Ushauri kwa watu ambao pombe zinawatesa na wameshindwa kabisa kuacha kwa kila mbinu.

Ushauri kwa watu ambao pombe zinawatesa na wameshindwa kabisa kuacha kwa kila mbinu.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
25,968
Reaction score
36,044
Kuna mbinu mbalimbali wanapewa watu ambao wanataka kuacha pombe.
Mfano wa hizo mbinu wanazopewa lakini mwisho wa siku wanarudi kulekule ni hizi.

1)Kupunguza kiasi cha unywaji.
Hapa ushauri wanaopewa ni kupunguza idadi ya pombe au siku za kunywa pombe.
Mfano kama alikuwa anakunywa bia 10 kwa siku apunguze angalau anywe sita, then 5 mpaka afike mbili.

Huu ushauri kamwe hauwezi kufanya kazi haswa kwa mtu yule anayependa kwenda kunywa sehemu za starehe, maana ili aendelee kuwepo eneo la tukio lazima atakunywa tena na tena.

2)Kukata urafiki na kampani ya wanywaji.

Hii nayo haiwezi kufanya kazi maana utakuta hao anaokunywa nao ni marafiki wake wa kushibana ambao wanashirikiana kwenye kila hali iwe furaha iwe huzuni na kubwa zaidi utakuta hao ndio business partners wake wakubwa na madili mengi wanapeana wakiwa wanakata kinywaji pamoja.

3)Kuombewa kanisani au misikitini.

Hii ni ngumu sana kufanya kazi labda huyo mnywaji awe amerogewa pombe, hivyo kupitia maombi kile kizuizi aj nguvu ya giza itaondolewa.

4)Dawa za kuacha pombe.
Hizi dawa zina madhara sana, na si wote zinawafaa wengine kweli wataacha ila wengine wataishia kupata matatizo ya kiafya hatimaye kufariki kabisa.

Sasa je suluhisho ni nini kwa hawa walevi wa pombe?

Suluhisho ni kubadili aina ya pombe unayokunywa.

Wengi wanaolalamika pombe inaletea madhara ni wale wanaokunywa pombe kali, mwisho wa siku wanakuwa na hangover ya mara kwa mara, sili zao kufeli, kugombana gombana hovyo, mahusiano kuharibika.

Sasa kama mtu ulikuwa unafakamia bia aina ya lager mfano Safari, Castle lager, achana nazo badala yake hamia kwenye lite.

Kunya castle lite, serengeti lite, kilimanjaro lite nk.

Uzuri wa hizi utakunywa kadri unavyopenda ila huto pata hangover, haitakutesa kwenye kula wala kuuuchosha mwili.

Pia kama ulikuwa unakunywa pombe kali mfano black and white, konyagi, hanschoice, kvang nk, hama huko kunywa zako bia.

Bia utalewa taratibu na utaona kabisa hapa nilipofika panatosha, tofauti ma hizo pombe kali zinalewesha ghafla ndani ya muda mfupi.

Pia kingine cha muhimu zaidi, pombe iendane na chakula na maji.

Kunywa bia tano kunywa maji, kabla kuendelea na bia zingine.
 
Kila mmoja huacha kwa wakati wake kinapomkuta kitu.
We tulia tu.

Witnesses will come one day.
 
Kuna pombe zingine mjini na uko vijijini mnalogwa na wenye hizo biashara pasipo wewe kujua ile ni biashara nikupe mfano ujawahi kwenda bar furani ukasema hapa napiga zangu mchesho bia mbili naenda kulala hapa nikitumia sana ni elfu kumi na tano tu na kweli unatumia hivyo hivyo hata kuwe kumechangamka vipi upati wazo la kuendelea kukaa hapo una maliza mchemsho wako bia mbili uyo unaondoka

Ila bar nyingine unaenda na hesabu hiyo ila galfa unashangaa mhudumu chukua na wewe moja wape na wale pale naona hobby zetu zinaendana bwana siye wazee wa zamani hii ndip miziki yetu unapigiwa sm nyumbani unajibu ondoeni hofu nakuja nakuja unashangaa saa saba usiku hii hapa asubuhi unamka umeacha laki na nusu bar

Na kila ukizishika pesa tu unawaza iende bar furani ukiwa huna kwakua wanakujua una kipato wanakukopesha unajikuta unaharibu utaratibu wa maisha yako pasipo kujua
Take care na sehemu unayokunywa pombe
 
Kila mmoja huacha kwa wakati wake kinapomkuta kitu.
We tulia tu.

Witnesses will come one day.
Na kwa nini mpaka usubiri upate madhara?

Dawa hapo ni kubadili pombe. Ukiona pombe kali zinakuchosha, unakuwa mgomvi mgomvi, mtu asiye eleweka, dawa ni kuanza kunywa pombe laini.
 
Kuna pombe zingine mjini na uko vijijini mnalogwa na wenye hizo biashara pasipo wewe kujua ile ni biashara nikupe mfano ujawahi kwenda bar furani ukasema hapa napiga zangu mchesho bia mbili naenda kulala hapa nikitumia sana ni elfu kumi na tano tu na kweli unatumia hivyo hivyo hata kuwe kumechangamka vipi upati wazo la kuendelea kukaa hapo una maliza mchemsho wako bia mbili uyo unaondoka

Ila bar nyingine unaenda na hesabu hiyo ila galfa unashangaa mhudumu chukua na wewe moja wape na wale pale naona hobby zetu zinaendana bwana siye wazee wa zamani hii ndip miziki yetu unapigiwa sm nyumbani unajibu ondoeni hofu nakuja nakuja unashangaa saa saba usiku hii hapa asubuhi unamka umeacha laki na nusu bar

Na kila ukizishika pesa tu unawaza iende bar furani ukiwa huna kwakua wanakujua una kipato wanakukopesha unajikuta unaharibu utaratibu wa maisha yako pasipo kujua
Take care na sehemu unayokunywa pombe
Hilo pia ni kweli.
 
Na kwa nini mpaka usubiri upate madhara?

Dawa hapo ni kubadili pombe. Ukiona pombe kali zinakuchosha, unakuwa mgomvi mgomvi, mtu asiye eleweka, dawa ni kuanza kunywa pombe laini.
Pombe laini eh! Sawa.😅😅
 
Back
Top Bottom