Ushauri kwa RC Makala juu ya wamachinga Dar es Salaam

Ushauri kwa RC Makala juu ya wamachinga Dar es Salaam

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
Nimeona taarifa kwamba unataka uwapange wamachinga. Ni kitu kizuri Sana na kinatakiwa kiungwe mkono na kila mtu.

Ushauri wangu; Usitumie maneno ya mitandao kufanya Jambo hili. Tumia mda wako wote kutafuta ushauri wa wamachinga kwanza. Huku kwenye mitandao utapotoshwa.

Kuna watu Wana hasira na wamachinga kisa tu wako mbele ya maduka yao na wengine wanachonganishi zidi ya wamachinga na serikali ya CCM. Wengine ni chuki zidi ya machinga wa Hayati JPM.

Faida za hao machinga ni nyingi mno. Na hapa nataja chache.

1. Serikali iendelee kutafuta njia rahisi ya kukusanya kodi kutoka kwao.

2. Hawa wanasogeza huduma karibu na mtumiaji na hivyo kufanya mzunguko wa biashara kuwa mkubwa.

3. Hawa wanapunguza vibaka mtaani. Pigia msitari hili kisha fanya uchunguzi. Asilimia kubwa ya Hawa watu Wana kipato kidogo, wako tayari kuiba ama kufa wakitafuta kipato. Jua lao mvua yao. Bila hii Kazi Hawa Ndio mateja na vibaka mtaani.

4. Wanaondoa misongo ya mawazo na huzuni kwenye maisha yao.

Chonde chonde usikurupuke. Utatujazia vibaka mtaani.
 
Machinga ni lazima wapangwe kwa utaratibu, serikali haiwezi kuogopa vitisho vya kuwa wakiondolewa wataiba.

Wakiiba watakutana na polisi, mahakama na magereza.

Mnaziba maduka ya walipa kodi, mnafunga njia za waenda kwa miguu, mnaziba vituo vya basi, mnafunga service road, mnachafua mji nk.

Wamachinga tunawahitaji maana ni vijana wetu lakini lazima kuwe na utaratibu mzuri.
 
Utaratibu gani wa kodi kwa mtu ambae leo yupo kesho hayupo?.

wapewe vizimba rasmi watambulike walipe kodi
 
Ukweli lazima usemwe, definition ya machinga irejewe upya! Kuna wanaojiita wamachinga lakini ni mawakala wa maduka makubwa. Wanapewa bidhaa toka dukani na wanasambaa mitaani na jioni wanarudixha hesabu kwa Boss! Bidhaa kubwa kubwa zinauzwa bila risiti ya EFD, hapo serikali itakuwa imepigwa kodi ya VAT! Na hawa wapk kwa maelfu na serikali hupoteza pesa kwa mamilioni kila siku. Hao nao ni wamachinga! wizi mtupu!
 
Machinga ni lazima wapangwe kwa utaratibu, serikali haiwezi kuogopa vitisho vya kuwa wakiondolewa wataiba.
Wakiiba watakutana na polisi, mahakama na magereza.
Mnaziba maduka ya walipa kodi, mnafunga njia za waenda kwa miguu, mnaziba vituo vya basi, mnafunga service road, mnachafua mji nk.
Wamachinga tunawahitaji maana ni vijana wetu lakini lazima kuwe na utaratibu mzuri.
Serikali imekuwa nyepesi sana. Hawa jamaa wanaweka vurugu tu kwenye mitaa. Huku Zenji tumewatimua Darajani na kisiwandui, wamepelekwa kibanda maiti. Yaani wanapanga vitu kwenye njia pakupita hamna. Walitaka kuleta ubishi wakajipeleka makao makuu ya CCM, walikula mabomu ya machozi saivi wapo kibanda maiti. Kazi kuharibu miji tu
 
Ukweli lazima usemwe, definition ya machinga irejewe upya! Kuna wanaojiita wamachinga lakini ni mawakala wa maduka makubwa. Wanapewa bidhaa toka dukani na wanasambaa mitaani na jioni wanarudixha hesabu kwa Boss! Bidhaa kubwa kubwa zinauzwa bila risiti ya EFD, hapo serikali itakuwa imepigwa kodi ya VAT! Na hawa wapk kwa maelfu na serikali hupoteza pesa kwa mamilioni kila siku. Hao nao ni wamachinga! wizi mtupu!
Yapo mabanda njiani wanauza vinywaji baridi na vikali,bidhaa zilizopo mwenye Grocery akasome
 
Muhimu ni mama samia ajiandae tu kua na upinzani na Hawa watu ambao ni wengi na wavuja jasho haswaaaa ktk utafutaji,Hawa si wale wa kupitisha fedha mabilioni kwa ajili ya kazi maalumu au vikao vya board vyenye maposho ya 600million na kubadili mradi wa 100million.

Ajipe muda mama ajiridhishe maana mbwembwe Zina mwisho wake
 
Suluhisho la machinga ni suala mtambuka (cross cutting), ambalo linahusisha Mamlaka za Jiji/ Manispaa, TRA, Polisi na Wizara ya Ardhi na Makazi na Wizara ya Biashara na Viwanda.

Kamwe Amos Makalla hawezi akakitatua peke yake kwa akili yake ya kutaka sifa. Nimemuona alivyo APRROACH suala la Ombaomba kwa mtindo huo huo.

Namshauri aombe kupitia ofisi ya Waziri Mkuu apate timu kutoka maeneo hayo niliyoyataja ndipo tutalitatua kwa amani suala la machinga kurundikana barabarani hadi CITY CENTRE.

Ila pamoja na yote Machinga lazima lazimawaondoke katikati ya Jiji, ni UCHAFU.
 
Back
Top Bottom