Ushauri kwa Rais Samia: Nafasi za uteuzi wa Ma DED na wakuu wa taasisi amwachie Dkt. Mpango huku yeye akibaki na Ma DC, RC, Mabalozi nk

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Habari zenu Wana wa JF siasa.

Mama Samia Suluhu amemkabidhi VP Dr Mpango kusimamia Uchumi kwa kuwa ni mtaalamu wa nyanja hii.

Nashauri pia aachiwe ateue wakurugenzi watendaji wa halmashauri mbalimbali nchini. Pia ateue wakurugenzi wa mashirika mbalimbali ya umma Kama TRA, TPDC, TPA, TCRA, nk.

Rais Samia Suluhu abaki na uteuzi wa ma DC, RC, Mabalozi, RAS, DAS, nk.
 
Hapana lazima aangalli kama kilichofanyika ni sawa, at the end of the day lawana zitakuja kwake. Hiyo hapana. She has to ascertain what is proposed.. at any rate
Mpango apendekeze alafu Rais anaruhusu au kutoa ushauri
 
Mshaurini kwamba atoe kipaumbele kwa watu walio soma Economics, Planning 'corporate planning', Finance, Business Administration, na field nyingine zinazofana nana hizo.

Mifano:
NSSF, PSSF & WCF - shahada ya kwanza: BA in Economics, elimu ya uzamivu /& uzamili: Labour Economics

TPDC, PURA & EWURA - shahada ya kwanza: BA in Economics, elimu za uzamivu /& uzamili: Natural Resource & Environmental Economics

Hata mabalozi wenyewe - shahada ya kwanza: BA in Economics, elimu ya uzamivu /& uzamili: International Economics

Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Mikoa - shahada ya kwanza: BA in Economics, elimu ya uzamivu /& uzamili: Labour Economics/ au Public Finance
 
Katika uteuzi wa madc, ninaomba awaondoe madc walioko wilaya zifuatazo;- nyangwale, bukombe, Geita vijijini, Geita mjini, Kahama,nzega,igunga, dodoma jiji, kibaha, meru, siha, Rombo,same, Hai, simanjiro,kiteto, mbulu, serengeti,Tarime, mkoa wa Mwanza wote.chato na Ruangwa.
 
Weka sababu za kuondolewa kwao
 
Mkuu upo kitengo nyeti sana hao wote unawajua madhaifu yao!
Hongera
 
Mimi namshauri Rais Samia aweke full time surveillance kwa makamu wake na activity zake zote.

Huenda waliomshauri kumuweka Mpango kwa makusudi au bahati mbaya wameweka tatizo litakalojifunua taratibu as time goes on.
Na hizi post za aina hii huenda zikawa nyingi humu za kumtaka Mpango awe kama ndio kila kitu serikalini.

Mama nadhani umeingia chaka kwa huyu V.P
Be careful.
 
DC wa Kahama ana shida ipi? Mbona wana Kahama tunaona Anamringi Macha anatosha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…