USHAURI: kwa wasioamini maswala ya time travel

USHAURI: kwa wasioamini maswala ya time travel

Labda ulimwengu tuliopo ni simulation, na time inaexist ndani ya hii simulation only. hivyo kuna sehemu ambazo zina glitch inapelekea ukifika hapo unakuwa kama upo nje ya simulation bila kujua. Na kama nje ya simulation hakuna time hivyo kila kitu hubaki kama kilivyo, ukirudi ndani ya simulation utakuta time inaendelea kama ilivyo.
 
Mate umetoa hitimishi bila hata kuweka facts about how it is possible, mimi ni muumini wa dhana hii ila mada yako na hitimisho lako halijitoshelezi.
No Einstein Rosen-bridge no time Travel...ungeenza kwanza hapo kuona ni jinsi gani tunaweza kutengeneza e.r.Bridge.
Point to ponder. unajua Gravity ndio kitu chenye spidi zaidi kuliko mwanga?
Time Travel: Je, linaweza kuwa suluhisho la kifo?
Time Heist and Time Apocalypse: Jinsi muda unavyoathiri Maisha ya ulimwengu na vilivyomo
Accoding to Kopeikin and Fomalont , but ukija kwa einstein gravity na light zina spidi sawa.
So upo upande upi? Maana umetumia concept ya einsteinian relativity kwenye part ya wormholes(einstein-rosen bridges) kumpinga jamaa kwamba haja time travel . Na kisha ukatumia pia concept ya kopeikin and fomalont ku prove kwamba gravity ina spidi kuliko mwanga .
 
kila nikiwaangalia vijana nyie wa 2020 nawashangaa sana yaan kitu kidogo kama hiki kinawasumbua mm nimetoka zangu mwaka 2600 nimerud nyuma mpaka mwaka 2020 ko msiwe na hofu ntaanza kuwapa some jinsi ya kufanya time travel🧐👻
 
Mmh mmenipa mwanga maana kuna mambo yalinitokea utotoni na sikufahamu maana yake na nikapewa na jina la potea kabisa wasababu wao wanadai nlipotea siku mbili na wakati ni masaa machache tu yalipita..ilikua hvi mwaka 2002 nilikua darasa la tatu wakati huyo shule ya msingi kawe A kila jumamosi mimi na mwenzangu mmoja tulikua tukishiriki kipindi cha watoto redio tumaini posta mpya st joseph kule...sasa basi tulikua tukiingia asubhi saa tatu kipindi kinaisha saa nne na kurud nyumbni kutoka posta kawe ni kama saa moja tu mwendo wa daladala hivyo nyumbani walitegema saa sita niwe nimerudi.. siku hiyo mimi na mwenzangu tuliamua kwenda kushangaa meli kubwa ya wa china iiyokuja pale bandarini siku hiyo.. tulifanikiwa kiungia ndani ya meli sikumbuki tulifanikiwaje maana tulikuwa wadogo tulishikwa mkono tu na wakubwa zety tulioongozana nao labda kwa kibali maalumu sikumbuki..sasa tulizunguka sana na kushangaa shangaa meli ilikua kubwa sana na bahati mbaya nikapoteana na wenzangu...nlikua nashangaa aquarym wenzangu kumbe wamshusha flo ya chini..niliwatafuta karibia meli nzim kuanzia saa sita mchana niko ndani ya meli mpaka saa moja usiku...nlipoona mlango wa kutokea nje nikaamua nitoke tu nirud nyumbani mana nlikua mkubwa kujielewa nlifika kituoni nikapanda daldala nafika nyumbani nakuta watu wameahatafuta kuanzia redio tumain kwenyewe mpaka kwenye meli nlipoachwa na wwzangu kwa siku tatu..naambiwa nimepotea siku tatu ilihali nlikuepo ndani ya meli lile kuanzia saa sita mpaka saa moja tu...nliambiwa taarifa hadi polisi imefika nlishindwa kujielewa nini kilitokea nikakubali nliptea siku tatu walivyosema wao but how ndio sielwi .. maana sikuchoka kutembea mule kwenye meli panda shuka wal kula na kunywa kitu chochote mpaka na toka nje kwa utoto ule nisngewza kukaa siku tatu bila kula na kunywa chochkte..pia nisingewza kutembea bila kupumzika mule ndani kwa siku tatu..nliishia kukubali tu lakini nilispend six hrs kwenye meli..na nje ilikua 3 days
 
I strongly disagree. You can't temper with three things TIME, SPACE & REALITY by any means. Kuna mengi tusiyoyajua kuhusu hivyo vitu vitatu.
 
