guojr
Member
- Dec 4, 2015
- 62
- 95
Habari za muda huu wana jukwaa.
Leo nimekuja na ushauri kwa TCRA na jeshi la Polisi kutokana na uhalifu wa mtandaoni.
Uhalifu wenyewe ni huu unaohusu kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno wa kitapeli. Katika utafiti wangu mdogo, nimegundua mambo kadhaa.
Mosi, namba zinazotumika kufanya utapeli ni za mtandao wa TTCL.
Pili, jumbe za kitapeli zinazotumwa kwa watu zina "keywords" zinazofanana.
Tatu, Wanaofanga huo utapeli unapowapigia hujibu kwa kujiamini kana kwamba serekali haifanyi jitihada zozote kupambana na uhalifu huu.
Nne, hakuna mrejesho wowote unapoiripoti namba husika kupitia 15040 zaidi ya "Ujumbe wako umepokelewa na utashughulikiwa haraka iwezekanavyo. Asante".
USHAURI WANGU
1. Ufanyike uchunguzi wa kina kubaini kwanini matapeli hutumia zaidi namba za TTCL. Je, TTCL inasajili line kiholela au kuna "loop hole" gani inayotumika kufanikisha uhalifu huu.
2. TCRA wafanye "blacklist" ya "keywords" zinazotumika kwenye uhalifu huu ili zile "sms" zisiwafikie watumiaji ambao hawana hatia. TCRA na jeshi la Polisi wanaweza kuzidaka hizo "sms" kutoka kwenye "blacklist repository" na kuendelea kuzifanyiakazi kuliko kutubebesha mzigo sisi watumiaji eti tuziripoti kupitia 15040.
3. Jeshi la Polisi liwe makini na kuongeza nguvu katima mapambano dhidi ya uhalifu huu, kwani wananchi tunarudishwa nyuma.
Naomba sasa niwasilishe hoja.