Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Kutokana na vitisho vinavyotolewa na polisi dhidi ya haki za wananchi kutimiza haki zao kikatiba, ni wazi polisi wanaweza kuumiza watu hata kuua kwa kisingizio cha kuzuia maandamano.
Nashauri waandaaji wa maandamano kuandaa media coverage kubwa sana hasa kwa upande wa picha mnato na picha mwendo yaani video kwa kila tukio watakalolifanya polisi iwe hadharani au sirini.
Kamera za siri na vinasa sauti viwe vingi kukusanya ushahidi wa uhalifu unaotegemewa kitendwa na dola kama ule uliofanyika Mbeya. Waandamanaji wote nao simu zao kamera ziwe on kurekodi kila tukio la uvunjifu wa amani utakaofanywa na wenye mabavuna kisha kuliweka wazi ikitokea wahalifu wakaruka kimanga.
Kuandamana ni kutembea. Ninyi polisi shida iko wapi watu wakiachwa watembee huku wakiimba na kulia? Kunahitajika akili na busara badala ya mabavu.
Soma Pia: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea