Ushauri kwa Rais Samia: Nafasi za uteuzi wa Ma DED na wakuu wa taasisi amwachie Dkt. Mpango huku yeye akibaki na Ma DC, RC, Mabalozi nk

Napingaaa,
Mwacheni apange safu yake
 
Ni kosa Kwa mtu kutoka Chato au Ruangwa kushika nyadhifa nchini?
 
Wana kitu gani cha zaidi walichofanya hao waliosoma uchuchumi. Kusoma uchumi haimaanishi unawazidi ambao hawajasoma uchumi.
 
Naona Dr Mpango masikio yanazidi kichwa na unaonesha kihalisia tabia zako za kirundi. Nikushauri tu, watch out, Samia ndo Rais na unawajibika kwa Samia na wewe si lolote wala chochote bila Mhe. Raisi Samia.

Narudia tena watch out. Tutakuja kukukumbusha humu yakikupata. Ni rahisi sana Samia kupeleka hoja za wewe kujiuzuru nafasi zako zote kwa kutotii Mamlaka. Kumbuka hata Aboud Jumbe alikuwa Makamu wa Rais ila alivuliwa nafasi zake zote ikiwemo ya Makamu wa Rais.
 
Nashauri amkasimishe hayo mamlaka kwa Dr Mpango. VP ni jembe Sana, sidhani Kama Kuna DED ataleta ujingaujinga.
Inaonekana hufahamu kabisa mfumo unavyofanya kazi. Rais ana timu ya washauri ktk kila sekta na kuna jopo la timu inayosimamia uteuzi wa watendaji watakaoendana na style ya utawala wake kulingana na vipaumbele vyake.

Kazi yake akiletewa majina ni ya kuidhinisha tu ila akihitaji kufahamu kuhusu mteule yeyote yule anapewa maelekezo kwa nini amepewa nafasi. Kosa kama la DG wa TPDC inaonekana kuna watu walikuwa na agenda binafsi haikuwa intentional move ya mama kufanya marekebisho ya uongozi. Kuna watu nyuma wanafanya ujinga na asifanye kosa awafute kazi waliohusika na hiyo vetting.

Hata hivyo Philip Mpango unamkuza sana ila mtu average tu kichwani.
 
Hawezi kukubali tena baada ya matangopori ya TPDC mliyomlisha Jana.
 
Umeandika haya kwasababu Rais ni mwanamke???
 
Sio suala la aachiwe fulani, hii nchi ni yetu sote, waondoe ukada, ukanda watangulize maslahi ya nchi mbele. Wapo tunaowaamini wakae kama Jopo kufanya teuzi. Hili suala la kusema mwachie fulani hapana, mjinga mmoja anachomeka jina la mjinga wenzie madhara yake ndo kama unavyoyaona mambo ya aibu teua tengua in 12HRS.
 
Mbona watu wanataka kumpangia Amiri Jeshi Mkuu, majukumu yake??
Huyo Mpango asubirie shughuli zake za kuzindua Mwenge, kufanya ziara za kuzindua ujenzi wa maabara shule za kata huko Kasulu na Namabengo.

Kila mtu a range kazi yake.

Mpango abakie na hiyo ceremonial post, karidhika nayo. Asitake kujimwambafayi!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Big NOOOO
Kwanza hujui kila kitu kinafanywa kwa mujibu wa Katiba.

Pili unataka atujazie akina Sabaya wengine ? Hell noooo...
Rais ni mmoja tu.

Na wewe VP hacha mambo ya jiwe ya hotuba makanisani !
Am a Christian lkn hiyo tabia ni mbaya. Nyerere didn't so is Mwnyi, Ben na JK.
Kama kuna la maana sana ongea Ikulu.
Analeta unnecessary inconveniences ktk nyumba za ibada..
 
Mmh!
Sio sawa kikatiba na sio busara kumpora rais mamlaka yake ya uteuzi.

Kuna kitu nadhani mleta mada hukifahamu kuhusu mamlaka ya urais hapa Tanzania. Suala la kuteua na kutengua watendaji wa serikali halikuanzia leo wala jana. Kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli walitumia mamlaka hayo. Hivyo mama Samia aachwe.

Rais anaweza kushinikizwa kisiasa au kushauriwa kikatiba kumtengua yoyote na akafanya hivyo, lakini sio rahisi wala busara kumshinikiza au kumshauri amteue fulani kushika nafasi fulani na akafanya.
 
Hili ni suala la kisheria, mwenye mamlaka ya kuteua ni Raisi, wewe unaleta porojo za vijiweni hapa.
Kwamba ni suala la kuachiana kama mambo yao binafsi.
Hizi akili mnapewa zinafaa tu kuvukia barabara na sio kufikiria.
 

Yeye kama rais na muwajibikaji mkuu lazima ashiriki
 
Huu utaratibu mbaya wa kuteua na kutumbua kila mtendaji wa serikali hadharani umekuzwa mnoo na Magufuli. Hauna mantiki kabisa.

Kwa mfano, hapo kabla wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa wilaya, makatibu tawala wa wilaya (DAS), Makatibu kata nk walikuwa wanasimamiwa moja kwa moja na waziri mkuu, Rais alikuwa na mamlaka ya kuteua na kutengua lakini mapendekezo yalikuwa yanatokea ofisi ya waziri mkuu. Kwanini? Waziri mkuu ndio mtendaji mkuu wa serikali wa kila siku, hao watu ndio timu yake ya watendaji. Anawajua vyema.
 
Mamlaka ya uteuzi ni moja tu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Serikali siyo ghetto la masela kila mtu ana mamlaka ya kufanya anavyopenda.
Kabisa Serikali siyo ghetto la masela. Eti mnaachiana tu, kama kawa!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…