Ushauri Kwa Urusi : Huwezi kuwaangamiza mchwa bila kumuua Malikia wao, Mwenzako Japan alilijua hilo na akajaribu Bahati yake

Well said, umeongea kwa busara ukiweka ushabik pembeni. Ongera kwa hili chief.

Hapo unaposema kuwa ishu ya ukraine imetia doa uwezo wao kiasi flani naomba urekebishe kidooogo, sema kuwa kwa sehemu kubwa imetia doa. Kwanini?

1. Russia kupitia putin amekiri kupoteza Askar 1,300. Sasa kikawaida utaweza kujua tu kuwa hiyo namba sio rahisi kuwa sahihi, itakuwa ni kubwa tu. Na hapa sio russia pekee, hata ukraine lazima afiche namba.

2. Russia alizama Ukraine ndege zao zikianza kupepea sana, ikafika wakati Ukraine akaomba msaada wa anga. Mida huohuo pia alikuwa anaingiza gari nyingi na vifaru vingi ktk uwanja wa mapambano. Leo hii naandika hii post, Russia hana teeena vifaru vyovyote ndani ya Ukraine, mpaka magari yamepigwa yoote.

3. Russia anatumia long range missiles, hii ni kutokana na ndege na vifaru vyake kukwama Ukraine. Kwa taifa lenye teknolojia, sikutegemea kuona hivi. Sasa mimi najiuliza, kama Ukraine tu ameweza kumzuia jamaa hivi, vipi kuhusu Ufaransa na UK? Angeingia Israel je?

- Mwisho kabisa Russia ametupa wasiwasi mno kuhusiana na uimara wa vifaa vyake, tunaanza mtilia mashaka kama china. Ndo maana bidhaa za Ulaya na US ni imara mno, popote pale hawa jamaa wana products jiwe kulinganisha na mataifa mengine. Napata wasiwasi kuhusu zana za Russia. Ninaamini hata Putin mwenyewe anatamani kusuka hili jeshi upya tena.
 
Kwa kumalizia mkuu, US sasa hivi anatengeneza lasee weapons, hatari sana. Hakuna silaha yoyote inaweza ikainuka juu yao, hata hizo hypersonic missiles hazifui dafu apo.
 
Pia na wewe acha kuichukulia poa Ukraine. Alafu wanaopigana pale Ukraine sio Ukraine peke yake.

Mnajifanya kuwaita mercenaries kumbe ni majeshi ya West huko..
Vita vilivyoanza zile siku za mwanzoni, Sukhoi za Ukraine zilikuwa haziruki, Russia alizihack systems zake. Akajua kama ameikomesha Ukraine, mzungu akaleta Javeline, hatari saana.
 
Ni kweli, lkn jamaa asiseme et Russia is weak. Kule Venezuela US kasanda. Na Putin aliwah kunujuliwa akisema "angelikua rais wakati wa Gaddafi, angelikua hai mpaka sasa"
siasa kutafuta sifa tu , alishindwa kumlinda Sadam
 
Ni ukweli kwa muono wa sisi tulio wengi tunaona Russia kama hakufanya vzr lakini yapo ya kujiuliza.
1. Ni ukweli usio shaka kwa ushahidi wa viongozi wa NATO kuwa walipeleka silaha kabla ya vita kuanza. Hivyo Russia alikuwa anapigana na NATO iliyojificha tangu mwanzo.

2. Ni ni kweli kuwa infantry soilders wa urusi hawakuwa vzr maana askari waliovaa kiraia wa Ukraine walipigana kiume kwa cover ya civilian uniform.

3. Kama alihitaji ushindi wa haraka hakutakiwa kujibu PROPOGANDA na Media. Kuua raia , kelele hizo za kutaka kuwa mwema zimemgharimu angepiga yeyote kwa nguvu na kwa upesi bila kujali humantarian corridors hii ilikuwa inafanya wanajipanga, kumbuka mashambulizi ya mwanzo yalifanikiwa sana.

Alifanya ujinga wa msafara mrefu wa magari ambayo ni rahisi kuwa targeted na kuleta madhara kwa haraka..

Ieleweke kuwa ikiwa ni points hadi sasa Russia amemzidi nguvu Ukraine pamoja na misaada ya NATO lkn miji yao inaharibiwa mno kwahiyo wanaosema anashinda sio kweli. UNHR inalipoti wakimbizi wa Ukraine ambao miji yao imefanywa magofu.
Wakati nchi za NATO wanaingiza kila mmoja silaha yake kujaribu ni tofauti na aliye front, wao wanaleta silaha hawana cha kupoteza.

Media Propaganda za magharibi na washirika hazisemi sahihi. Zinaonesha Russia akizidiwa na zqna zake kuharibiwa lkn hazioneshi kuharibiwa zana za Ukraine na wenzake. Je hawakuwa na vifaru wala ndege?

Kuhusu uwezo wake Russia vs NATO hili tuliweke kapuni, kwani hata Russia hajatumia silaha zake zingine wakiparagisha ndio tutajua kumbe huyu ana nini cha ziada . Ikumbukwe hakuna atakaye tumia Nuke kwa sasa maana akirusha mmoja na wengine wanarusha.

Kama angeniomba ushauri mimi ningemwambia usiende vitani na silaha zote hizo peleka mamuluki 100 well trained wamuondoe rais uje uchaguzi mwingine
 
Pia na wewe acha kuichukulia poa Ukraine. Alafu wanaopigana pale Ukraine sio Ukraine peke yake.

Mnajifanya kuwaita mercenaries kumbe ni majeshi ya West huko..
Mara ngapi Russia awaambie anachofanya ni operation?

Targets za Russia ni mbili: Kupunguza nguvu za kijeshi na kuwaondoa Nazi. Askari wa Ukraine na Nazi ni wanafahamu nguvu ya Russia ipoje! Kupambana nao moja kwa moja ni hatari. Wanachofanya wanajificha kwenye makazi ya raia na kuwaweka raia mateka na kuwafanya kama ngao.

Hapo atakachofanya ni vita au operation ya kuwaokoa raia ili kuepusha maafa mengi kwa raia kwa sababu athari za hapa na pale zitatokea. Ingelikuwa vita Russia angeangusha makombora kwa saa 48 mfululizo kwa majiji yote ya Ukraine lakini hili hulioni likitokea kwa sababu anachofanya ni operation.

Na ndiyo maana mbinu anazozitumia anauzungira mji na kukata miundombinu yote muhimu ambayo itakayowawezesha jeshi la Ukraine wakiwemo Nazi kukosa vichocheo vitakavyowawezesha waendelee kuishi.

Wanazuia kuingia kwa vyakula, wanakata umeme, mawasiliano yote, wanalipua hifadhi za mafuta hivyo magari ya jeshi la Ukraine halitakuwa na mafuta ya kuendesha mitambo yao. Silaha ukitumia zinaisha! Hivyo wanaziba miundombinu yote ya adui kupata silaha.

Wanalipua kambi za jeshi, viwanda vya kutengenezea silaha, ghala za kuhifadhia silaha n.k na kuhakikisha wanadhibiti anga. Mapigano yanayobaki ni ya ndani kwa ndani kwenye makazi ya raia unafikiri utatumia nguvu kubwa? Au utatumia makombora yenye nguvu kubwa?

Hapana! Bali hapa utafanya operation ya kuukomboa mji na raia wake na kwa namna hii operation itachukua muda ila mafanikio ni ya uhakika na ndiyo maana sehemu nyengine jeshi la Ukraine linajisalimisha kwa sababu ukizingirwa namna hii unakuwa hauna msaada wa aina yoyote.

Phase ya kwanza ilikuwa ni kulipunguza nguvu jeshi na ndiyo maana miji mingi ilikuwa akipiga anasonga mbele zaidi kuua miundombinu ya jeshi ili kulifanya liwe halifanyi kazi na hili msimaji wa Zelensky ameshaliweka wazi kuwa jeshi la Ukraine kwa asilimia kubwa sana ni toothless kwa sasa.

Phase ya 2 ni kukomboa majimbo yanayoongea Kirusi. Anachokifanya Russia kwa sasa kupitia hii operation anaenda kuigawa Ukraine na kuwa nchi mbili. Ukraine ya mashariki na Ukraine ya magharibi. Ila mbinu zinazotumiwa na jeshi la Ukraine ni hizo hizo wanaweka raia mateka na kuwafanya ngao.
 
Walianza kuondoka hata kabla ya makubaliano yoyote kufikiwa.
 
Ulielewa nin Russia aliposema anaivamia Ukraine ( Full scale millitary invasion) ? Wakat anashambulia miji inayopakana na yeye , msururu mkubwa wa magar ya kivita ukawa unaelekea Kiyv , lengo la kwenda Kiyv ni nini? Now anapakimbia Kiyv ni nini kimemtokea ?

