vyote muda huo, hujui kipi ni kipi na kipi siyo na ndiyo maana nikasema kungewekwa option ya kuvikusanya videni vyote mtu alipe kwa pamoja
4. Salary advance kwa watumishi itolewe kwa mtindo huu mnaotoa mshiko fasta. Namaanisha wekeni utaratibu mtu kama salary advance yake ni laki 2 basi akiamua leo achukue elf 10 keshokutwa laki na wiki ijayo buku. Siyo hii ya sasa ambapo mtu ana shida ya 50 anavuta 100 eti kisa tu anahofia mbeleni asije kukwama na hana uwezo wa kuvuta kwa mara nyingine. Pia wekeni wazi mnakataje huu mkopo wa mshahara
5. La mwisho tena hili naomba hata wataalamu wa uchumi mtuambie hapa, ni kwanini kwenye mashine za atm tusiweze kutoa chenji za elfu kumi? Namaanisha kwanini mtu asiweze kutoa hizo elfu kumi zikiambatana na buku, elfu mbili na elfu tano? Majibu ya katoe kwa wakala siyataki!