Ushauri kwa watia nia wote wa ubunge -2025

Ushauri kwa watia nia wote wa ubunge -2025

Daraja2

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2017
Posts
285
Reaction score
346
Habari za jioni wapendwa,
Huu ni ushauri wa bure kwa wale (waliokwisha chukua & wanaotarajia kuchukua fomu na kuzirudisha).

1. Andaa "press conference" Moja matata sana nyumbani kwako chinja ng'ombe,pika chips,ndizi za kurosti na vinywaji vya kutosha ukiunganisha na pira biriani.

Wote watakaofika hapo ( vyombo vya redio & tv) wape posho ya 150,000 Kila Mmoja.

Eleza/ainisha changamoto za watanzania kwa ujumla na namna utakavyozikabili (kutoa afua Stahiki ) ikiwezekana ukiwa "mubashara"

Baadae anza kuchambua za Jimbo unalogombea katika nyanja zote ikiwemo namna ya kuboresha elimu,uchumi kwa mtu Mmoja Mmoja pamoja na kuondoa kero mbali mbali zilipo.

2.Tembelea wajumbe wote wa chama kuwapa "Hi" ukianzia mabalozi wa shina hadi wale wa wilaya ( ukiwapa 200,000 sio mbaya ,lengo ni kusalimia).

3.Tumia mabalozi wa mashina na wajumbe wa serikali za mitaa kukukusanyia wanachama wa "chama" kuwapa "Hi" na wenyewe ukiwaachia hata "50" sio mbaya pia.

4.Zunguka mtaani kwa mama lishe, vijiwe vya kahawa na kwa wenye changamoto binafsi wape msaada hata wa mawazo ikikupendeza ukiwaachia "50" sio mbaya.

5.Tembelea raia wa kawaida mtaani tatua changamoto zao na kubadilishana mawazo.

Yote haya rusha kwenye media mbali mbali ikiwemo
picha/picha mjongeo ulizowahi piga na wakubwa.

ANGALIZO;

Kama huna "hela" hakikisha hotuba utakazozitoa ( ikiwemo ile ya ufunguzi) ziwe nzito na kukupelekea misukosuko ya hapa na pale.

Kupitia hotuba "nzito" na misukosuko" itakutangaza zaidi kwa raia na kukuletea faida mbeleni (jambo hili lifanyike Sasa kabla ya uchaguzi wa ndani).

FAIDA;

1. Kugombea upinzani na kushinda.

2.Kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya na mamlaka.

USHAURI;
Hakikisha hotuba yako iambatane na " supporting documents" za "ukweli na uhakika" na ziwe za kujenga na sio za kubomoa.

Alamsiki.
 
Back
Top Bottom