Je, ulisoma vizuri na kuelewa comments zangu hizi:-
COMMENT YA KWANZA:-
1. What are the Motives for the demonstration?
2. What are the Goals that planned to be achieved at the end of the demonstration? What are the targets?
Inavyoonekana huko CHADEMA hakuna wataalamu au wanamikakati wazuri wa kuweza kupanga mambo Kama haya. Mambo mengi inavyoonekana huwa yanafanyika tu kiholela tena kwa kukurupuka bila ya kuwa na mpango dhabiti kwanza.
Mnapaswa kuwa wabunifu kwa kufanya kwanza utafiti wa kina, upembuzi yakinifu wa kina na Kisha mpange mipango na ajenda zenu vizuri zaidi ndipo mje kwa wananchi kuomba support yao ili waweze kuunga mkono mipango yenu na ajenda zenu. Mje kwa Wananchi mkiwa na Hoja zenye mashiko zinazogusa maslahi mapana zaidi ya umma, kwa kufanya hivyo, wananchi watajikuta wanalazimika kuwaunga mkono bila ya kulazimishwa. Hata kama Polisi watajaribu kuhujumu mipango yenu kwa Namna yoyote ile, automatically na wao watajikuta wanashindwa kuwahujumu kwa sababu kitendo cha kujaribu kuhujumu mipango yenu itakuwa ni kuwahujumu wananchi au kuanzisha vita dhidi ya wananchi.
Mimi binafsi nawashauri nyinyi Watu wa CHADEMA kwamba mjipange sawasawa kabla ya kuanzisha Jambo fulani, msiwe mnakurupuka.
Mwisho tambueni kwamba: Unapotaka kufanya Uamuzi wa Kudumu ni lazima uzingatie sababu za kudumu.
COMMENT YA PILI:-
Kwa taarifa yako, CHADEMA wanaweza wakawa na nia njema kabisa ya kutaka kufika mahali fulani, isipokuwa tatizo ambalo walilonalo ni kwamba wamekuwa wanakosea kupita kwenye njia sahihi ya kuweza kuwafikisha huko wanakotaka kwenda, they lack the right strategies to reach at their intended destination. Maandamano yenye positive impacts kwa jamii ni yale tu ambayo yamepangwa vizuri na kuratibiwa vizuri.
Narudia tena kusisitiza kwamba, muda wote unapotaka kufanya uamuzi wa kudumu basi ni lazima uzingatie sababu za kudumu.