Ushauri kwa Rais kuhusu mahindi yanayosafirishwa nje ya nchi

Nawapa tahadhari kuwa njaa inayokuja mbeleni kwa nchi ya Tanzania itakuwa ya kutisha. Jana nimeshuhudia kwa macho yangu katika mpaka wa Sirari mamia ya malori yakiwa na shehena ya mahindi yakipelekwa Kenya.

Huu ni mwezi wa sita bei ya gunia moja la mahindi ni zaidi ya Tshs.130,000 maeneo ya Mkoa wa Mara na sasa itakapofika Septemba hali kama hii itakuwaje.

Mhe. Rais mimi ni mtu mdogo ila nakushauri weka zuio chakula kisisafirishwe nje ya nchi mpaka hapo itakapoonekana hali ni nzuri.

Jana nchi ya kenya imeondoa ushuru wote wa mahindi na sasa wengi watamudu kununua kiasi chochote wananchohitaji na hivyo maelfu ya tani ya mahindi yatasombwa kwenda Kenya.

Mhe. Waziri wa Kilimo suala hili ni la muhimu sana unashauriwa kusimamia suala hili. Kwa hili nitamkumbuka sana Mhe. Magufuli sana.
Mtu yoyote anayetaka mipaka ifungwe ni mwenda wazimu. That's all I can say.
 
Kwa hiyo sisi tunaolima hatuna haki kupata Faida!? Tunapoenda shamba kuhenya nyie mnakimbilia press conference ya Manara.
Acheni mipaka ikae wazi kula urefu wa kamba yako.
 
Nawapa tahadhari kuwa njaa inayokuja mbeleni kwa nchi ya Tanzania itakuwa ya kutisha. Jana nimeshuhudia kwa macho yangu katika mpaka wa Sirari mamia ya malori yakiwa na shehena ya mahindi yakipelekwa Kenya.

Huu ni mwezi wa sita bei ya gunia moja la mahindi ni zaidi ya Tshs.130,000 maeneo ya Mkoa wa Mara na sasa itakapofika Septemba hali kama hii itakuwaje.

Mhe. Rais mimi ni mtu mdogo ila nakushauri weka zuio chakula kisisafirishwe nje ya nchi mpaka hapo itakapoonekana hali ni nzuri.

Jana nchi ya kenya imeondoa ushuru wote wa mahindi na sasa wengi watamudu kununua kiasi chochote wananchohitaji na hivyo maelfu ya tani ya mahindi yatasombwa kwenda Kenya.

Mhe. Waziri wa Kilimo suala hili ni la muhimu sana unashauriwa kusimamia suala hili. Kwa hili nitamkumbuka sana Mhe. Magufuli sana.
Kwanini usiitazame hiyo kama fursa na kuingia shambani kulima?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni wakulima nao wapate hela kwa walichozalisha mnataka yauzwe bei rahisi ili iweje na wao waondokane na umasikini wajenge nyumba bora.
 
Back
Top Bottom