Ushauri kwa Spika: ili kulinda hadhi ya Bunge, kwamba si sehemu ya mzaha, Mbunge aliyepiga sarakasi apelekwe kamati ya Maadili, aombe radhi nchi

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Bunge ni mahala pa kuwasilisha mawazo ya Taifa. Ni mahala ambapo nchi inatarajia mijadala mizito ya mambo mbalimbali ya taifa.

Ni jambo la kutia hasira na aibu, mbunge anafanya mzaha wa sarakasi mbele ya vyombo vya habari, live, tena wakati huu mgumu wananchi wanapambana na hali ngumu.

Huyu mtu anayelipwa milioni zaidi ya 12 anaenda kufanya kituko cha ajabu, hivi wananchi wataelewaje?

Nashauri Bunge limuite kamati ya Maadili, CCM pia wamwite, sharti moja tu, aombe radhi mbele ya Bunge na wananchi wa Tanzania.
 
Bunge ni mahala pa kuwasilisha mawazo ya taifa. Ni mahala ambapo nchi inatafajia mijadala mizito ya mambo mbalimbali ya taifa.

Ni jambo la kutia hasira na aibu, mbunge anafanya mzaha wa sarakasi mbele ya vyombo vya habari, live, tena wakati huu mgumu wananchi wanapambana na hali ngumu.

Huyu mtu anayelipwa milioni zaidi ya 12 anaenda kufanya kituko Cha ajabu, hivi wananchi wataelewaje?

Nashauri Bunge limuite kamati ya Maadili, CCM pia wamwite, sharti moja tu, aombe radhi mbele ya Bunge na wananchi wa Tanzania
Mkajenge barabara kule alikosema mbunge achana na mambo ya kuitwa kamati ya maadili
 
Yaani mtu WA kupeleka Milembe/Mirembe hospital tangia lini akawa WA kupeleka kwenye Kamati ya maadili!? Huyu Mtu alishapewa Ambulance akafanya hivyo hivyo, hayuko sawa
 
..ishambulieni Serikali iliyoshindwa kutimiza ahadi ya kujenga barabara ya lami Mbulu vijijini kwa miaka 20 sasa.

..msimshambulie mbunge kwa kueleza ukweli na kuonyesha hisia zake kutokana na ulaghai wa CCM na Serikali.
 
Wamebaki wabunge wa kupiga mbao tu,hutosikia miswada yenye tija,hutosikia hoja za maana za kuiwajibisha Serikali, sana sana viroja, makofi na vijembe!!
 
..amejenga hoja.

..na ameruka sarakasi.
Tunasubiri kanuni za CCM na Bunge zimuandame kama nyuki waliowekwa kwenye kiroba, wakamwagiwa pilipili kichaa, wakatikiswa halafu wakaachiwa ukumbini
 
..msiwazibe midomo wawakilishi wa wananchi.

..nyinyi mnaopanda ma-V8 mara nyingi hamuelewi shida za wananchi.

..inakera serikali kutoa ahadi ya barabara ya lami kwa miaka 20 bila kuitekeleza.
 
Lakini mkuu JokaKuu, enzi za Jiwe angethubutu kuruka sarakasi bungeni? Ni kama dharau hii.

..sijaona jambo la dharau hapo.

..kila mbunge yuko pale kutetea wananchi anaowawakilisha.

..na wabunge hutumia mbinu mbalimbali kukoleza hoja zao.

..wako wabunge wenye vipaji vya kuimba huamua kuimba kusisitiza hoja zao.

..huyu mbunge huenda kipaji chake ni sarakasi hivyo aachwe atumie kipaji chake kuipa msisitizo hoja yake.

..wabunge wasizongwe. Waachwe wachangie kwa uhuru.

NB:

..kipindi cha Jpm ilikuwa ni wakati wa kusifia serikali.

..Mbunge wa Ccm asingeweza kuchangia kama alivyofanya Mh.Massay.
 
Huyu ndo jimboni kwake mawe yanarushwa kutoka kusikojulikana?
 
..kilichosababisha mbunge akachukia na kuamua kupiga sarakasi ni ulaghai wa Ccm na uzembe wa serikali ktk kushughulikia kero na matatizo ya wananchi wa jimbo la Mbulu.
Ni kweli kabisa kuhusu hiyo chuki ya Mbunge. Lakini sheria za Bunge haziruhusu sarakasi kuchezwa humo ndani. Huyu Mheshimiwa anastahiki adhabu kwa kadri ya sheria hiyo inavyotaka.
 
Bunge ni mahala pa kuwasilisha mawazo ya taifa. Ni mahala ambapo nchi inatafajia mijadala mizito ya mambo mbalimbali ya taifa.

Ni jambo la kutia hasira na aibu, mbunge anafanya mzaha wa sarakasi mbele ya vyombo vya habari, live, tena wakati huu mgumu wananchi wanapambana na hali ngumu.

Huyu mtu anayelipwa milioni zaidi ya 12 anaenda kufanya kituko Cha ajabu, hivi wananchi wataelewaje?

Nashauri Bunge limuite kamati ya Maadili, CCM pia wamwite, sharti moja tu, aombe radhi mbele ya Bunge na wananchi wa Tanzania
Hizi akili za wapi?.
Watu kama ninyi hamna maana.
 
Kwani kavunja sheria gani ,mbona yupo sawa tu,hapo kapeleka meseji kwa serikari itumize ahadi yake ya kujenga barabara kitu ambacho ni kizuri .Anadai maendeleo tumpongéze na kumtoa moyo.
 
Back
Top Bottom