SoC04 Ushauri kwa Serikali, Wazazi, vijana kuhusu kupunguza tatizo la ajira

SoC04 Ushauri kwa Serikali, Wazazi, vijana kuhusu kupunguza tatizo la ajira

Tanzania Tuitakayo competition threads

Hofajr16

New Member
Joined
Sep 3, 2022
Posts
1
Reaction score
3
Suala la ukosefu wa ajira hapa nchini Tanzania limekuwa sio stori tena ni suala ambalo linaonekana ni kama changamoto sana kutokana na sababu mbalimbali, lakini andiko langu nitagusia sana katika ujifunzaji wa lugha za kigeni hususani lugha ya kichina katika kupanua soko la ajira kwa vijana.

Lugha ya Kichina ni lugha ambayo inashika hatamu sana kwa sasa ulimwenguni hii ni kutokana na makampuni mbalimbali ya wachina kuwekeza maeneo mbalimbali duniani na wao wachina kutamani lugha yao ienee kwa kasi zaidi ndiyo maana wanachukua jitihada zote za kutoa ufadhili kwa wageni wa nchi mbalimbali ili kujifunza lugha yao lengo kubwa ni kueneza lugha katika nchi mbalimbali kama ilivyo lugha ya Kifaransa pamoja na kiingereza,sote tunafahamu kwamba lugha ya kiingereza ni lugha ambayo ndiyo imesambaa duniani kote na karibu kila taifa linafahamu kuzungumza lugha hii ya kiingereza na sasa imeonekana ni lugha ya kawaida sana kwa watumiaji ulimwenguni kwani karibu kila mtu anaifahamu hivyo kupunguza fursa za ukalimani kupitia lugha hii.

Lugha ya kichina ni lugha inayoenea kwa kasi sana ulimwenguni siku hizi kwani makampuni mengi ya wachina yamewekeza nchi mbalimbali hii imepelekea kuwa na mahitaji makubwa sana ya ukalimani kwa kuwa kazi hizo haziwezi kuendeshwa bila wakalimani,ukizingatia vijana wengi sana wamejikita kusoma kozi mbalimbali ambazo ushindani wa soko la ajira ni mkubwa sana hivyo kupelekea ongezeko la wahitimu wengi kubaki mitaani na kuanza kufanya shughuli mbalimbali ambazo hawajazisomea mfano kuendesha bodaboda, kufanya vibarua mbalimbali ili kujipatia kipato kidogo cha kusogeza siku mbele na wengine kujiingiza katika makundi ya wizi wakati huo lugha hii ya kichina kwa sasa imekuwa ni lugha ambayo haina ushindani mkubwa katika soko la ajira hapa nchini kwani mahitaji ya wakalimani na wafasiri yamekuwa mengi sana kwa kuwa makampuni ya wachina yameongezeka hapa nchini hivyo kupitia vijana hawa kuitambua fursa hii itawawezesha wao kuwa tofauti na wale waliosomea kozi nyingine kwani tatizo si elimu kubwa kwani unaweza ukawa na elimu kubwa lakini bado ukabaki hauna pesa na maisha ya sasa yanahitaji mifumo sahihi yenye ujanja katika kupata pesa.

USHAURI KWA WAZAZI
- Wazazi wa kitanzania watambue kwamba maisha yamebadilika sana tofauti na zamani ambapo mtu ukisoma sana hukai mtaani na kusubiri kazi yaani ukishamaliza tu ajira moja kwa moja lakini hali halisi ya sasa hapa nchini Tanzania haipo hivyo tena. Wazazi watambue kwamba mtoto kujua kiingereza sana hakutamsaidia kupata ajira kwani wengi wanaifahamu hii lugha na bado wapo mtaani wakingoja ajira miaka nenda rudi na sio kwamba naikataa lugha ya kiingereza bali najaribu kuonyesha ni namna gani ushindani wa ajira ulivyo, hivyo nitoe ushauri kwa wazazi kuwa na muono wa mbali zaidi kuwapeleka watoto wao katika kozi fupi za lugha ya kichina na kuwasisitiza wasome kwa bidii kwani lugha hii ajira zake zipo nje nje sana tena ni rahisi kama mtu amesoma! kusoma sana ni vizuri lakini wazazi waondoe kasumba ya kuwataka watoto wasome kozi walizozoea kuzisikia bali wawahimize kusoma lugha hii na wawatie moyo kwani hakuna mwanzo uliokuwa rahisi bali kila jambo linaenda kwa hatua.