Naomba niingie kwenye maada mojakwamoja,

Ni baada ya kupitia mijadala kadhaa ya kitu kinachoitwa time travel nimeona watu wengi wakipingana na hii kitu, mimi binafsi bila ya lengo ya kujinufaida na faida yeyote ile napenda nikupe shuhuda na kukuomba pia uamini na ufanyie kazi kuwa hii kitu IPO.

Nakumbuka wakati nikiwa mdogo huko kijijini kwetu (....) Mkoa wa pwani. "Kijiji kimezungukwa na mito, vichaka mabonde na misitu mikubwa.
Kulikuwa na kawaida ya kupotea kwa watu mara kwa mara huku imani ya wengi ikiwa ni wachawi ndo wahusika wa kupotea kwa watu. Na hii nahisi wenda si kijijini kwetu tu bali hata kijijini kwenu wenda kuna haka ka tabia ka kupotea kwa watu ila niseme tuu sio watu wote wanapotelea kwa wachawi ila baadhi yao ni time travel. kwanini nasema ni time tlavel iliwahi nitokea pia ilikuwa hivi;-
(Shuhuda ya kwanza)::;
mimi na vijana wenzangu tulikuwa tunakwaida ya kusaka wanyama wadogowadogo kwa kutumia mbwa. Siku moja shambani kwetu waliingia ngedere kama kawaida nikafungulia mbwa na kuanza kimbiza ngedere (tumbili) kimbiza yangu ikaishia kwenye msitu mdogo ulioko mbali kidogo. Nikafika mahali na kupumzika nakumbuka ilikuwa kama majila ya saa saba mchana kwendea saa nane nikakaa chini ya mti mmoja aina ya mtopetope na kuanza kula matunda ya mti huo. Hada kufika saa 11 jioni ndio safari ikaanza ya kurudi home ile nafika home napata taarifa kuwa nilikuwa nimepotea tena siku mbili na watu walishapiga mpaka nyanga.
nikaanza kuwaelezea na hakuna aliyeniamini kuwa nimetumia kama masaa manne tu hivi kuwa msituni wala sio siku mbili nikaenda shambani kuhakiki baadhi ya mazao waliyokuwa wameharibu ngedere siku ile ni kweli nilikuta ni mazao yaliyoalibiwa kama siku mbili zilizopita nyuma. Kwa wakati ule niliamini kweri wenda ikawa ni wachawi ila baada ya kufika JF na kukutana na hii kitu time travel. Imenifanya niamini kuwa hata hapa dunianibkuna maeneo ukifika ukitoka hapo unaeza ona umetumia dakika mbili ila ukitoka kwenye hilo eneo unakuta hata masaa saba yameahapita. Na hata kama unasaa ya kimwekumweku itakulazimu uilekebishe.
(Shuhuda ya pili)
Wakati nasoma pia shule ya msingi ilikuwa inanilazimu nilekebishe saa yangu kila ninapopita njia flani yaani saa yangu imekuwa imechelewa hata dakika tano na saa wenzie.
HITIMISHO
time travel ni yakweli na ipo na hata kuna baadhi ya maeneo hapa hapa ndani ya dunia.
Kwa maelezo hayo bas hai hitaji chombo chcht kusafiri ktk muda
 
Hivi ndoto na yenyewe ni time travel ama ni ability ya kuona future...??? Maana nakumbuka nilishawahi ona tukio kwenye ndoto na baada ya miaka kadhaa... Niliona tukio nilikuona exactly Kama lilivyokuwa kwenye ndoto...
 
Hivi ndoto na yenyewe ni time travel ama ni ability ya kuona future...??? Maana nakumbuka nilishawahi ona tukio kwenye ndoto na baada ya miaka kadhaa... Niliona tukio nilikuona exactly Kama lilivyokuwa kwenye ndoto...
Deja vu.. kinaitwa hivo hicho ulichokiona
 
Naona game tu hapa. Tena haya matukio ya kuona future ndo yana zihilisha hili ni game
 
Back
Top Bottom