Ushauri kwa wamiliki wa HILL WATER

Syntax ERROR

Senior Member
Joined
Jan 2, 2019
Posts
184
Reaction score
165
Habarini za Usiku ndugu Zangu poleni na Majukumu ya kazi ya wiki nzima huku tukisubiri bia za Bure kutoka kwa Konda boy

Nirudi kwenye mada, Hill Water mliingia vizuri sana kwenye soko mkapindua pindiua woote waliokuepo, mkawa nyinyi tuuuu, si masafi, si uhai, si Kili mkagaragazaaaa

Mmeongeza Tshs.100 tu kufanya 600, mmejiua Wenyewe, mmejizika, mtapotea kwenye soko, muulizen Uhai alipoongeza 100 ikawa 600 alijuta na Masafi ikatake over soko mpaka mkaja kuishinda.

Kuna mwingine kaingia sokoni CANADIAN PURE Tshs 500 tu, huyu atakua mzikaji wenu

Huu ni ushauri tu mnaweza kuuchukua au kiuacha

Usiku mwema


Naambatisha picha kwa maelezo zaidi
 
Watz sasa hivi tunaangalia being kwanza, maji AFYA, Lita 1 sh. 500 yananyweka kwenda mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I must be honest,hill water na io canadian ndo nmesizkia leo

Sent using Brain
 
hill wamejisahau wamepandisha bei watapotea si mda uswahilini mtu anaona bora masafi au afya 500
walikuja vizuri sana mwanzo pia usambazaji wao ni hafifu sana tofauti na masafi au afya au uhai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena Hill water yana ladha moja matata sana, nilipo karibu yangu kuna dada ni agent wao, ngoja nitamuuliza manake anapeleka balaa. Canadian kwa 500/- unapata lita moja na robo(1.25ltr), hapa nilipo watu wanakunywa sana Canadian.

Sent from my TA-1032 using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…