USHAURI KWA VIJANA
- Vijana waliopo mashuleni, vyuoni (kama somo linafundishwa) ni vyema wakajiunga katika madarasa yanayofundisha lugha ya kichina ili kuweza kujifunza kwani wengi wao hujisingizia eti kuwa wana kozi au masomo mengi hivyo wakichukua na somo la kichina wanahisi kuwa watafeli mitihani jambo ambalo si la kweli kwani ukiweka ratiba yako huwezi ukafeli kama inavyodhaniwa na wengi kwani hata mimi nilianza kusoma kozi hii nikiwa chuo kikuu mwaka wa mwisho lakini nikaweza kufanikiwa kumaliza masomo yangu yote bila kufeli na baada ya hapo kuingia kufanya kazi katika makampuni ya wachina.

Pia niwashauri vijana waliohitimu vyuo au shule kujiunga na kozi fupi za lugha hii ambapo kozi hii inatolewa vituo mbalimbali mfano Chuo kikuu cha Dar es Salaam katika taasisi ya Confucius kama mtu akifanya jitihada vizuri ndani ya mwaka anakuwa mahiri wa lugha hii itamsaidia kupata kazi katika makampuni kwa wachina au shule ambapo serikali imeliingiza somo hili mashuleni kwa minajili kufundishwa.

Wasikate tamaa na kusema wamechelewa hapana! Muda bado upo wanaweza wakafanya jambo na vijana wakipata kazi basi tunategemea kupata taifa imara sana kwa vizazi vijavyo kwani vijana ni nguvu ya mabadiliko katika taifa lolote lile, mimi mwenyewe namshukuru Mungu sana kwa kuniongoza kusoma somo hili kwani nimeshaanza kula matunda ya zile jitihada nilizozifanya japo nilibezwa sana na marafiki zangu nilipoanza kusoma lakininleo nimekuwa mwanga kwa wengi wakinifafuta na kuomba mwanga wa wao kuanza kujifunza.

USHAURI KWA SERIKALI
Kwanza niipongeze Serikali kupitia wizara ya elimu kwa kurasimisha somo la kichina kufundishwa mashuleni, sasa ni muda sahihi wa kushirikiana bega kwa bega na wadau wa lugha ya kichina ili kuona uwezekano wa kupata walimu wengi na kuongeza vituo kwa wale walio nje ya mfumo wa taasisi za elimu kuweza kujifunza lugha hii kwani serikali inaweza ikatoa ufadhili wa masomo kwa vijana waende nchini china kujifunza lugha kwa kuwa wataalamu wa lugha bado ni wachache. Hii itafungua milango ya vijana kufanya kazi katika nchi nyinginezo ambapo makampuni mengi yamefunguliwa lakini hakuna wakalimani wa kutosha wa lugha, hii hivyo hii itaongeza fursa za ajira kwa vijana hapa nchini na kukuza uchumi wa nchi.
 
Upvote 5
Wazo Zuri ila watanzania tuelewe hakuna ajura nzuri kama kujiajiri Tanzania bado tuna aridhi nzuri, uvuvi, misitu mingi, mito,bahari na madini
 
hivyo nitoe ushauri kwa wazazi kuwa na muono wa mbali zaidi kuwapeleka watoto wao katika kozi fupi za lugha ya kichina na kuwasisitiza wasome kwa bidii kwani lugha hii ajira zake zipo nje nje sana tena ni rahisi kama mtu amesoma
Anhaa, kwa hivyo ni lugha ya kichina tu tatizo la ajira litaisha!??? Kichina tu mmmmh!


hujisingizia eti kuwa wana kozi au masomo mengi hivyo wakichukua na somo la kichina wanahisi kuwa watafeli mitihani jambo ambalo si la kweli kwani ukiweka ratiba yako huwezi ukafeli kama inavyodhaniwa na wengi
Wengi ni uzembe ndio maana wanatamani kujifungia kwenye ubize. Labda hadi wewe umeweza ni huko kujituma kujiongeza. Namna unafanya jambo moja ndivyo unafanya mambo yote nafikiri.

Pia niwashauri vijana waliohitimu vyuo au shule kujiunga na kozi fupi za lugha hii ambapo kozi hii inatolewa vituo mbalimbali mfano Chuo kikuu cha Dar es Salaam katika taasisi ya Confucius
Ahsante kwa ushauri mzuri ulioushi mwenyewe na ukayaona matunda, walking the talk.
 
Back
Top Bottom