Ushauri kwa Spika: ili kulinda hadhi ya Bunge, kwamba si sehemu ya mzaha, Mbunge aliyepiga sarakasi apelekwe kamati ya Maadili, aombe radhi nchi

Ushauri kwa Spika: ili kulinda hadhi ya Bunge, kwamba si sehemu ya mzaha, Mbunge aliyepiga sarakasi apelekwe kamati ya Maadili, aombe radhi nchi

Sorry mtu akichukia anapiga sarakasi? This is new
But hata hivyo hiyo sarakas imemsaidia nn?

..kila mtu ana namna tofauti ya kuonyesha furaha, hasira, au huzuni.

..bado ni mapema kuamua kama hotuba iliyofuatiwa na sarakasi ya mbunge imefikisha ujumbe serikalini.

..ktk BAJETI inayokuja, serikali isipotenga fedha za kutosha na kuteya mkandarasi kujenga barabara ya lami ktk jimbo la Mbul, then tutajuwa na haki ya kuhukumu kwamba mbunge amejaribu njia zote, mpaka kupiga sarakasi, lakini serikali haikumsikiliza.
 
Bunge ni mahala pa kuwasilisha mawazo ya Taifa. Ni mahala ambapo nchi inatarajia mijadala mizito ya mambo mbalimbali ya taifa.

Ni jambo la kutia hasira na aibu, mbunge anafanya mzaha wa sarakasi mbele ya vyombo vya habari, live, tena wakati huu mgumu wananchi wanapambana na hali ngumu.

Huyu mtu anayelipwa milioni zaidi ya 12 anaenda kufanya kituko cha ajabu, hivi wananchi wataelewaje?

Nashauri Bunge limuite kamati ya Maadili, CCM pia wamwite, sharti moja tu, aombe radhi mbele ya Bunge na wananchi wa Tanzania.
ANGEKUWA WA UPINZANI ILA SIO WALE COVID 19 SIKU ILE ILE ANGEJIKUTA KWENYE HIYO KAMATI NA KUFUNGIWA VIKAO 10

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom