Well said, umeongea kwa busara ukiweka ushabik pembeni. Ongera kwa hili chief.Pamoja na yote, tusi-underestimate uwezo wa kijeshi wa Russia. Ni miongoni mwa nchi zenye best missile systems katika masuala ya defense (nafahamu kuna debates mbalimbali kuhusiana na theoretical capabilities za silaha ukilinganisha na performance katika mapambano).
Pia, ni miongoni mwa nchi zenye share mkubwa katika uuzaji wa silaha kwenye soko la dunia.
Hata hivyo, hili suala la Ukraine limetia doa uwezo wao kwa kiasi fulani. Hilo ni kutokana na objectives walizojiwekea zikiwemo tunazozijua pamoja na nature ya vita ambayo wamekuwa wakipigana.
Nadhani niliwahi kusema awali mahali fulani humu kuhusiana na masuala ya muhimu katika kufanikisha malengo mahususi katika vita hasa zenye nature ya uvamizi (invasion).
Invasion lazima iwe na malengo ambayo yanapaswa kuwa achieved kwa gharama ambayo lazima ifanyiwe mahesabu yenye usahihi. Military strategy inapaswa kuzingatia movements sahihi za majeshi pamoja na anticipation ya kiwango cha upinzani kitakachotokana na adui. Hapa ndipo tunapoona utofauti kati ya "operation" na "campaign".
Kumekuwa na makosa ya kiufundi katika hilo kwa upande wa Russia. Resistance ya Ukraine imeonekana sana, pia kutokana na flow ya silaha kutoka nje. Objective kuhusu "de-militarization" kupitia jeshi haijaonekana kuwa achieved ipasavyo hadi sasa. Tusubiri tuone kama itaweza kuwa achieved kwenye mazungumzo yanayoendelea.
Hayo pamoja na masuala mengine ya kiraia kama 'local support' katika sehemu yenye uvamizi n.k. yanapaswa kuzingatiwa ili kutengeneza kitu kinachofahamika kitaalamu kama, technical feasibility, ambapo kwa case hii, pamoja na objectives tulizoambiwa, uvamizi haukuwa technically feasible.
Hapo unaposema kuwa ishu ya ukraine imetia doa uwezo wao kiasi flani naomba urekebishe kidooogo, sema kuwa kwa sehemu kubwa imetia doa. Kwanini?
1. Russia kupitia putin amekiri kupoteza Askar 1,300. Sasa kikawaida utaweza kujua tu kuwa hiyo namba sio rahisi kuwa sahihi, itakuwa ni kubwa tu. Na hapa sio russia pekee, hata ukraine lazima afiche namba.
2. Russia alizama Ukraine ndege zao zikianza kupepea sana, ikafika wakati Ukraine akaomba msaada wa anga. Mida huohuo pia alikuwa anaingiza gari nyingi na vifaru vingi ktk uwanja wa mapambano. Leo hii naandika hii post, Russia hana teeena vifaru vyovyote ndani ya Ukraine, mpaka magari yamepigwa yoote.
3. Russia anatumia long range missiles, hii ni kutokana na ndege na vifaru vyake kukwama Ukraine. Kwa taifa lenye teknolojia, sikutegemea kuona hivi. Sasa mimi najiuliza, kama Ukraine tu ameweza kumzuia jamaa hivi, vipi kuhusu Ufaransa na UK? Angeingia Israel je?
- Mwisho kabisa Russia ametupa wasiwasi mno kuhusiana na uimara wa vifaa vyake, tunaanza mtilia mashaka kama china. Ndo maana bidhaa za Ulaya na US ni imara mno, popote pale hawa jamaa wana products jiwe kulinganisha na mataifa mengine. Napata wasiwasi kuhusu zana za Russia. Ninaamini hata Putin mwenyewe anatamani kusuka hili jeshi upya tena.