Option ya kuyachukua majimbo yanayopakana nae imekuja baada ya lengo la Kwanza kufail ,
 
Umeiandika kipropaganda sana Rusia kuiita hii ni operation alimaanisha vitu vingi sana Kwanza ni kuangalia usalama WA raia ingekuwa vita asingetizama uyu Nani wala Yule Nani na asingechukua mwezi mzima kuikalia Kiev Ukrein wanajitetea ndyo maana wanakuwa ata raia wao Kwa kisingizio cha usaliti
 
Ninachoweza kusema ni kuwa upo nyuma ya taarifa na pengine haukupata nafasi ya kukisikia kinachotoka mdomoni mwa Warusi wenyewe kuhusu kilichotokea na kinachoendelea Ukraine na wanachokifanya ni nini na malengo ni yapi!

Aidha, haukupata taarifa au ulikuwa nyuma kufuatilia kikao cha amani kuondosha ghasia inayoendelea nchini Ukraine baina ya Russia na Ukraine yenyewe. Miongoni mwa makubaliano ndiyo hayo yaliyofanya Russia kuondosha majeshi baadhi ya maeneo nchini Ukraine.
Option ya kuyachukua majimbo yanayopakana nae imekuja baada ya lengo la Kwanza kufail
Ninachoshauri itakuwa ni vyema ukifuatilia habari husika kutoka vyombo vya Russia vyenyewe. Matokeo ambayo kwako unaona wamefeli ila kwao yalishawekwa wazi.

Rejea kauli ya Putin siku anatangaza operation ya kuingia Ukraine utangulizi ulikuwa ni nini: Alitangaza kuyatambua majimbo yaliyojitenga nchini Ukraine. Alitangaza pia Russia imeamua kuyasaidia hayo majimbo kwa baraka walizopatiwa kutoka kwao ili kukomesha mauaji wanayofanyiwa na jeshi la Ukraine.

Kwa kufanywa hivyo kuna mambo yatafanyika kwenye operation hii muhimu ambayo inalinda usalama wa nchi ya Russia haikadhalika na usalama wa majimbo yaliyojiyenga. Hivyo, operation itakuwa ni demilitarize na denazification.

Phase ya 1 ilikuwa ni demilitarize ya jeshi la Ukraine ambalo kwa mujibu wa kwao tayari wameshamaliza hilo ambalo Putin alishalizungumza kwenye nukuu ya hotuba yake maneno niliyokuwekea.

Phase ya 2 ni kulinda usalama wa raia na mali wa hayo majimbo dhidi ya majeshi ya Ukraine. Bado majeshi ya Ukraine yapo humo kwenye hayo majimbo, hivyo ni kuyaondoa kabisa.

-Ukiyatizama kinachofanyika ni tayari Russia ama Putin alishakizungumza. Hakuna ambacho kilichofanyika kipo nje ya walichokitangaza Kremlin. Muhimu tufuatilie habari kutoka kwa vyombo vya habari vya Russia kwa kufanya hivi tutakuwa na a,b,c ya kilewanachokifanya ama kinachofanyika Ukraine kwa jeshi lao.
 
muvi zimekuharibu sana
 
Aim tangu mwanzo ni
Demiritarize na Neutralize.

Lkn ukitaka kujua Russia ni m bad sikiliza kile UN saa hii wanasema.
"Wamtoe kwenye UN human right. Yaani ni Katili . Hii ni kusema jeshi la Ukraine halukuweza ku defend watu wake i.e walilala yombo.

Mauaji haya mengi ya raia ZELENSKY ashitakiwe kwa kuhamasisha raia kwenda front na silaha wakati akijua hawana ABC za vita na wanakuwa target kwa kuwashambulia wale wa badman
 
Ila yale mataifa 30 yanayoungana yaliyoungana nayanayozidi kutaka kuungana ndio yana hio power uisemayo kuizidi hio RUSSIA
Ambayo wanaungana kwaajili yake
Tupe ama nipe sababu tano zinazofanya uione RUSSIA haina nguvu ukiilinganisha na VITA yeyote ile ambayo US alipigana nataifa lolote lile unalolijua ULIMWENGUNI
Ukinipa sababu kwamlingano wa US ambae ni SUPER POWER ntaungana nawe MKUU
 
@Aleyn kama hutamuelewa huyu bwana sidhanii kama utaelewa tena
Yaani hio OP watu walikua wanapewa muda wakujikomboa wakat kama ingekua VITA jamaa ingekua BOOOM 24/7 katika kipindi chote cha hii OP mpaka kufikia sasa nahuu uwezo kwa %100 RUSSIA yupo nao kama tuu angekua yumo VITANI
Siku mwana NATO mmoja ama hayo mataifa uloyataja hapo juu yajaribu kuingia VITANI na RUSSIA ndio ungeelewa na hili lingewezekana tu kama jamaa wangeeka NO FLY ZONE
Yaani hujajiuliza whY jamaa kalilia sana NO FLY ZONE ila NATO na SHOST yao US walikua wanagoma???@Aleyn
 


Mtaelewa tu, watakapomtundika jamaa yenu
 
"Mpaka unapoandika post hiyo Russia hana kifaru chochote Ukraine na magari yamepigwa yote"

Ukiambiwa unaandika kwa ushabiki itakua kukukosea heshima?

