Mifano ipo tu kwenye biblia
Kama king Solomon
Ubaya wa shetani akitaka kukudanganya huwaga anatumia maandiko hayohayo kwenye biblia
Mfano kama hivi
Shetani; “Ati Mungu alisema msile matunda ya mti wowote
Mwanamke; Mwanamke akamjibu huyo nyoka, “Twaweza kula matunda ya mti wowote bustanini; lakini Mungu alisema, ‘Msile matunda ya mti ulio katikati ya bustani, wala msiuguse, msije mkafa.’”
Shetani(nyoka); Hamtakufa! Mungu alisema hivyo kwa sababu anajua kwamba mkila matunda ya mti huo mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Basi, mwanamke alipoona kuwa mti huo ni mzuri kwa chakula, wavutia macho, na kwamba wafaa kwa kupata hekima, akachuma tunda lake, akala, akampa na mumewe, naye pia akala. Mara macho yao yakafumbuliwa, wakatambua kwamba wako uchi; hivyo wakajishonea majani ya mtini, wakajifanyia mavazi ya kiunoni.
MfAno mwingine ni huu [emoji116][emoji116]
Shetani: Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.”
YESU; Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’”
Shetani; Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza. Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu.
YESU; Imeandikwa: ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako, na kumtumikia yeye peke yake.
Shetani; Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini kwa maana imeandikwa: ‘Atawaamuru malaika wake wakulinde,’ na tena, ‘Watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa mguu kwenye jiwe.’”
YESU; Imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’
BASI NILICHOTAKA KUSEMA NI HIVI SHETANI AKITAKA KUKUPATA ATATUMIA KILA NJIA MPK HAYO MAANDIKO MATAKATIFU
HAO WATU UNAOWATAJA SIJUI WALIOA WAKE WENGI HATUANGALII MWANZO WAO TU TUNAANGALIA NA MWISHO WAO ULIKUWAJE
MFANO SULEMAN BAADA YA YOTE ALIONA NI UBATILI TU HAKUNA FAIDA ZAIDI YA HASARA
MHUBIRI 1:1-3
Maneno ya Mhubiri, mwana wa Daudi, mfalme katika Yerusalemu Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili. Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?
HUWEZI UKACHUKUA TABIA MBAYA ZA BAADHI YA WATU KATIKA BIBLIA HALAFU UKATAKA KUFUNDISHIA JAMII TUNAWAOMA WOTE HAO WALIKUWA NA HIZO TABIA WALIISHIA KUTUBU
SASA NDUGU YANGU KWA SABABU MUNGU ALIMUUMBA MWANAMKE NA MWANAMUME AKAWAPULIZIA PUMZI HAI WAKAPATA UHAI BASI NDOA NI YA MKE NA MUME MMOJA TU