Ushauri kwa Rais: Ili kukuza uchumi wa nchi na kupata fedha za ujenzi wa miundombinu, Mishahara ya watumishi wa umma na viongozi wa kisiasa ipunguzwe

Ushauri kwa Rais: Ili kukuza uchumi wa nchi na kupata fedha za ujenzi wa miundombinu, Mishahara ya watumishi wa umma na viongozi wa kisiasa ipunguzwe

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,858
Reaction score
5,101
Wapo watumishi wa Serikali pamoja na viongozi wa kisiasa wanalipwa mishahara mikubwa Sana.

Wapo wanaolipwa mpaka Laki nane, Tisa, milioni 2, 3, 4, 5, 10, 20 n.k kwa mwezi kiasi kwamba Hata ikikatwa na kuwa nusu yake bado kitakuwa Ni kiwango stahiki kitakachokidhi mahitaji Yao ya msingi na fedha zilizobaki zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
 
Tumechelewa Sana Ndugu Zangu
Nakukumbusha Mleta Mada Siku Nyingine Weka Number Yako Ya Simu Ya Mkononi Upate Teuzi Haraka. Vyeo Vipo Vingi
Nasema Uongo Ndugu Zangu
😁😂😀😅😏😃😃😀😁😂😂🤣😅😏😏😏
Ukivimbiwa Unasema Lolote
 
Naunga mkono hoja! Watumishi wote wapunguzwe mshahara kwa asilimia 25% ili hiyo 25% iende kwenye maendeleo.

Sisi wananchi hatuna shida sana na mshahara kwa kuwa mahitaji ya msingi ni chakula tu ambacho awamu hii kimeshuka sana bei.

Watanzania tujitolee kufunga mkanda ili nchi yetu ipate maendeleo kwa haraka kama Mh rais anavyotuasa.

Au nakosea wazalendo wenzangu? 😊
 
Wapo watumishi wa Serikali pamoja na viongozi wa kisiasa wanalipwa mishahara mikubwa Sana.

Wapo wanaolipwa mpaka Laki nane, Tisa, milioni 2, 3, 4, 5, 10, 20 n.k kwa mwezi kiasi kwamba Hata ikikatwa na kuwa nusu yake bado kitakuwa Ni kiwango stahiki kitakachokidhi mahitaji Yao ya msingi na fedha zilizobaki zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
sasa nisikilize mimi mchumi, watu wanaoongoza kwa kulipa kodi na kufanya manunuzi ni wafanyakazi wa serikali. Sasa ukipunguza mishahara utakua umepunguza vipato vyao. Hivyo moja kwa moja utakua umepunguza manunuzi. Ukipunguza manunuzi unapunguza soko la bidhaa ukipunguza soko la bidhaa wazalishaji wanapunguza uzalishaji wakipunguza uzalishaji GDP inashuka. GDP ikishuka uchumi unashuka. Uchumi ukishuka basi ni vyema wachumi wafanye economic analysis.

Kwa ushauri wangu watalaam wanasema utajiri unapatikana ardhini. Hivyo ili tuweze kuwa matajiri ni Bora tungejikita kwenye effective utilization of our resources. Kuna vitu viwili efficiency and equity. Wewe uliyo izungumzia ni equity ambapo unataka serikali ijikite kuwa na mgawanyo sawia wa mapato tuliyo nayo ili tuweze kupata fedha za kuendeshea nchi. Hivyo ilikupata mgawanyo huo mbinu mojawapo ndio hiyo ya kupunguza mishahara, ili pesa zitakazo punguzwa huko ziende kwenye miradi. Mimi nakuja hapa kwenye effeciency kwamba Mimi naiomba serikali badala ya kupunguza mishahara ni bora tutumie sera ya kutumia rasimali zetu kwa ufanisi ili kuziongezea thamani. Tuna gesi tuiongezee thamani ili ituletee fedha nyingi zaidi ndio ziende kwenye miradi. Tutafute mafuta na madini ya kila aina na tuyaongezee thamani ili tukiyauza yatuletee pesa nyingi ndo ziende kwenye miradi.
 
Wapo watumishi wa Serikali pamoja na viongozi wa kisiasa wanalipwa mishahara mikubwa Sana.

Wapo wanaolipwa mpaka Laki nane, Tisa, milioni 2, 3, 4, 5, 10, 20 n.k kwa mwezi kiasi kwamba Hata ikikatwa na kuwa nusu yake bado kitakuwa Ni kiwango stahiki kitakachokidhi mahitaji Yao ya msingi na fedha zilizobaki zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Sawa kabisa ila, na gharama za umeme zipunguzwe fro 350 per unit. Had sh. Hamsini tulipoanzia. Wakat wa Luku.
Kodi ya Mafuta ( petrol) iondolewe Mafuta Lita ya 350tsh Hadi Sh. 500.

Gharama za maji iwe 20 tsh per Lita.

Ukiagiza bidhaa Kama gari. Ule Ushuru, Vat, na gharama zote zifutwe Ibaki labda laki 2. Tu hivi unaondoa far yako bandarini inatia barabarani.

Gharama za kiwanja per square meter iondilewe kabisa , si Mali ya wananchi.

Etc etc.

Mbona inawezekana tu kupunguza mishahara na Maisha yakabaki kuwa poa.

Ni swala lakubalance hesabu tu.

Ila ukipunguza halafu gharama na tozo nyingine zibaki pale pale, Ni kuleta disaster kubwa.

Rushwa itarudi kubwa ambayo itazorotesha huduma na kuumiza wananchi wengine wanaopafata huduma kwenye ofisi/ huduma za Uma.

Unadhani Viongozi woote wapoahidi Maslahi Bora kwa watumishi wa Umma Ni Vilaza?
 
Wapo watumishi wa Serikali pamoja na viongozi wa kisiasa wanalipwa mishahara mikubwa Sana.

Wapo wanaolipwa mpaka Laki nane, Tisa, milioni 2, 3, 4, 5, 10, 20 n.k kwa mwezi kiasi kwamba Hata ikikatwa na kuwa nusu yake bado kitakuwa Ni kiwango stahiki kitakachokidhi mahitaji Yao ya msingi na fedha zilizobaki zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Nakubaliana nawe serikali kupunguza mishahara ya viongozi (wote wakisiasa na wasio wakisiasa) na watumishi wengine wanaopata nyingi 'husasani kwenye mataasisi'

Pia serikali ipunguze viwango 'rate' za posho (marupurupu)
 
Mkuu una roho mbaya Sana Yani mtumishi anaelipwa 2m bado akatwe,naona vyema KWA Sasa mtumishi anaetaka kustahafu apewe mafao yake ,mkaajili wengine ambao mtakua mnawakata mishahara Kama mpendavyo

Back
Top Bottom