Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Mheshimiwa rais, natumaini unaendelea vema na majukumu yako ya kuongoza serikali.
Niende moja kwa moja kwenye ushauri wangu.
Tengeneza sera ya kubadili mfumo wa manunuzi nchini kuondoka kutoka kwenye matumizi ya cash na kuwa wa kieletroniki.
Na jambo hili lisifanyike kwa kutunga sheria ya kulazimisha watu wahamie, bali ziwekwe matisha za kuwashawishi walaji / wanunuzi kutumia zaidi mifumo ya kielectroniki.
Mfano;
Baada ya miaka miwili mitatu nakuhakikishia mambo ya cash yatakuwa ni historia.
Ni kweli serikali itapoteza mapato kidogo kwa miaka michache lakini faida yake ni kubwa zaidi.
Ni vigumu sana kukwepa kodi na kudanganya mahesabu pale miamala inapofanyika kwa njia za kielectroniki tofauti na cash.
Hakutakuwa na haja ya TRA kwenda na polisi kukagua kama mfanyabiashara anatoa risiti au la, as long as anatumia account ya benk au mobile money kupokea malipo kutoka kwa wateja basi anaweza kukaguliwa 'remotely' bila mabavu.
Sijui ni nani alikupa ushauri wa kuweka tozo kwenye miamala lakini kaa ujue kuwa uwezo wa mtu huyo wa kufikiri na kupanga mipango ya muda mrefu sio mzuri. Huyo mtu ni mzigo ambao unapaswa kuutua.
Ni hayo tu, cashless market = easy tax collection.

- Futa tozo zote kwenye miamala ya simu na mobile banking.
- Ongea na mitandao ya simu na mabenki ili huduma ya kufanya malipo kwa kutumia kadi ya benki na mobile money ziwe bure kabisa.
- Weka tax refund (kwa mfano 2% ya total VAT) kwa mwaka kwa wateja wote waliofanya malipo kwa njia ya kieletronic.