Air defense systems za Ukraine nyingi zimeharibiwa, wanajeshi wa Ukraine wamekua hawako frontline wanapigana kwa kujificha ficha wanatumia raia kama human shield

Tatizo sisi wachambuzi wa vita ni wajuaji tunafanya uchambuzi huku tumeegemea upande flani narudia tena kusema tujue kwamba Putin ni rais wa mojawapo ya nchi zenye taasisi imara sana ya kijasusi, nashangaa sana kusikia mashabiki wa vita wanasema upinzani putin anaokutana nao hakuufikiria wengine wanasema vikwazo ambavyo kawekewa this time ni vikubwa vitamshusha. Leo nani tena anaongelea vikwazo?

Tumekua brainwashed na hollywood movies tunaamini US anauwezo wa kila kitu ila jua kwamba US na nchi nyingine za ulaya zinazounda NATO wanajua uwezo wa Russia kivita vizuri kuliko sisi washabiki wa vita usione wanabwekea mbali hawajiingizi direct, unakumbuka NATO walisema hawaweki No fly zone pale Ukraine kwa sababu hiyo itakua ni kuichokoza Russia directly mpk leo hamna No fly zone.

Unakumbuka US alitaka Poland apeleke ndege vita ukraine ila poland akazipeleka kwenye base ya US kule ujerumani ili US azipeleke mwenyewe badae US alitoa kauli gani?

Suala la majeshi ta Russia kuondoka kyiv na chernihiv nashangaa mtu anasema wameshindwa vita wanaondoka hivi hata makubaliano ya mazungumzo ya last week waliyofanya mtu hajui ni nini waliafikiana juu ya kupunguza military operation maeneo hayo? Bado mtu huyo anachambua vita?

Vikosi vya Russia vilivyopo kwenye miji ambapo mapambano bado yanaendelea wana move kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa kutumia miguu?
 
Unaongea usi chokijua mkuu.russia hapigani na Ukraine ,pale anapigana na na Uk,US ,NATO na the like fans of United States.russia alijua tangu mwanzo kuwa marekani na fans wake lazma watapeleka msaada wa kijeshi Tena wakutosha ,so Russia alikuwa na 2 option in mind ,moja ikiwa marekani na fans wake wataogopa kupeleka military suport Ukraine Basi ampige zelensk na kumtoa on power na akabidhi power kwa mtu ambaye atakuwa humble kwa Russia ,au Kama US na fans wake wataingilia na kutoa support kimya kimya basi option ya kwanza anaachana nayo,na ajikite kumharibia kwanza Ukraine miundombino ya kijeshi lkn pia ,kulazimisha Ukraine kwa kipigo na hasara aliyoipata kuyasahau na kuachana na mpango wa kujoin NATO,pamoja na kusahau na kuachana na mpango wa kuyapigania majimbo Yale mawili ,ambayo ni majimbo muhimu Sana kwa Russia , for future plans .haya mqjimbo ni muhimu Sana kwa Russia hata zelensk anajua wazi haya majimbo ni muhimu kwa Russia kwa mipango ya baadae .

Kwenye medani ya kivita lazima ubalalqnce nguvu na skills,pasipo kuadhiri plans zako (ambitions).Japan kilichowagharim ni kuweka ambitions mbele zaidi ,bila kuweka balance ya skills & military power. Hata China ambitions yake kubwa ni kuitwaa Taiwan ,nguvu za kuichukua anayo ,lkn anajua impact ya kuharakisha kufanya hivyo na hapa ndo kubalnce skills na power ,pasipo kuadhiri ambitions yako. mkuu kwenye medani za kivita lzm uwe perfect kwa kila kitu,kule hakuna upumbavu wa kusema Mimi sio mungu mpaka niwe mkamilifu kwa kila Jambo [emoji23]. Kwenye medani ya kivita just a dot mistake u kill the whole plan!!!! Hitler alifeli kwa Hilo ,mistake moja na ndogo tu ya kumpuuza mrusi ,ika ua the whole plans!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…